bosi junius
umesema Mda huu tunahisabu tarehe tu kuifutilia mbali CCM Zanzibar,
vipi unataka uturudishe utawala wa chama kimoja?enzi zile zishapitwa na wakati bosi,upinzani lazima uwepo in order challenge the ruling party
Mzee hii inaonekana kama vile hawataki lakini wanataka. Vyao vyao lakini vyetu vyao pia. Muungano ukivunjika wapemba wote waliotapakaa huku tanganyika wafunge vilago waende kwao, sisi pia tutawakaribisha nyumbani wanyamwezi kidogo walioko huko na tutawapa pa kuishi na uchumi wetu ingawa si mkubwa utamudu tu. Hofu kwangu hao wanaoleta za kuleta itakuwaje???Suala la mali zao litenganishwe na uraia. Kuvunjika kwa Muungano hakutakuwa na maana kuwa raia wa nchi moja hawawezi kuishi katika nchi nyingine. Raia wa Zanzibar ataweza kuishi, kufanya kazi au biashara Bara kama raia mgeni mwengine yeyote na haki zake zitakuwa hivyo hivyo. Wapemba wa namanga watakaotaka kutambulika kama raia wa Zanzibar wataendelea ni lazima waruhusiwe kuendelea kuishi Bara kama wanataka ili mradi wakitimiza masharti ya uhamiaji. Watakuwa kama raia wa Kenya n.k. wanaoishi Tanzania hivi sasa. Na wanyamwezi walio Zanzibar wanaotaka kubaki na uraia wa Bara navyo hivyo hivyo. Haki yao ya kuishi Zanzibar kama raia wageni ni lazima ilindwe. Na kama wakati huo tutakuwa na uraia wa nchi mbili basi wanaotaka wanaweza kuwa na uraia wa Bara na Zanzibar. Yote haya yawekwe wazi wakati wa kampeni kuhusu Muungano. Wananchi lazima waelewe maana ya kuvunja Muungano na namna gani itakavyo-affect maisha yao ya kila siku. Safisha safisha itatokea kama Muungano utavunjika kwa mabavu kama ilivyokuwa Yugoslavia. Mbona Czechoslovakia hapakuwa na hiyo safisha safisha?
Amandla.........
Mzee hii inaonekana kama vile hawataki lakini wanataka. Vyao vyao lakini vyetu vyao pia. Muungano ukivunjika wapemba wote waliotapakaa huku tanganyika wafunge vilago waende kwao, sisi pia tutawakaribisha nyumbani wanyamwezi kidogo walioko huko na tutawapa pa kuishi na uchumi wetu ingawa si mkubwa utamudu tu. Hofu kwangu hao wanaoleta za kuleta itakuwaje???
thats exactly the point.. kila mtanzania au kundi la watanzania watakaoona kuwa Muungano hauwapi manufaa wanayotaka wajitenge. Hivi watu wa Kigoma (na wameshawahi kusema hili) wakisema Muungano hauwanufaishi au Tanzania Bara haiwanufaishi tutawabishia? Vipi kuhusu watu wa Mtwara na Lindi (nao wameshawahi kusema hili) wakisema kuwa Muungano hauwanufaishi na wangependa kuwa sehemu ya Msumbiji au kutangaja kijamhuri chao tutawaambia wanasema uongo au tutawakubalia ati kwa sababu muungano hauna manufaaa "kwa pande zote"? Hivi watu wa Chunya wananufaika vipi na Muungano? Watu wa Nansio, Mkongo na Duga wananufaika vipi na Muungano?
Hivi Wamarekani wote wananufaika na muungano wa US? Na wote wanafuraha?
Ndio maana nilisema wabongo tunapenda mambo mepesi mepesi!
@Mkandara, nimependa take yako.. thats whatsup!
Mbona viongozi wa Zanzibar hawathubutu kutamka wazi wazi kuwa hawautaki huu muungano... wanacho kiogopa kitu gani...!?
Wanaoleta za kuleta ni hao wapemba waliozagaa huku,, kama hawataki muungano waende zao nasi hatuwataki! waende huko wanakoona kutawafaa.Wapemba na Wanyamwezi wataamua uraia gani wachukue kwani si lazima kuondoka!! Na wazanzibar wameona EAC itawasaidia ku-maintain mambo yao bara!
Mkuu nadhani nitatofautiana nawe ktk hili. Maudhui ya kuhoji Muungano ndiyo yanayokera watu kama mimi. Na siwezi kufananisha Muungano na dini kwa sababu dini ni Imani ya watu na Muungano unatokana na kutengeneza mazingira safi kwa jamii inayoungana. Hivyo tunaposhindwa kuelewa kwamba lengo kuu la Muungano ni kuunganisha WATU na swala la nchi ni kuyaweka Maingira yetu ktk hali ya kudumisha Umoja huo.
