Ni ufisadi wa Spika Samwel Sitta

Upuuzi mtupu, MOD tuondolee hii kitu hapa, majungu pelekeni kwenye vikao vya mafisadi
 
Upuuzi mtupu, MOD tuondolee hii kitu hapa, majungu pelekeni kwenye vikao vya mafisadi

haya mambo mbona hayaishi, vitu kama hivi visipewe nafasi hapa JF majungu hayajengi
 
kwa kweli mimi naomba unihakikishie haya uliyoyasema, maana ni mazito sana, halafu jinsi ninavyomjua spika, kidogo napatwa na shaka, ngoja kwanza nitafakari kwa kina, ila ahsante kwa kuniweka bayani na habari hii
 
nadhani hamjui juu ya hayo myasemayo, kuna mamlaka zinazo husika kuidhinisha hizo pesa na kama ni kweli hao ndio wezi na so spika, acheni kupika majungu, leteni ushahidi ; kwangu hizo ni porojop tu,
 
kwa hiyo sasa hivi Spika kafanikiwa kugeuza kibao na yeye dio anaonekana victim!

duh!

bongo kiboko
 
nadhani hamjui juu ya hayo myasemayo, kuna mamlaka zinazo husika kuidhinisha hizo pesa na kama ni kweli hao ndio wezi na so spika, acheni kupika majungu, leteni ushahidi ; kwangu hizo ni porojop tu,

Mtui nakuunga mkono kwamba haya tunayosuhudia hapa ni majungu. Mwandishi hajafanya uchambuzi wa kutosha kubainisha mtiririko wa matukio. Na kubwa zaidi, ufisadi unaotaka kuanikwa hapa mbona ni kiwango kidogo sana ukilinganisha na EPA, Richmond, Kagoda, Kiwira etc.. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!!!
 
Nami naunga mkono ni majungu tu haya tumeshasikia sana juu ya hili na nafikiri we are fed up with stories without any direction. we need to discuss serious issues sio majungu tu ya watu hapa. I said yesterday that some contributors in this forum are not to be trusted and they are biased towards certain groups in the ruling party.
 

Ni kiwango kipi cha ufisadi tunapaswa kuvumilia?Nikidhani kuwa hakuna ufisadi mdogo wala mkubwa.... wote ni mbaya tu na unapaswa kupigwa vita.
 
Ni kiwango kipi cha ufisadi tunapaswa kuvumilia?Nikidhani kuwa hakuna ufisadi mdogo wala mkubwa.... wote ni mbaya tu na unapaswa kupigwa vita.

Mimi naona kama ufisadi wa Spika unataka kukuzwa ili kumudhoofisha Spika na kufanikisha kuufunika ufisadi mkubwa anaopambana nao. Magnitude ya tukio ni muhimu kuzingatiwa.
 


Safi sana nangetwa!! Kwani kuna jipya hapa ukilinganisha na utovu wa nidhamu wa viongozi wetu wa juu ambao hawana maadili kabisa??? Mbona wapo waandamizi wengi ambao wana vimada lukiki kushinda hivi vilivyotajwa hapa???? Hebu jaribuni kudondosha mafuska yaliyopo katika ngazi za juu tudondoshe vimada vyao hapa kama list haitakoma!!!! Hizo ni personal weakness zake ila anaziweka pembeni na anachapa kazi. Ingekwa kweli serikali hasa ile tume ya maadili ya viongozi iko serious na nidhamu basi tabia kama hizi zingekomeshwa tangu awali. Sasa wakimua kukomesha viongozi wenye vimada leo hii nani atabaki????!!! Tume ya maadili ilifumbia suala la ufuska kwa viongozi na sasa wavune walichopanda!!! Inatia aibu sana pale unakuta jiongozi lina wadhifa mkubwa kwa jamii na linapigania vichangu na vijana au kuweka vi-mitresses kila kona, bila kusahau Dodoma ambako ndiko vikao vingi vya chama na serikali vinafanyika!!!! Tuwe serious!!!


Ufisadi huu wa kuwa na vimada na kuhudumiwa na magari ya serikali upo kwa asilimia kubwa ya viongozi wetu, na huu wa kiongozi mmoja Spika hauwezi kamwe kulinganishwa na ufisadi wa Richmond, IPTL, Meremeta, Tangold, Deep Green, Kiwira, Kagoda, you name all. Kummaliza kisiasa Sitta imeanza muda sana, tangu Bunge la awali na hasa pale aliruhusu moto wa Richmond kuwashwa na kuruhusu uundaji wa kamati, famously known as Kamati ya Makyembe!!! Na kiongozi asiye mzinzi ndani ya serikali yetu basi na asimame hadharani tumwone!!! Hakuna atakayesimama!!!

Iliyobakai tumuunge mkono Mh. Sam Sitta kwa uchapakazi wake. Na ninakuhakikishia kama Sita atakoma uspika hatutaweza kumpata Spika mwingine ambao atalifanya Bunge active and live bila woga!!!! Hakuna, labda ipite muda sana!!! Mtu akitishiwa nyau basi anaogopa, ndivyo tulio wengi. Naamini Sitta hujaogopa Nyau na ataliendeleza Libeneke kama kawa.
 
