Baba Mtu akifa anaweza kumnunulia mtu zawadi? Jifunze kitu kutokana na hii hadithi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,139
JIFUNZE KITU HAPA.jpg

Baba kwani mtu akifa anaweza kumnunulia mtu zawadi?? Lilikua ni swali kutoka kwa mwanangu wa miaka 5, nilistuka kidogo kwani alikua anazungumzia mambo ya kufa.

Ndiyo kwanza tulikua tumetoka kuzunguka Mlimani City kwaajili ya kuwanunulia wanangu watatu zawadi na tulikaa kidogo ili kunywa Juice kabla ya kurejea nyumbani. Nilimuuliza kwanini anasema hivyo lakini hakua tayari kunijibu, aliniambie nimjibu tu na kumuambia ?Hapana, mtu akishakufa hawezi kufanya kitu chochote.?

Nilimuona alivyo nyong'onyea na kila nilivyojaribu kumchangamsha hakuchangamka tena. Nilirudi nyumbani na kuanza kugombana na mke wangu nikimuambia ni kwanini wanangu wanazungumzia habari za kufa kipindi kile. Alisema hajui chochote lakini nilijua tu ni yeye tu kawajaza ujinga wanangu, nilikasirika sana na kila wakati niliwaambia wanangu wasiwaze chochote kwani Baba yao nipo na siendi popote.

Siku zilienda na sikukuu ilikuwa inakaribia, wanangu wote walikua na furaha kasoro Anna peke yake, ni yule ambaye aliniuliza kuhusu kufa, kila wakati nilipojaribu kumpa vizawadi na kumfurahisha alikua akiishia kulia tu. Sikujua anausmbuliwa na nini lakini nilihisi kuna kitu, mpaka wakati mwingine nilipogopa na kudhani kua labda kwakua ni mtoto kuna kitu kaoteshwa na maisha yangu yapo hatarini lakini niliziondoa hizo fikra.

Usiku mmoja nikiwa nimetulia chumbani Anna alikuja chumbani, mkononi alikua amebeba begi lake la shule, alikuja na kukaa kitandani, alikua analia, nilaicha kusoma Kitabu na kumkumbatia nikimuuliza tatizo ni nini, hakusema chochote zaidi ya kufungua Begi lake. Alitoa fungu la hela elfu mojamoja na miatano tano zilikua nyingi kidogo, bila kuzihesabu zilikua zinafika kama elfu hamsini hivi. Alinikabidhi zile hela, nilimuuliza kazipata wapi na kwanini ananipa ndipo akanijibu.

Nizakwangu Baba, nimekua nikikusanya Poket Money unayonipa na zawadi ili nikupe ukamnunulie Dada Jane nguo mpya, yeye Baba yake amefariki hawezi kumnunulia zawadi kama unavyotununulia sisi hivyo anakua anavaa nguo mbaya kila sikukuu.

Nataka umnunulie ili uwe kama Baba yake, mimi siwezi kumnunulia kwani
mimi si mwanaume siwezi kuwa Baba yake, yeye hana Baba?
Nilikuta machoazi yanaanza kunidondoka kama mtoto mdogo. ?Nimefanya nini?? Niliwaza. Jane ni mtoto wa kwanza wa mke wangu, alizaa na mwanaume mwingine kabla sijakutana naye na yule mwanaume kumtelekeza hivyo mke wangu alikua anamlea yeye mwenyewe. Ingawa hakumuambia hivyo lakini ni kama kila mtu alijua kuwa Baba yake Jane kafariki ndiyo maana alikuwa haji kumtembelea.

Baada ya kumuoa nilianza kuishi naye, ingawa mwanzo niliona itakuwa kawaida na nilikuwa nikimpenda Jane lakini baada ya mimi kupata watoto wangu niliwapenda zaidi, nilimtenga na kusema kweli sikumchukulia kama mwanangu, sikujua kama wanangu wanajua kwani muda wote nilikua nawapa kila kitu nawanunulia zawadi huku Jane nikimtenga. Mpaka pale Anna aliponipa ile hela ndiyo nilijua kua inawaumiza wanangu namna ninavyomtenga Jane.

