tatizo wanafikiri kuwa tunazungumza kutoka hewani tu ati tunaitakia Zanzibar mabaya; kama mazungumzo ya watu wawili leo hii (karume na seif) yamechukuliwa kuwa halali na kukumbatiwa yale ya wa Nyerere na Karume nayo yalikuwa na nguvu hiyo. Wazanzibar hawawezi kuwa na keki yao halafu waile huku wabakie nayo. Kama kuna watu Zanzibar wanataka kuwa nchi "nje" ya Muungano, waliseme hilo, kama ni kupigwa kura ipigwe na tuanze mahusiano baina ya nchi mbili.
But as long as we are a United Republic jaribio lolote la kuivunja ni uhaini - as simple as that.
Ni jukumu la kila Mtanzania (yes wapo watu wa taifa hilo) kulinda Muungano ulivyo. Hatupaswi na hatuwezi kuachii kikundi cha watu wachache kuivunja ati kwa sababu hawajisikii. Wazanzibari ambao wanajitambua kuwa ni Watanzania na wapo wengi ni lazima wakatae uhuni huu.
Kama Zanzibar haitaki kuwa ndani ya Muungano kwenye baraza la wawakilishi waseme hivyo mapema, wajitangaze kuwa wanataka kutoka nje ya Muungano na nina UHAKIKA Kikwete na uongozi wa CCM hakuna atakayeweza kujenga hoja za kuzuia kwani mashujaa hao hawapo tena. Basi watoke na kama nilivyosema tuanze uhusiano wa nchi mbili, binafsi wala sina tatizo kabisa. Lakini kama wanataka tuwe wamoja kama nchi ni lazima mpango wao wa kuitangaza Zanzibar kuwa ni nchi sijui madudu gani ukemewe mara moja na KILA MTANZANIA.
Si kwa sababu hatuwezi kuishi bila Zanzibar au wao bila sisi, bali kwa sababu MUUNGANO UPO na ni lazime utetewe kwa gharama yoyote. Kwanini Zanzibar wasipige kura ya maoni kutaka kujua kama wanataka kubakia ndani ya Muungano?
PIGENI HII KURA TUMALIZE MZIZI WA FITINA!!!
viNGINEVYO NI UHALIFU ULIOKUBUHU AMBAO ADHABU YAKE NI KIFO! Uhaini haurembuliwi macho.
of course.. hilo wala siyo hoja; wakitaka watangaze tu kuwa wanataka kutoka nje ya Muungano, wadai kile wanachokiita ni "uhuru". Kikwete awaruhusu kwa sababu sidhani kama ana uwezo wa kuzuia Zanzibar kutoka nje ya Muungano. Na ninaamini guess what will happen:
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar watatoa hoja ya kutaka kutoka nje ya muungano na kupendekeza kura ya maoni kwa Wazanzibar wapige kaa wanataka kubakia ndani ya Muungano, hoja hiyo italetwa NEC (musoma au dodoma) CCM hawana watu wa kuutetea Muungano wetu na watasema endeleeni kupiga kura na mkishinda basi tunaachana "salama"..
Hili LITATOKEA! Kwani baada ya kuiweka Zanzibar kuwa ni nchi na mipaka yake kama ilivyo kwenye mabadiliko haya, kitakachofuata ni kujiuliza "je nchi yaweza kuwa sehemu ya nchi nyingine?". JIbu haliepukiki ni HAPANA.
OOH HOW I PITY THAT DAY!!
Zanzibar ilianza kujitenga mapema tu pale walipo taka wimbo wao wa Taifa wakaja na bendera yao na hii nilihisi ingekuja kufikia hapa maana kipindi wanatengeneza wimbo wao wa Taifa (Zanzibar) ilitakiwa kpindi kile Mkapa akemee hilo but aliwaachia wakafanya kile watakacho ikaja wakatengeneza bendera ya Taifa (Zanzibar) sasa wamekuja na katiba kinachofuata itakuw ukitaka kwenda kwao (Zanzibar) unaomba visa halafu watadai nao wawekwe kwenye EA Community kama Kenya,Uganda, Rwanda na Burundi.
Uhaini ni neno zito. Sidhani kama wamefanya yote haya bila wenzao wa Bara kuwa na habari. Kinachonitatiz mimi ni hii dhana ( ambayo kwa bahati mbaya na wewe unaiendeleza) kuwa Muungano ni sacrosant na wenye uamuzi nao ni wazanzibari peke yao. Naamini wakati umefika wa kufanya walichofanya wenzetu wa Canada na Czechoslovakia walipojikuta hapa tulipo. Ipigwe kura ya maoni (referendum) pande zote za Muungano (Bara na Zanzibar) na iwapo pande zote mbili zinataka Muungano uendelee basi uendelee kama ilivyokuwa Canada. Kama upande mmoja ( Bara au Zanzibar) ikipinga basi tutengane kwa amani kama ilivyokuwa Czechoslovakia. Kulazimishana kutaweza kutugeuza Yugoslavia nyingine. Ni kwa referendum peke yake ndipo tutajua kama kweli kuna wazanzibari na watanzania bara wanaotaka Muungano uendelee. Huku kupulizia wakati wanauma lazima kuishe.
