nadhani I will be the last person kusapoti muungano uliojaaa malalamiko yaliyopitiliza .....ht mke/mume akionekana haridhishwi na ndoa mliyofinga bora umuache tuu..maana ukijifanya kumbembeleza anakupotezea muda wa kufanya majukumu yako mengine...kila siku mtajadili kero..ukisovu moja anakuja na mpya..ooops .....kuungana na mlalamishi ni KERO Na upotevu wa muda......nadhani hkukufanyika research kabla ya maamuzi haya....ooops naboreka sana
mix with yours
Sidhani kama kuna mtu anaungangania Muungano, na hata ukiforce uwepo, unakuwa hujawatendea haki wasio utaka, hapa kinachozungumzwa, haki ifuatwe, maana isije ikawa wasitaka muungano ni wachache kuliko wengi wanaoutaka, hapa hoja ilikuwa iende kwenye bunge la JMT na hapo ndio wangeamua ama kuitisha kura ya maoni ama njia yoyote nyingine inayofaa kuupima huu Muungano na kama haiwezekani basi uvunjwe
hapo juu naona unazungumzia habari za ndoa, nadhani hata wewe ukitaka kuachana na mkeo/mmeo kuna utaratibu wa kufuata ili ijuliknae kuwa mmeachana, uwezi kukurupuka na kusema umemwacha mtu bila kufuata utaratibu (Usuruhishi na mwisho taraka)
Sidhani kama kuna mtu anaungangania Muungano, na hata ukiforce uwepo, unakuwa hujawatendea haki wasio utaka, hapa kinachozungumzwa, haki ifuatwe, maana isije ikawa wasitaka muungano ni wachache kuliko wengi wanaoutaka, hapa hoja ilikuwa iende kwenye bunge la JMT na hapo ndio wangeamua ama kuitisha kura ya maoni ama njia yoyote nyingine inayofaa kuupima huu Muungano na kama haiwezekani basi uvunjwe
hapo juu naona unazungumzia habari za ndoa, nadhani hata wewe ukitaka kuachana na mkeo/mmeo kuna utaratibu wa kufuata ili ijuliknae kuwa mmeachana, uwezi kukurupuka na kusema umemwacha mtu bila kufuata utaratibu (Usuruhishi na mwisho taraka)[/QUOTE]
hoja ya kukurupuka inatoka wapi?
mix with yours
... kwa sheria ya dual citzenship sijui itakuwaje
tunahitaji viongozi smart kama wakina Lincolin huko Marekani maana kama Lincolin angekuwa na hulka za Kikwete, i swear today Texas ingekuwa nchi huru! Nashangaa Kiwete yuko kimya!
Mengi yamesemwa hapa jamvini kuhusu huu Muungano na Katiba,
mimi nafikiri sehemu kubwa ya Watanzania walikuwa hawajazaliwa
wakati Muungano huu ulipoasisiwa tarehe 24 April, 1964.
Wengi wetu tumesoma katiba na maandishi kadhaa kuhusu Muungano
huu, wananchi wanahaki ya kujadili na kukarabati kwa kutumia wawakilishi
wao kwenye vyombo vya kutunga sheria kama wanaona kuna jamabo
la kurekebishwa kwa manufaa ya wengi.
Sioni tatizo kama wawakilishi walitumia nia ya dhati kurekebisha vifungu
vya katiba ya Zanzibar kama itawaletea manufaa Watanzania.
Tafsiri isitupotoshe muungano utakuwepo tu kwa miaka mingi ijayo, kwa
sababu huu haukuanzia tarehe 24 April 2010. ukisoma historia utaona jamii
ya Tanganyika na Zanzibar ilikuwa pamoja hata kabla mipaka kuwekwa
na wakoloni.
Tatizo jengine wengi humu jamvini hawajaisoma katiba ya Jamhuri ya muungano wa
Tanzania na ile ya Zanzibar lakini wanashabikia kiupofu upofu tu kama mchezo ambao
unachezwa lakini huelewi kanuni za huo mchezo iwe football, baseball, basketball, tennis,
golf kama huelewi nini kinachezwa huwezi hata kujua magoli au points zinapatikana vipi.
Tutenge wakati wa kusoma katiba zetu ili tukichangia tuwe na vitu vya maana vya kujadili.
Mkjj,
..toka 9th Dec 1961 na kabla hatujaungana na Zenj tulikuwa na Tanganyika yetu.
..wa-Tanganyika hatukuwa na tatizo kabisa kujivua utaifa wetu na kuungana na wenzetu wa-Zenj. tatizo ni kwamba ndugu zetu wa-Zenj wamegoma.
..kwa hali ilipofikia sasa hivi na huko tunakoelekea hatuna jinsi isipokuwa tu kukubaliana nao na kurudisha Tanganyika yetu.
..kama kuna wanaoona kuitwa wa-Tanganyika ni matusi na dharau, basi wapendekeze jina jipya la nchi yetu, lakini wa-Zenj wameamua kwamba hawatakuwa na sisi.