Sasa kama kuna mtu anahoji Muungano ambao ni wa WATu kwa kisingizio cha mipaka au nchi atueleze vizuri kumekosekana kitu gani kuufanya Muungano huu wa WATU usiwe imara..Nina hakika hakuna kati yao anayeweza kuzungumzia matatizo ya muungano kwa kigezo cha haki za wananchi wenyewe tofauti na Dini ambazo watu wanahoji haki na freedom ya waumini.
Ikumbukwe tu kuna thin line kati ya haki na freedom na abusive of the certain rights. Kila sheria inayohusiana na haki au freedoma za binadamu ni ktk kuleta USAWA baina ya wahusika wote na sio UTENGANO baina yao kuwa ndio right kama inavyoiombwa pasipo sababu zaidi ya kutumia mipaka ya ramani za mkoloni.
Mimi siepndi kabisa malumbano ya Muungano zaidi ya kuwatazama wananchi wenyewe na kero zao. Kero zote za Muungano zimetokana na Uongozi uliopo na wote hawa ni wanafiki wakubwa. Nakujmbuka Ni Karume aliyekubali Muungano, kisha alitaka kuuvunja baada ya kuondokana na kina Abrahman Babu. Muungano kwake ilikuwa kuhakikisha maradaka yake hayapati upinzani kama alivyofanya Nyerere kuua vyama vingi bara.
Kisha akaingia huyo Aboud Jumbe kuserve Muungano lakini ajabu ya Mussa naye akataka kugeuka na ya Firaun huyu Seif ndiye aliyepinga m,awazo ya Jumbe na kuwatonya kina Nyerere. Leo hii yeye ndiye mpiganaji maarufu hali hawa woote mwanzoni walipokuwa ndani ya serikali ya Muungano hawakutaka kabisa kusikia kuvunjika kwa Muungano lakini wanapokuwa nje ya madaraka ndio kelele zao zinaposikika.
Maadam wamelianzisha wao kuhusiana na Muungano nadhani sisi wananchi tunatakiwa kuwauliza wao maswali muhimu kwetu ktk kuvunjika kwa huu Muungano. Je, wataweza vipi kuunganisha jamii hizi mbili na kwa njia zipi za kudumu ambazo sisi wananchi tunazikubali kwani kesho kesho kutwa tunaweza kufukuzana mipakani tukitumia katiba hizi mpya wanazotunga wao leo hii.
Sisi hatuyataki hayo na hatua za kuyaondoa ndiyo hizo tushaanza kuzichukuwa...CUF ipo ikulu...we do'nt have to wait for another saviour...he has already come. Mda huu tunahisabu tarehe tu kuifutilia mbali CCM Zanzibar, inayolea muungano wa kidhalimu...ambao hatuutaki.
mkandara
mjadala mkuu unahusu uhaini wa zanzibar kama ulivyoletwa na mwanakijiji, tuujadili huo, tusiende pembeni sana
sawa baada ya yooote hayo uliyosema, swali rahisi tu linakuja hapa, je nchi ni nini? Na serikali ni nini? Halafu je zanzibar ni nchi ama si nchi? Kama jibu ni zanzibar ni nchi, je ina mipaka au haina? Kama inayo je ina haki ya kuitangaza na kuilinda au haina? Kwa kila jibu lako eleza kwanini?
MKKJ,
Nina wasi wasi kuna mtu kavamia ID ya Mwanakijiji, na anaongea kama mlevi, anapayukwa payukwa tu, hatujuwi hasa anasimama na hoja ipi na ipi ana kataa. Tunaomba kama kuna mtu kaivamia ID ya Mwanakijiji atupe nafasi...asimtie aibu...mwenyewe kwa maongezi yasiyoeleweka eleweka.
Hapo juu kwenye post 113 unakataa kuwa hujawahi kusema Zanzibar lazima iwe kwenye muungano...wakati thread yako inakusuta kwa kauli za "tutaulinda kwa gharama yoyote", "jeshi lichukuwe hatua" n.k...na jazba,chuki na nongwa kwa Wazanzibar unaiyonesha wazi wazi kwa sababu tu kwa umoja wao wamekubali mabadiliko ya muundo wa serikali yao na hadhi yake katika muungano.
Mkuu unayejiita Mwanakijiji(siye yule ninayemfahamu kuwa mtu muelewa wa mambo), inaonyesha neno "jamhuri ya muungano" kwa kiswahili cha kusini ya Tanzania linamaanisha siku zote "nchi moja", unasahau neno kama 'muungano' linaashiria kitu zaidi ya kimoja, kwa muktadha wetu ni nchi/jamhuri mbili ambazo ni Tanganyika na Zanziabar.
