Ni vibaya binti kumnunulia baba yake boxer?

Ni vibaya binti kumnunulia baba yake boxer?

Kwani zawadi ni "NGUO" peke yake hadi uhisi wazazi wako watajisikia vibaya kwamba huwanunulii zawadi

ndio huwa nawapa cash but cash na kitu chenye thamani ni kitu..unakuta tuna tabia ukipenda wax unampelekea mama..sasa mama utampa wax na baba umwache? kwanini asipate shati ama trouser? uwezo wa kuwanunulia gari ama kuwajengea sina..uwezo.wangu wa zawad ni.vitu vidogodogo kama hivyo ndugu.
 
Mmh!sio wasukuma tu hata mie naona ajabu kumnunulia baba yangu boxer!pamoja na kwamba nimekulia mazingira ya mjini!sijawahi kufanya hivyo hadi sasa nimeshazeeka. Wala kufikiria kumnunulia baba boxer maishani sijawahi!
Au labda kwa kuwa nina kaka wengi!

nahisi basi mimi labda kwa vile tupo wa kike wengi maana tupo 5 wa kike na mdogo wetu wa mwisho wa kiume labda..ila kama ni vibaya sina budi kuacha mara moja na kumpa mama kwa siri ili baba asione.
 
kununua zawadi kwa wazazi ni kitu cha kawaida, endelea kufanya ivo ila kununua boxer kwa ajili ya baba yako hilo na mashaka nalo
 
kununua zawadi kwa wazazi ni kitu cha kawaida, endelea kufanya ivo ila kununua boxer kwa ajili ya baba yako hilo na mashaka nalo

nashukuru basi boxer ntaacha kabisaaa sitarudia tena..
 
Hata kama hujaolewa huwezi kumnunulia babako c.h.u.p.i bana.
 
mi imenishangaza..nikifikiria kumnunulia mzazzi zawadi boxer na vest hazijawahi kupita kichwani kwangu..hilo ni jukumu la mama..mie nitanununua vingine
Mmh!sio wasukuma tu hata mie naona ajabu kumnunulia baba yangu boxer!pamoja na kwamba nimekulia mazingira ya mjini!sijawahi kufanya hivyo hadi sasa nimeshazeeka. Wala kufikiria kumnunulia baba boxer maishani sijawahi!
Au labda kwa kuwa nina kaka wengi!
 
kamuulize mama yako kama kuna kitu si sawa atakwambia, achana na wanajf
 
anayekukataza kumnunulia boxer ni rafiki yako sio moyo wako.chakujiuliza ni huwa baba anafurahia zawadi zako? vilevile kumbuka kununua vya baba na Mama kwa pamoja huongeza upendo kwa wazazi wako.ni alama yakujali na kuonyesha uthamini.unalofanya linamfanya baba yako apate uamini kuwa wewe bado ni mtoto wake,bado huogopi kukaa juu ya mapaja yake kwa upendo anaamini wewe unamheshimu yeye kama Baba hata sasa.


keep it up.....wewe yule ni baba yako na kwake haukui dada angu hata ukiolewa bado ni mtoto kwake.anajua unafanya hayo kwa upendo wa mtoto
 
Na umesema pia shemeji yetu(mumeo) huwa anamnunulia mama yake nguo za ndani au sijaelewa? kama nimeelewa basi ni dharau kwa bi.mkubwa kabisa.
 
ila sasa mimi nimeolewa ndugu..baba pads alitununulia sana wakati.tunasoma tena sekondari..ile nliambiwa hain shida hata nlivofanya vile kabla sijaolewa..tatizo ni sasa nishaolewa eti baba hastahili zawadi.zangu.tena?

Kwa mawazo yangu me naona hakuna tatizo lolote
 
umnunulie babako boxer na mamako afanye nn?c bure kuna namna hapa.inamana ww unajua size ya kiuno cha baba ako kuliko mama ako anavyomjua.fanya ukafunzwe
 
Wana MMU naombeni msaada wa ushauri..
Kabla sijaoewa nilikua na tabia ya kuwanunulia wazazi wangu zawad mbalimbali..mfano nikimnunulia mama vitenge au makatalogi yaliyotoka baba nae humnunulia mashati, suruali, viatu, mikanda n.k nikinunua underware za mama na nguo nyingine za ndani bas na baba namnunulia vilevile boxerz, pants,vest n.k na huzipeleka kwa pamoja..walikua wameshazoea na kuzifurahia zawad..na nilifanya hivi kwa muda mrefu tu na nlikua sina ubaguz wa mzaz yeyote.wote wanapata.
baada ya kuchumbiwa pia sikuacha hata mchumba wangu aliona wakat nanunua zawad.hizo na wakat mwingine tunachagua wote nae akimnunulia.mama yake.

Baada ya.kuolewa sasa..siku moja nikanunua kama kawaida makadet na mashati pamoja na nguo za mama na wakwe zangu kama zawadi nikamwita mdogo wangu aje dukani kuchukua za wazaz wangu awapelekee.sasa rafiki yangu nliekua nae akanambia unafanya nini? unamnunulia babako nguo mpaka leo? wewe mke wa mtu acha mke wake (mama yangu) amnunulie! hutakiwi kumnunulia tena! mnunulie mama tu! mh na.maneno mengi tu aliongea yaliyonikatisha tamaa mpaka ikabidi nisitishe zawad hizo mpaka leo sijawahi tena kuwanunulia sio baba wala mama kwani naogopa kumpa mama bila baba kwani nilishazoea kuwapa wote.

Nauliza jamani;: kuna ubaya wowote kwa binti alieolewa kumnunulia baba yake zawadi kama nguo na nguo za ndani n.k?
sina amani najisikia vibaya kwani wazaz wangu wataona nimewatelekeza tangu niolewe hakuna zawadi tena..naombeni mnisaidie wale wenye uzoefu na haya mambo jamani.

Una juhudi naomba nikupe hongera kwa hilo tu
 
Nadhani zawadi si lazima iwepo boxer, waweza kununua vitu vingine na bado daddy yako akafurahi na kukupa kheri.

Ila swali kama hilo jaribu kumuuliza mama yako, kama yeye anaona ni sawa, unaweza kununua.
 
umnunulie babako boxer na mamako afanye nn?c bure kuna namna hapa.inamana ww unajua size ya kiuno cha baba ako kuliko mama ako anavyomjua.fanya ukafunzwe

hahahhaahahahahaah!!!!!! unaniua mbavu.
 
Zawadi zoteee sawa ila sio zinzolinda nyeti za mtu. Hapa ni lazima mhusika mwenyewe ahusike. Kwa mama bado unaweza kumnunulia. Nguo za ndani kwa baba zinaweza kuleta suala la research!
 
nashukuru basi boxer ntaacha kabisaaa sitarudia tena..

, mara nyingi jambo amabalo mtu hajazoea kulifanya huonekana geni na ala ajabu. ulishazoea kumnunulia mzee, endelea. ukiacha ataanza kujiuliza maswali mengi. kuna families ambazo baba kumbusu mtoto wake wa kike ni kawaida wakati wengine huona kama tayari wamezini.
 
Back
Top Bottom