Hii nchi ni yetu sote na ni lazima sote tuulizwe. Tunaweza kushangaa hapo watakapokuta kuwa machogo nasi hatuutaki Muungano! Huku kutingisha kiberiti lazima kuwe na mwisho wake. Hii imani ya kuwa tuko tayari kuulinda Muungano kwa gharama yeyote ndiyo inayowapa kiburi. Watapojua kuwa hatuko tayari kumwaga damu kwa kitu ambacho ni figment ya imagination pengine watasita kabla ya kufanya upuuzi huu. Wasitugeuze Spain na Catalanya!
Amandla.......
mzee kama Bara watataka ( na mimi ni mmoja wao ambao nataka tuendelee kuungana) na Zanzibar hawataki tutafuta matakwa ya nani na kwanini?
Halafu wakishajitenga (assuming ndiko tutakakoishia) uraia wa Zanzibar utakuwa vipi na wa Bara utakuwa vipi kuhusu Wazanzibari walioko Bara na wa Bara walioko Zanzibar?
Kama Bara watataka na Zanzibar wakikataa basi tutengane kwa vile Muungano hautakuwa na ridhaa ya wahusika.
Kama Bara wakikataa na Zanzibar wakitaka basi napo tutengane kwa sababu zile zile. Tuendelee na Muungano pale tu watu wa Bara na Zanzibar wote wakonyesha kuwa wanautaka.
Hatutakuwa nchi ya kwanza kutengana. Ikiwa USSR waliweza ( hata bila referendum) kwa nini sisi tuogope?
Kuendelea na Muungano wakati upande mmoja hautaki utatufikisha kubaya.
Mfano hai ni Yugoslavia. Mwingine ni Belgium ambayo mpaka sasa haitawaliki.
Ni lazima tuwe majasiri kama walivyokuwa Canada na Czechoslovakia. Mbona pamoja na kelele zao Quebec walisita walipoambiwa kama unataka kuondoka nenda na RoC?
Raia wa Tanzania ya sasa watachagua uraia wanaoutaka kutokana na makazi. Wenye asili ya Zanzibar walioko Bara watachagua kama wanataka uraia wa Bara au wa Zanzibar. Vile vile wenye asili ya Bara walioko Zanzibar nao wachague uraia wanaoutaka. Pande zote mbili zilazimishwe na jumuia za kimataifa kuhakikisha kuwa wananchi wake hawanyimwi haki ya kuchagua uraia wanaoutaka bila unyanyasaji wa aina yeyote. Masharti ya uraia yawekwe wazi na yafuate misingi ya haki za binadamu inayotambulika duniani kote.
Amandla........
Na suala la mali zao? Na wale ambao wako Zanzibar lakini wanataka kutambulika kuwa ni raia wa Bara watafanywa nini na vice versa? Isije ikaanza kampeni ya kusafisha safisha.. like somewhere we know..
Suala la mali zao litenganishwe na uraia. Kuvunjika kwa Muungano hakutakuwa na maana kuwa raia wa nchi moja hawawezi kuishi katika nchi nyingine. Raia wa Zanzibar ataweza kuishi, kufanya kazi au biashara Bara kama raia mgeni mwengine yeyote na haki zake zitakuwa hivyo hivyo. Wapemba wa namanga watakaotaka kutambulika kama raia wa Zanzibar wataendelea ni lazima waruhusiwe kuendelea kuishi Bara kama wanataka ili mradi wakitimiza masharti ya uhamiaji. Watakuwa kama raia wa Kenya n.k. wanaoishi Tanzania hivi sasa. Na wanyamwezi walio Zanzibar wanaotaka kubaki na uraia wa Bara navyo hivyo hivyo. Haki yao ya kuishi Zanzibar kama raia wageni ni lazima ilindwe. Na kama wakati huo tutakuwa na uraia wa nchi mbili basi wanaotaka wanaweza kuwa na uraia wa Bara na Zanzibar. Yote haya yawekwe wazi wakati wa kampeni kuhusu Muungano. Wananchi lazima waelewe maana ya kuvunja Muungano na namna gani itakavyo-affect maisha yao ya kila siku. Safisha safisha itatokea kama Muungano utavunjika kwa mabavu kama ilivyokuwa Yugoslavia. Mbona Czechoslovakia hapakuwa na hiyo safisha safisha?
Amandla.........
Mkuu usirushe changa la macho mchana kweupe ili kuficha nia ya kuvunja muungano.Utaifa muutetee nyie, wakitetea wengine makosa! Ama kwa hakika nyani haoni makalio yake.
Binafsi napima hili suala la muungano ktk muono wa kiuchumi, achana na falsafa na hizo sarakasi za katiba, maana katiba yenyewe haimlindi yeyote zaidi ya tabaka twawala la mazuzu wa huko bara. Katiba inasema muizi akiiba apelekwa jela, kiongozi wenu Dr. Mkwere anasema walipe lakini wasiguswe..(na hakuna utrhibitisho kama wamelipa na hamna anayethubutu kuuliza)! sasa usitake kuniambia huoni priority hapa ni nini?
Muungano haujawasaidia lolote waznz kiuchumi na hali zao zinakuwa mbaya siku hadi siku, huku mazuzu wa huko bara wakizidi kujineemesha. Sasa sioni kwanini waendelee kuwakumbatia mawakala wa ukoloni kutoka bara wakati hawana msaada wowote. Its time to call the quits, and try something better.