ni ulimbukeni (UBOYA) kuwa na simu ya gharama.

ni ulimbukeni (UBOYA) kuwa na simu ya gharama.

Ninasikitishwa na ulimbukeni wa vijana hasa wa kibongo kutumia fedha nyingi kununua simu za gharama ili mradi eti kufanana na fulani au nae aonekane...unakuta kijana mwingine kapanga chumba hana hata hata stuli lakini utamkuta ana galaxy note! mbaya zaidi hata kutumia hawezi kila siku wanakuja kusumbua humu mara nimeilock oh mara siwez kufungua net...pumbavu kabisa iyo hela kwanini usinunue itel.. elfu 35 halafu iliyobaki ukachonga kitanda na meza pale geto kwako?

samahani mtoa mada,naomba kujua wewe unatumia simu ya aina gani na bei yake pia,ntarudi kukomenti.
 
Mtoa mada yuko sawa kabisa. kuna watu hawana kitu..na bado wanakaa kwa shemeji zao.. alafu wakati analaa kwenye kochi la shemeji yake.. ananunua simu ya laki saba..kwanini usipange chumba..unaendelea kulala kwenye kochi la mme wa dada yako..!
uza simu yako kapange chumba idiot!

laki saba ikiisha?!.unarud kwa shemeji na simu umeuza.
 
Ungeniuliza wakati nanunua gari nilikuwa nina hata hiyo leseni ya udereva... Nimemuelewa sana mtoa mada na ndiyo maana hili jukwaa linaitwa ....of Great Thinkers, usipoelewa vizuri unaweza kujikuta ukimpiga konzi hata mtu aliye upande wako....

We bwana acha kujitetea,kununua gari bila kuwa na leseni ni tofauti na muuza chips mtaji laki 2 simu ya laki sita,uza cm nunua ya elf 30 inayobaki ongezea mtaji wako,wenye ufahamu wataelewa tu.
 
we unajisikiaje una miliki simu ya mil 1 halafu huna uwezo wa kununua hata vocha unategemea kulegeza sauti ili urushiwe kifurush,...

hhahahaha! waambie hao 'wapenda vya kunyonga', vya kuachinja hawawezi....wana tabia kama za ndege jamii ya vultures....wao hawana uwezo wa kuwinda bali wanategemea kuzengea mizoga inayoachwa na simba. hahahahaha! wachane hao mademu wapendao vya dezo!!!!!!!!
 
Inavoonekana huyu fake ID ni masikini sana tena wakutupwa..anadhan mtu akiwa na simu ya laki8 anachezea ela,kumbe wenzake hyo n ela ya maji..
Watu wanahonga hadi range we unaonglea kumiliki simu za bei..
Kama mtu anaemiliki simu ya laki8 hana akili kazpataje hzo hela za kununua hyo smu..

Mkuu punguza stress acha watu waishi watakavyo bhana,kama we hauna ela go for Tecno..

Wewe inaonekana hujaelewa kabisa THEME ya huu uzi...hebu rudia tena kusoma upya huenda ukaokota angalau pointi 1!
 
Last edited by a moderator:
Simu ya maana ni mhimu na inabidi uwaze kwa mapana,ndo maana hata mitandao ya simu inatoa mb za internet,ukiwa na simu ya maana unaweza usiingie gharama ya kununua magazeti maana habari unazipata online au unaingia kwenye website la hilo gazeti unapata news,smartphones zina GPRS zinazosaidia usipotee njia au kuonyesha unapokwenda,ina ramani na kila kitu,ukiwa na simu kali hata haikuhitaji utumie gharama za kutuma msg unaingia tu whatsap unawasiliana na mtu bure kwa msg,ukiwa na simu ya maana unawasiliana na mtu bure kwa kufanya call kama unatumia viber au skype.

Hizo ni kwa uchache tu kwahiyo usiwadharau wanaonunua simu za gharama,unapitwa na mengi mkuu!