Wazanzibari muda mrefu wamekua wakitaka muungano ufanyiwe marekebisho na kero za muungano zitafutiwe ufumbuzi, lakini Watanganyika wemekuwa wakiwapuuza wazanzibari kwa muda wote ...Sasa mimi si shangai kuona wameanza kufanya yale ambayo wao wana weza bila ya Tanganyika... Hii kasumba tuliyokuanayo sisi ya kuwaona waZanzibari vijitu kidogo kwahiyo sisi ndio tuamue kila kitu mapaka nani awe Rais wa Zanzibar...Vukuto la kisiasa liko muda mrefu Zanzibar, mimi sishangai kuano tumefikia hapa... na kama tunataka ukweli ni kwamba option ya kujitoa katika muungano kwa upande mmoja wa muungano ilikuwapo tangu kuanzishwa kwa huu muungano...Sina haja ya kunukuua kauli za Nyerere nyinyi mnazielewa... Senegal na Gambia ziliungana na baadaya Gambia kuona inakandamizwa walijitoa katika muungano wao na Senegal aliokua ukiitwa SENEGAMBİA.... Hizi kasumba zimeshapitwa na wakati na mwenyewe Nyerere hayupo tena hapa... Kwanini tuishikilie Zanzibar wakati hapa Tanganyika hatuna lolote, Mtwara kunahitaji maendeleo na ni sehemu ya Tanganyika sio Zanzibar...:confused2:Kujaribu kuvunja Jamhuri ya Muungano kwa kisingizio chochote kile cha kisiasa ni uhaini. Mnaweza kutafuta kura na support ya wapiga kura lakini ukweli ni kuwa kuna nchi moja ambayo ni Jamhuri ya Muungano ambayo imetokana na kuungana kwa nchi mbili huru za Tanganyika na Zanzibar.
Jaribio la upande mmoja kuirejesha kinyemela nchi iliyokwisha ungana na nyingine ni kutangaza secession kutoka kwa Muungano na viongozi wote wanaopanga kufanya hivyo ni wa kutiwa pingu.
Sijawahi kufikiria kusema JWTZ liangalia ulinzi wa Katiba lakini wakati huu endapo mabadiliko yanayopendekezwa Zanzibar yatafanyika ni wakati wa kuwaangalia hawa "maadui wa ndani".
Ati wenyewe wamekaa kupitisha mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ili kipengele kimojawapo kisomeke hivi:
Wenyewe wanashangilia!! Lakini wanasahau kabisa waliapa kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema (msisitizo wangu):
na Magenius wetu hawaoni tatizo hapo: Je hii ni chemsha Bongo? Hivi ukisoma katiba hizo mbili utaelewa kuna nchi "ngapi"? Hivi hata hesabu za seti hawazielewi masikini wa Mungu au somo la mantiki linahitaji kufundishwa kuanzia darasa la kwanza?
Kama a. Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo "LOTE" la Tanzania bara na eneo "LOTE" la TAnzania Zanzibar, sasa Zanzibar ina ENEO GANI ambalo si sehemuya Eneo la Jamhuri ya Muungano? Kama seti moja inahusisha wanyama wote wa mwituni na seti nyingine inauhusisha simba na chui ambao nao ni wanyama wa mwituni, inakuwaje mtu anaanzisha seti nyingine inayosema "wanyama wa mwituni"?
Wanachezea maneno lakini maneno yana maana. Na miye natumia nasema kinachofanyika ni uhaini... (mnaweza kutafuta namna nyingine ya kulikwepa neno hilo). Lakini wataalamu wetu hawa hawa wanasahau Ibara ya 28:3 ya Katiba (waliyoapa kuilinda) inasema nini:
(
Halafu kama watu wasiojua Katiba wanasahau Katika ya Muungano inasemaje kuhusu wakuu wa mikoa. Katiba inasema hivi:
sasa magenius wetu wa Zanzibar wameamua kumnyang'anya madaraka Rais wa Muungano ya kushiriki uteuzi wa wakuu wa mikoa ya Zanzibar kama Katiba ya Muungano inavyotaka na kina Werema wamekaa na tai zao wanachekelea!
Sasa hawa wahuni wa Zanzibar wamepata wapi ujasiri wa kuridhia kuligawa taifa na kutengeneza nchi nyingine nje ya hii NCHI moja? Kuna njia moja tu ya kuunda Nchi ya Zanzibar- KUJITOA kwenye MUUNGANO. Nje ya hapo ni UHAINI!!!
I couldn't be more blunt than that.
Labda nikumbushie sehemu kidogo tu ya hotuba ya Baba wa Taifa kwenye Bunge lililoridhia Muungano Aprili 25, 1964 (msisitizo wangu):
Ooh how prophetic!!!
I'm standing on guard, by CHOICE!
Zanzibar sio sehemu ya Tanganyika na haitokua sehemu ya Tanganyika milele.... usitoe mifano ya kulinganisha Mbwa na paka...GU mbona unalinganisha tembo na sungura?? Kikwete si mtu wa kulinganishwa na hata dharimu Mgabe, yeye ni yes man ni mtu anayeogopa kuchukua maamuzi magumu (unpopular decisions). Mtu yeyote ambaye hawezi kuchukua maamuzi ambayo ni unpopular hafai kuwa kiongozi, inapotokea mtu huyo ni Rais wa nchi basi ujue ni tatizo kubwa kuliko tunavyoweza kuamini... Leo hii Wasukuma wakisema wanataka wawe na serikali yao ya jimbo (Mwanza, Shy, Tbr, na baadhi ya maeneo ya Mara na Kagera) Kikwete anaweza kuridhia kwa kuogopa kuwakosea!