Mabadiliko tuliyoyafanya wazanzibar wengi wetu (wahuni, maadui kama ulivyotuita) ni kuainisha tafsiri sahihi ya neno "jamhuri ya muungano" ambao ni wa nchi mbili ambazo kabla ya 1964 kila moja ilikuwa na "jamhuri" yake.
Kinachokufanya uwashwe sijuwi nini tena. Acha jazba na chuki zako kwa wazanzibar, sisi si mazuzu kama nyinyi sisi tuna njaa ya mabadiliko ya kweli si ya vitabuni, nyinyi endeleeni kuabudu CCM na mizimu ya muasisi wake,sisi tushatoka huko,hatutaki kurudi tena...mnaibiwa rasilimali zenu, mnanyanyaswa na kudharauliwa na watawala halafu hao hao mnawachaguwa kwa kishindo.
Sisi hatuyataki hayo na hatua za kuyaondoa ndiyo hizo tushaanza kuzichukuwa...CUF ipo ikulu...we do'nt have to wait for another saviour...he has already come. Mda huu tunahisabu tarehe tu kuifutilia mbali CCM Zanzibar, inayolea muungano wa kidhalimu...ambao hatuutaki.
tatizo wanafikiri kuwa tunazungumza kutoka hewani tu ati tunaitakia Zanzibar mabaya; kama mazungumzo ya watu wawili leo hii (karume na seif) yamechukuliwa kuwa halali na kukumbatiwa yale ya wa Nyerere na Karume nayo yalikuwa na nguvu hiyo. Wazanzibar hawawezi kuwa na keki yao halafu waile huku wabakie nayo. Kama kuna watu Zanzibar wanataka kuwa nchi "nje" ya Muungano, waliseme hilo, kama ni kupigwa kura ipigwe na tuanze mahusiano baina ya nchi mbili.
But as long as we are a United Republic jaribio lolote la kuivunja ni uhaini - as simple as that.
Ni jukumu la kila Mtanzania (yes wapo watu wa taifa hilo) kulinda Muungano ulivyo. Hatupaswi na hatuwezi kuachii kikundi cha watu wachache kuivunja ati kwa sababu hawajisikii. Wazanzibari ambao wanajitambua kuwa ni Watanzania na wapo wengi ni lazima wakatae uhuni huu.
Kama Zanzibar haitaki kuwa ndani ya Muungano kwenye baraza la wawakilishi waseme hivyo mapema, wajitangaze kuwa wanataka kutoka nje ya Muungano na nina UHAKIKA Kikwete na uongozi wa CCM hakuna atakayeweza kujenga hoja za kuzuia kwani mashujaa hao hawapo tena. Basi watoke na kama nilivyosema tuanze uhusiano wa nchi mbili, binafsi wala sina tatizo kabisa. Lakini kama wanataka tuwe wamoja kama nchi ni lazima mpango wao wa kuitangaza Zanzibar kuwa ni nchi sijui madudu gani ukemewe mara moja na KILA MTANZANIA.
Si kwa sababu hatuwezi kuishi bila Zanzibar au wao bila sisi, bali kwa sababu MUUNGANO UPO na ni lazime utetewe kwa gharama yoyote. Kwanini Zanzibar wasipige kura ya maoni kutaka kujua kama wanataka kubakia ndani ya Muungano?
PIGENI HII KURA TUMALIZE MZIZI WA FITINA!!!
viNGINEVYO NI UHALIFU ULIOKUBUHU AMBAO ADHABU YAKE NI KIFO! Uhaini haurembuliwi macho.
DAH! huyu MWKJJ ni mtu khatari sana kwa maendeleo ya wa zenj, alijaribu kuwakumbusha wa znj mambo yaliyo pita ili wazenj wasiungane akashindwa, leo wa zenj wamekua wamoja anawaita wahaini, anamawazo yakizamani kwa kweli ana akili mbaya, akili ya kikoloni,anshawishi vitu vya ajabu kweli. kama umri wako unazidi miaka 80 si shangai ikiliyako itakuwa imesha choka, lakini kama chini ya 50 matamanio maovu yasikutawale
Is this the home of great thinkers, or is the botomless Pit of rubbish Spiters?? Someni bandiko la mwanakijiji na kuingia kwenye mjadala kama mko fiti kwenye Historia na Filosofia. Nyie mnaoshabikia Zanzibar kujitenga ina maana nyie (wanyakyusa,Waha, Wanyamwezi, wabarabaig, wanyia, na wengineo) mna mahusiano ya karibu na Wazaramo na wangindo na wandengereko kuliko makabila hayo yalivyo na ukaribu na wazanzibar?
Hivi kabila la Mzee Karume Mnalijua??!!