Wakuu,

Nimekuwa nikifuatilia mjadala huu kwa makini, lakini ukweli ni kwamba ufisadi ni ufisadi tu, hauna udogo! Msisahau pia nyumba ambayo Spika Sitta, tumeambiwa, amepangiwa ya USD 8,000 (TSh. Milioni 10) za walipa kodi kwa mwezi na kuipuuza nyumba yake aliyopewa zamani, akisema siyo hadhi yake; samani za Tsh. Milioni 250 kwa hiyo nyumba mpya ya kupanga; gari la kifahari analolitaka la aina ya Mercedes Benz la TSh. Milioni 300 linalonunuliwa na Ofisi ya Bunge na kuliona la sasa halifai! Hoja hizi Spika alishindwa kuzijibu Bungeni na badala yake akaomba ulinzi wa askari zaidi wa usalama, vimulimuli na mapikipiki, kama vile yeye ni Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu!
LAKINI tatizo la mzee huyu la fitina na usaliti wa kisiasa, halikuanza leo! Katika miaka ya mwanzoni ya 1990, akiwa Waziri wa Sheria (na baadaye akaondolewa, baada ya kushindwa Ubunge wa Urambo), alishiriki "kiujanjaujanja" katika hoja ya kutaka kuleta Serikali ya Tanganyika katika mfumo wa Muungano, ili uwe wa Serikali Tatu badala ya Mbili.
Katika kitabu chake, UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA. Uk. wa 20 hadi Uk. 27, Mwalimu Nyerere alimsema vibaya sana Sitta, kwa kupeleka mbele ya Halmashauri Kuu ya CCM, Dodoma, "TAARIFA YA SERIKALI JUU YA AZIMIO LA BUNGE KUHUSU HAJA YA KUUNDA SERIKALI YA TANGANYIKA NDANI YA MUUNDO WA MUUNGANO". Mwalimu Nyerere alisema, kuhusu taarifa hiyo, katika kijitabu hicho: "Taarifa yenyewe ni ndefu, maana ina maelezo mengi ya mapambo tu, au ya kiinimacho(Uk. 20)...Baadaye, baada ya kikao, nilimtafuta Ndugu Sitta, nikampa pole kwa kupewa jukumu la kueleza jambo ambalo halielezeki (Uk. 27)...". Huyo ndiyo Spika Sitta, mbele ya macho na fikra za Mwalimu Nyerere! Hivi ni mpiganaji kweli wa vita dhidi ya "Ufisadi", au ni msaliti tu wa Chama chake? Wana-CCM na msio wana-CCM na ni Watanzania tu wenye nia njema, pimeni!

Bwassa
 
Mungu atusaidie...aliye juu ataki kushuka chini na wa chini anataka kupanda juu!!!
Kuna kamati imeundwa kumchunguza SS, tuipe muda tupate yaliyo kweli.
 
mimi najua Bwana bwassa anatumikia kina nani? anaangalia gharama za kujenga au ku furnish nyumba ya spika wa bunge la jamhuri ya muungano??/ je alikuwa na mpangpo wa kujiuzia nyumba hiyo kama alivyofanya yule ndugu yangu wa Umeme pale ubungo? au alikuwa anataka kuibinafsisha kama Rais mstaafu alivyofanya Kiwira na nyumba kadha za Serikali? Bwassa acha hizo labda useme wewe umenunuliwa kwa shilingi ngapi tu. Mkapa alitumia fedha nyingi kukarabati Ikulu wala hatukusema maana aliimwachia mwenzie wala hakuichukua, hivyo hivyo hakuna tatizo kubwa kwa bwana six kukarabati nyumba ya spika. uspika wenyewe unaisha mwakani, na washirika wa bwassa mmepania kutokumrudisha bungeni na uspika atausikia kwenye bomba tu.
 

Mwenye Akili zake anajua fika umesimamia wapi. Hela zinazidi kumwagwa na mafisadi mwenzetu basi tupatie na sisi lakini hatutaungana na wewe katika propaganda ya siasa za maji taka unazozifanya hapa JF
 


Mkuu asante umenena. Halafu wajue kuwa ofisi ya spika huwa ina kitengo cha utawala ambacho kipo responsible kuona kuwa boss wao anaishi a descent house, wamejiwekea standards na status!!! Waliamua kumlipia nyumba hiyo na ya dola 8,000!!! kwa kufanya contract na mwenye nyumba. Leteni mkataba wa hiyo nyumba kama amesaini Mh. Sitta!!!! Kama ni malalamiko ya matumizi ya spika waulizeni wahusika wa maintainance ya spika na stahili zake nyingine!!! Ulisikia wakilalama kuwa spika kawa-influence katika kupanga matumizi yake ya ofisi na stahili nyingine?? Acheni madongo. Ndiyo ukubwa huo!!! Mnamwonea wivu???

Kuna viongozi waandamizi ambao wana stahili lukuki za spika ndogo?!!!! Halafu pia kazi ya spika ni sensitive anahitaji nyumba na ulinzi mkali!!! Unafikiri kupambana na mafisadi ni mchezo, kuendesha zile fikra pale kwenye mjumba kwa vikao vyote ni mchezo, anatumia akili ya hali ya juu tena yaneya kujibu haraka sana. Mzee namkubali, ana majibu, hakurupuki kama wale wa kikaoni juzi cha tarehe 16-17 August, 2009!!! Waswahill hao wa uswazi!!!??? Kama ni mchezo jaribu kuwa mchezaji!!!??? Ndiyo ubosi huo mazee!!! unatamanisha eeeeeehhhh!!! Acheni wivu. Ex-Fisadi kudos.
 
FISADI NI FISADI TU. Hapa hakuna kuangalia chama, cheo. Hata kama aliwaumbua mafisadi mbona hajajiumbua yeye mwenyewe. CAG anafanya kazi yake kwa mujibu wa sheria sio kuangalia kama wewe unapambana na mafisadi au la. Waache waandishi waendelee kutuhabarisha. Uzania siyo kumbe NDIYE.
 
Nzee Busara asante kwa info lakini ni outdated hata nimeshindwa kuelewa ni vp iko hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…