Machozi yalinitoka uchungu nilioupata ulinifanya nijione kama mnyama. ? Hivi napata faida gani kumtenga mtoto wa watu asiye na hatia, huyu si Dada wa wanangu? Kwani ni shilingi ngapi kumpenda huyu Binti? Niliwaza mambo mengi bila majibu, nilikuwa katika lindi la mawazo mpaka Anna aliponistua?

Baba utamnunulia nguo Dada Jane? Nilimwambia ndiyo na kumwambia abaki na zile pesa nitamnunulia na pesa zangu.

Siku iliyofuata niliwachukua wanangu wote na mke wangu na ilikuwa ni siku ya kumnunulia mke wangu pamoja na Jane zawadi. Mke wangu alishangaa upendo nilimuonyesha Jane siku ile, Jane mwenyewe alishangaa kwani nilikuwa mtu mpya sana, alikuwa na furaha mpaka machozi, kila wakati alikuwa na wasiwasi, hata kuchagua nguo aliogopa aliposikia bei yake, hakujua nini kimetokea lakini nilimuaomba msamaha mke wangu na kumuambia Jane sasa nitakuwa Baba yake, sasa najiona mtu mwenye furaha zaidi.

Naamini mejifunza kitu!
Muda mwema
 
View attachment 2859064
Baba kwani mtu akifa anaweza kumnunulia mtu zawadi?? Lilikua ni swali kutoka kwa mwanangu wa miaka 5, nilistuka kidogo kwani alikua anazungumzia mambo ya kufa. Ndiyo kwanza tulikua tumetoka kuzunguka Mlimani City kwaajili ya kuwanunulia wanangu watatu zawadi na tulikaa kidogo ili kunywa Juice kabla ya kurejea nyumbani. Nilimuuliza kwanini anasema hivyo lakini hakua tayari kunijibu, aliniambie nimjibu tu na kumuambia ?Hapana, mtu akishakufa hawezi kufanya kitu chochote.?
Nilimuona alivyo nyong'onyea na kila nilivyojaribu kumchangamsha hakuchangamka tena. Nilirudi nyumbani na kuanza kugombana na mke wangu nikimuambia ni kwanini wanangu wanazungumzia habari za kufa kipindi kile. Alisema hajui chochote lakini nilijua tu ni yeye tu kawajaza ujinga wanangu, nilikasirika sana na kila wakati niliwaambia wanangu wasiwaze chochote kwani Baba yao nipo na siendi popote.
Siku zilienda na sikukuu ilikuwa inakaribia, wanangu wote walikua na furaha kasoro Anna peke yake, ni yule ambaye aliniuliza kuhusu kufa, kila wakati nilipojaribu kumpa vizawadi na kumfurahisha alikua akiishia kulia tu. Sikujua anausmbuliwa na nini lakini nilihisi kuna kitu, mpaka wakati mwingine nilipogopa na kudhani kua labda kwakua ni mtoto kuna kitu kaoteshwa na maisha yangu yapo hatarini lakini niliziondoa hizo fikra.
Usiku mmoja nikiwa nimetulia chumbani Anna alikuja chumbani, mkononi alikua amebeba begi lake la shule, alikuja na kukaa kitandani, alikua analia, nilaicha kusoma Kitabu na kumkumbatia nikimuuliza tatizo ni nini, hakusema chochote zaidi ya kufungua Begi lake. Alitoa fungu la hela elfu mojamoja na miatano tano zilikua nyingi kidogo, bila kuzihesabu zilikua zinafika kama elfu hamsini hivi. Alinikabidhi zile hela, nilimuuliza kazipata wapi na kwanini ananipa ndipo akanijibu.
Nizakwangu Baba, nimekua nikikusanya Poket Money unayonipa na zawadi ili nikupe ukamnunulie Dada Jane nguo mpya, yeye Baba yake amefariki hawezi kumnunulia zawadi kama unavyotununulia sisi hivyo anakua anavaa nguo mbaya kila sikukuu. Nataka umnunulie ili uwe kama Baba yake, mimi siwezi kumnunulia kwani
