Ni ujasiri, uzembe au ujinga?

Ni ujasiri, uzembe au ujinga?

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,898
Reaction score
15,126
View attachment 116452
Hawa jamaa , dereva na utingo wake, wamepata pancha barabarani.
Katika kusubiri msaada toka kwa bosi wameamua kulala chini ya gari, na jeki yenyewe mchina.
No warning sign mbele wala nyuma, mi nasema ni ujasiri, wewe wasemaje?
 
Na ajali nyingi husababishwa na malori km hayo yanayoharibika na kupaki bila warning sign yeyote ile.
 
Hawana tofauti na " viongozi" wetu..

Chagua moja kati ya hayo ma 3
 
Ujinga mwingine bhana! Ni kama huyo jamaa aliyemuua mama ufo then kumjeruhi ufo na yeye kujimaliza sipati picha nini faida ya ujinga kama huo?
 
View attachment 116452Hawa jamaa , dereva na utingo wake, wamepata pancha barabarani.Katika kusubiri msaada toka kwa bosi wameamua kulala chini ya gari, na jeki yenyewe mchina.
No warning sign mbele wala nyuma, mi nasema ni ujasiri, wewe wasemaje?

Ukiona mpaka leo fiati kama hiyo iko barabarani ujuwe tajiri, wafanyakazi na serikali yao wote legelege!
 
Ujinga mwingine bhana! Ni kama huyo jamaa aliyemuua mama ufo then kumjeruhi ufo na yeye kujimaliza sipati picha nini faida ya ujinga kama huo?

Tatizo linaanzia serikalini, umiliki wa silaha siku hizi ni pesa yako tu!
 
Ni kutojua madhara ya wanachokifanya, na kufanya mambo kwa mazoea
 
Kuna jamaa wengi sana wamekufa kwa ujinga wa namna hiyo.

Ajali moja ambayo naikumbuka vizuri ilikuwa maeneo ya Mamboya (Dodoma-Moro). Jamaa lori lao limepata tatizo, wakajipumzisha kama hao. Hakuna sign wala nini. Gari ndogo ikaja kutoka huko ilipotoka, ikabisha hodi humo uvunguni...hakuna aliyeomba maji, si kwenye gari ndogo wala hao waliojipumzisha.
 
Back
Top Bottom