Mkuu, umei-miss pointi kidogo sana. Mtoa mada hawakatazi watu wenye uwezo kununua simu za bei kubwa...hoja yake ya msingi ni wale masharibaro (MABOYA) wanaoshindia mihogo na maji ya 100 na hawana fedha za kununua vocha, na wakati huo huo wanalala sebuleni kwa shemeji....lakini utajiri wao wote wameuelekeza kwenye manunuzi ya simu za bei mbaya. Hawa ndio walengwa wa mada hii. Na hapa tunajadili tabia za watu wa namna hii---Je, hayo mambo wanayofanya ni ujanja au ni UBOYA tu? Huu hasa ndio msingi wa mjadala huu. You get the point now? Haya, tuendelee na mjadala wetu bila kupepesa macho.
 
Vijana nmefanya skimming ya hoja zenu..na hii ndo concLusion ya pande zote mbiLi ili hii confrotation iishe' ni hiv ieleweke kwamba kila m2 anafanya kile anachojskia regardiness hakipo nje ya maadili ya jamii husika! Pia ifahamike hizo simu gharama watu wananunua kwa bei rahs tu kwa dark market mfano, simu ya laki 5 mtu anawezapata kwa laki 2 au hata pungufu! So ucsh2ke kuona m2 ana gallaxy s4 ukajua katoa milion dukan la hasha! Halafu pia ni wangap wanaokopa benk na kununua magar pas na kuwa na hata pakulala..ile hali inajulikana wazi kuwa MJINI HAKUNA BABA MWENYE GARI?


Mind yo biz..




Sent from my iPhone4 using JamiiForums
Mkuu, hii ni CONCLUSION au CONFUSION? Mbona hueleweki? Ina maana unasapoti wizi na usharobaro? Sijakuelewa bado.
 
Mleta mada ameleta thread nzuri ubaya amegeneralise watu wote. Nafikiri angeandika; watu wananunua simu ghali ambazo hawana uwezo wa kuzitumia. Ni kweli kuna kero sana kwa mtu hajui lugha ata kidogo, ananunua cmu na mwishowe ni kero kwa marafiki.kuna rafiki yangu ana simu kali, anatumia whatsaap,fbook. Juzi kataka kuandikia mtu kwenye face book. Kaenda google kaandika.......HI, MIMI DK NIKO FACE BOOK APA NAKUPA HI BEST. ujumbe huu ulinichekesha sana, simu ya elfu 35 inamfaa na haina makolokolo kibao kama simu nokia phantom. Mwenye uwezo na anajua kuioperate anunue lakini kama Huna uwezo usinunue kile usichojua kukiendesha la sivyo utaumbuliwa na simu

Asante sana mkuu, umelenga kwenyewe!
 
Si sahihi kwamba kila anayenunua simu ya 'gharama' ni limbukeni, na pili sijajua unatafsiri 'gharama' kuwa kiasi gani cha hela kwani hata tshs 1m inaweza isiwe gharama kwa baadhi ya watu.

Simu zina matumizi mengi na ya aina mbali mbali; na mtu hununua simu kulingana na aina yake ya matumizi. Kama simu ya shs 35,000/- inakidhi mahitaji yako basi usimsemee wa laki nane-hayo ndiyo mahitaji yake. Ujuzi wa kuitumia hiyo simu ni suala la maarifa; si kila mtu anajua kila kitu, hivyo usimlaumu anayeuliza.

Usipende kuwa mwepesi wa kulaumu; viwango vya maisha vinapishana kati ya mtu na mtu.

Mtoa mada hajaLAUMU bali ametoa ANALYSIS, tena kwa ufasaha mkubwa. Rudia upya kusoma uzi utamuelewa mtoa mada anachotaka kijadiliwe, usikurupuke!
 
Toka jana nimeshauri huu uzi uondolewe kwenye jukwaa hili, maana ni kuchanganya maharage kwenye pilau.

Kwa nini wewe usiende chitchat ukafungue uzi wako na watu watakufuata huko? Kwanini unataka kulazimisha uzi upelekwe unakotaka wewe? Omba kazi ya u-moderator basi.
 
