Ni ujasiri, uzembe au ujinga?

Ni ujasiri, uzembe au ujinga?

Kuna jamaa wengi sana wamekufa kwa ujinga wa namna hiyo.

Ajali moja ambayo naikumbuka vizuri ilikuwa maeneo ya Mamboya (Dodoma-Moro). Jamaa lori lao limepata tatizo, wakajipumzisha kama hao. Hakuna sign wala nini. Gari ndogo ikaja kutoka huko ilipotoka, ikabisha hodi humo uvunguni...hakuna aliyeomba maji, si kwenye gari ndogo wala hao waliojipumzisha.
Kweli mkuu, kabla ya kupiga hiyo picha nikawauliza hao jamaa kama hawaoni kuwa wamekaa kihasara hasara.
Wakanijibu ati mtu asiyeliona hilo lori ana matatizo!

Na kwa kawaida madereva zaidi ya asilimia hamsini ya waliopo barabarani wana matatizo!
Hao jamaa kama waliendelea na mtindo huu ni lazima hawapo duniani sasa.
 
Ujinga mwingine bhana! Ni kama huyo jamaa aliyemuua mama ufo then kumjeruhi ufo na yeye kujimaliza sipati picha nini faida ya ujinga kama huo?

Yaani hata mimi nimeshangaa kweli. Ule ni ujinga na huko aliko sijui anatoa maelezo gani dah.
 
Matingo na madereva wengi wana tabia hiyo. Tingo mmoja alifanya hivyohivyo pale Tunduma na matokeo yake walikuja na machepe kubandua mabaki ya mwili wake kwenye lami!
 
uwenda wazimu.....alafu mijitu kamaa hii inawatoto wengi kama kuku.
 
Back
Top Bottom