mimi si mwanaume siwezi kuwa Baba yake, yeye hana Baba?
Nilikuta machoazi yanaanza kunidondoka kama mtoto mdogo. ?Nimefanya nini?? Niliwaza. Jane ni mtoto wa kwanza wa mke wangu, alizaa na mwanaume mwingine kabla sijakutana naye na yule mwanaume kumtelekeza hivyo mke wangu alikua anamlea yeye mwenyewe. Ingawa hakumuambia hivyo lakini ni kama kila mtu alijua kuwa Baba yake Jane kafariki ndiyo maana alikuwa haji kumtembelea.
Baada ya kumuoa nilianza kuishi naye, ingawa mwanzo niliona itakuwa kawaida na nilikuwa nikimpenda Jane lakini baada ya mimi kupata watoto wangu niliwapenda zaidi, nilimtenga na kusema kweli sikumchukulia kama mwanangu, sikujua kama wanangu wanajua kwani muda wote nilikua nawapa kila kitu nawanunulia zawadi huku Jane nikimtenga. Mpaka pale Anna aliponipa ile hela ndiyo nilijua kua inawaumiza wanangu namna ninavyomtenga Jane.
Machozi yalinitoka uchungu nilioupata ulinifanya nijione kama mnyama. ? Hivi napata faida gani kumtenga mtoto wa watu asiye na hatia, huyu si Dada wa wanangu? Kwani ni shilingi ngapi kumpenda huyu Binti?? Niliwaza mambo mengi bila majibu, nilikuwa katika lindi la mawazo mpaka Anna aliponistua ? Baba utamnunulia nguo Dada Jane?? Nilimwambia ndiyo na kumwambia abaki na zile pesa nitamnunulia na pesa zangu.
Siku iliyofuata niliwachukua wanangu wote na mke wangu na ilikuwa ni siku ya kumnunulia mke wangu pamoja na Jane zawadi. Mke wangu alishangaa upendo nilimuonyesha Jane siku ile, Jane mwenyewe alishangaa kwani nilikuwa mtu mpya sana, alikuwa na furaha mpaka machozi, kila wakati alikuwa na wasiwasi, hata kuchagua nguo aliogopa aliposikia bei yake, hakujua nini kimetokea lakini nilimuaomba msamaha mke wangu na kumuambia Jane sasa nitakuwa Baba yake, sasa najiona mtu mwenye furaha zaidi.
Naamini mejifunza kitu!
Muda mwema
Ulikosea sana, ninachofahamu mimi wanaume hatunaga hizo roho mbaya za kike hasa kwa watoto
 
View attachment 2859064
Baba kwani mtu akifa anaweza kumnunulia mtu zawadi?? Lilikua ni swali kutoka kwa mwanangu wa miaka 5, nilistuka kidogo kwani alikua anazungumzia mambo ya kufa.

Ndiyo kwanza tulikua tumetoka kuzunguka Mlimani City kwaajili ya kuwanunulia wanangu watatu zawadi na tulikaa kidogo ili kunywa Juice kabla ya kurejea nyumbani. Nilimuuliza kwanini anasema hivyo lakini hakua tayari kunijibu, aliniambie nimjibu tu na kumuambia ?Hapana, mtu akishakufa hawezi kufanya kitu chochote.?

Nilimuona alivyo nyong'onyea na kila nilivyojaribu kumchangamsha hakuchangamka tena. Nilirudi nyumbani na kuanza kugombana na mke wangu nikimuambia ni kwanini wanangu wanazungumzia habari za kufa kipindi kile. Alisema hajui chochote lakini nilijua tu ni yeye tu kawajaza ujinga wanangu, nilikasirika sana na kila wakati niliwaambia wanangu wasiwaze chochote kwani Baba yao nipo na siendi popote.