Mtoa mada hajaLAUMU bali ametoa ANALYSIS, tena kwa ufasaha mkubwa. Rudia upya kusoma uzi utamuelewa mtoa mada anachotaka kijadiliwe, usikurupuke!

Nimerudia kuusoma uzi, naona hoja yako iko sawa na bado hoja yangu inabaki kuwa sawa pia. Nadhani umefanya haraka kuni'analyse'; ni suala la kukubali kukubaliana tu, basi!
 
Ninasikitishwa na ulimbukeni wa vijana hasa wa kibongo kutumia fedha nyingi kununua simu za gharama ili mradi eti kufanana na fulani au nae aonekane...unakuta kijana mwingine kapanga chumba hana hata hata stuli lakini utamkuta ana galaxy note! mbaya zaidi hata kutumia hawezi kila siku wanakuja kusumbua humu mara nimeilock oh mara siwez kufungua net...pumbavu kabisa iyo hela kwanini usinunue itel.. elfu 35 halafu iliyobaki ukachonga kitanda na meza pale geto kwako?

tatzo kila mtu na maisha yake so we anglia tu
 
Mkuu, umei-miss pointi kidogo sana. Mtoa mada hawakatazi watu wenye uwezo kununua simi za bei kubwa...hoja yake ya msingi ni wale masharibaro (MABOYA) wanaoshindia mihogo na maji ya 100 na hawana fedha za kununua vocha, na wakati huo huo wanalala sebuleni kwa shemeji....lakini utajiri wao wote wameuelekeza kwenye manunuzi ya simu za bei mbaya. Hawa ndio walengwa wa mada hii. Na hapa tunajadili tabia za watu wa namna hii---Je, hayo mambo wanayofanya ni ujanja au ni UBOYA tu? Huu hasa ndio msingi wa mjadala huu. You get the point now? Haya, tuendelee na mjadala wetu bila kupepesa macho.

ufafanuzi wako mzuri sana....kwa kweli watu wa aina hio ni MABOYA...nishakutana nao ndugu zangu,marafiki zangu sometimes unabaki unawaangalia tu kwa sababu ukiwaambia utapata reaction kama zinazopingana na mleta mada hapa JF.....unatamani kumwambia mtu si uuze hio simu upate hicho unachoomba!!!
 
ufafanuzi wako mzuri sana....kwa kweli watu wa aina hio ni MABOYA...nishakutana nao ndugu zangu,marafiki zangu sometimes unabaki unawaangalia tu kwa sababu ukiwaambia utapata reaction kama zinazopingana na mleta mada hapa JF.....unatamani kumwambia mtu si uuze hio simu upate hicho unachoomba!!!

Kila mtu mtu ana uhuru wa kuishi atakavyo, mi sioni jambo la kumuumiza mtu haopa...maisha ni kuchagua, kama DNA zetu zilivyo tofauti, lazima tutofautiane....huwezi mcorrect kila mtu aishi utakvyo ww....life is full of varieties yet God loves us all the way we are! Unless our actions do not anger him. I don't think if owning a fancy mobilephone is a sin. Please learn no to judge your fellow human for earthenly things.
The world is full of varieties bhaana....that makes life enjoyable.
 
Kweli masikini wanaongoza kwakununua vitu vya bei ya juu

Kabisa! hata Rais wetu jk licha ya kuwa anahudumiwa kila kitu na serikali lakini anatumia simu ya kawaida sana! tatizo letu tumekuwa wadandiaji tu, mtu anayenunua sim ya laki 7 wakati pato lake halifiki hata laki kwa mwezi atweje kama sio mshamba? sote tunapenda vitu vizuri ila tununue vinavyoendana na hali ya uchumi wetu.
 
Uzembe pia ni gharama, big up mtoa mada, wajinga wote hawatakuelewa,mi nina simu ya laki 2 inanitosha.
 
Back
Top Bottom