Siku zilienda na sikukuu ilikuwa inakaribia, wanangu wote walikua na furaha kasoro Anna peke yake, ni yule ambaye aliniuliza kuhusu kufa, kila wakati nilipojaribu kumpa vizawadi na kumfurahisha alikua akiishia kulia tu. Sikujua anausmbuliwa na nini lakini nilihisi kuna kitu, mpaka wakati mwingine nilipogopa na kudhani kua labda kwakua ni mtoto kuna kitu kaoteshwa na maisha yangu yapo hatarini lakini niliziondoa hizo fikra.

Usiku mmoja nikiwa nimetulia chumbani Anna alikuja chumbani, mkononi alikua amebeba begi lake la shule, alikuja na kukaa kitandani, alikua analia, nilaicha kusoma Kitabu na kumkumbatia nikimuuliza tatizo ni nini, hakusema chochote zaidi ya kufungua Begi lake. Alitoa fungu la hela elfu mojamoja na miatano tano zilikua nyingi kidogo, bila kuzihesabu zilikua zinafika kama elfu hamsini hivi. Alinikabidhi zile hela, nilimuuliza kazipata wapi na kwanini ananipa ndipo akanijibu.

Nizakwangu Baba, nimekua nikikusanya Poket Money unayonipa na zawadi ili nikupe ukamnunulie Dada Jane nguo mpya, yeye Baba yake amefariki hawezi kumnunulia zawadi kama unavyotununulia sisi hivyo anakua anavaa nguo mbaya kila sikukuu.

Nataka umnunulie ili uwe kama Baba yake, mimi siwezi kumnunulia kwani
mimi si mwanaume siwezi kuwa Baba yake, yeye hana Baba?
Nilikuta machoazi yanaanza kunidondoka kama mtoto mdogo. ?Nimefanya nini?? Niliwaza. Jane ni mtoto wa kwanza wa mke wangu, alizaa na mwanaume mwingine kabla sijakutana naye na yule mwanaume kumtelekeza hivyo mke wangu alikua anamlea yeye mwenyewe. Ingawa hakumuambia hivyo lakini ni kama kila mtu alijua kuwa Baba yake Jane kafariki ndiyo maana alikuwa haji kumtembelea.

Baada ya kumuoa nilianza kuishi naye, ingawa mwanzo niliona itakuwa kawaida na nilikuwa nikimpenda Jane lakini baada ya mimi kupata watoto wangu niliwapenda zaidi, nilimtenga na kusema kweli sikumchukulia kama mwanangu, sikujua kama wanangu wanajua kwani muda wote nilikua nawapa kila kitu nawanunulia zawadi huku Jane nikimtenga. Mpaka pale Anna aliponipa ile hela ndiyo nilijua kua inawaumiza wanangu namna ninavyomtenga Jane.

Machozi yalinitoka uchungu nilioupata ulinifanya nijione kama mnyama. ? Hivi napata faida gani kumtenga mtoto wa watu asiye na hatia, huyu si Dada wa wanangu? Kwani ni shilingi ngapi kumpenda huyu Binti? Niliwaza mambo mengi bila majibu, nilikuwa katika lindi la mawazo mpaka Anna aliponistua?

Baba utamnunulia nguo Dada Jane? Nilimwambia ndiyo na kumwambia abaki na zile pesa nitamnunulia na pesa zangu.

Siku iliyofuata niliwachukua wanangu wote na mke wangu na ilikuwa ni siku ya kumnunulia mke wangu pamoja na Jane zawadi. Mke wangu alishangaa upendo nilimuonyesha Jane siku ile, Jane mwenyewe alishangaa kwani nilikuwa mtu mpya sana, alikuwa na furaha mpaka machozi, kila wakati alikuwa na wasiwasi, hata kuchagua nguo aliogopa aliposikia bei yake, hakujua nini kimetokea lakini nilimuaomba msamaha mke wangu na kumuambia Jane sasa nitakuwa Baba yake, sasa najiona mtu mwenye furaha zaidi.

Naamini mejifunza kitu!
Muda mwema
Naam, nimejifunza kitu , haswa kasisi tuliokuwa kwa mtindo kama wa jane.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom