Ni tuhuma tu Lowassa kumbe si Fisadi!!

Ni tuhuma tu Lowassa kumbe si Fisadi!!

Allen ntake radhi. mi sipo huko. labda wewe. ila ni bora tum support Magufuli kwa utendaji wake. chadema asilia wote tupo huko. tumewaacha chadema maslahi muendelee nayo
Kigezo gani unatumia kujiita CHADEMA asilia, maana inaonekana kama vile kuna haki fulani umejipa ya kuwa na uasili wa chama kitu ambacho kwa sisi wengine tunaona unawaya waya tu!!
 
Ndugu Yangu, ili kutetea uamuzi wa Chadema kumsimamisha Lowasa kuwa mgombea uraisi mwaka jana inabidi ujitoe ufahamu, huu ndiyo ukweli japo hamtaki kuukubali.
Mimi nina akili zangu timamu na bado natetea uamuzi wa CHADEMA kumsimamisha Lowassa kwani nyie mnaosema walikosea hamsemi ni athari gani kama chama wamepata. Kama CHADEMA imeathiriwa kwa kuwepo kwa Lowassa hii mikiki mikiki ya kuizuia isifanye siasa inatoka wapi?
 
Ambatanisha na lile gazeti la Kubenea, kiwa jamaa hasafishiki hata kwa dodoki.
Kigezo cha kutosafishika kwa mawazo yako wewe ni kipi? achana na Kubenea, au wewe ndiyo wale wenye akili za kushikia mpaka wengine waseme na wao ndiyo wajue?
 
Wewe aliyekwambia kuwa kumbe lowassa sio fisadi ni nani?? Kwa nini unasema kumbe?? Ni nani amesababisha aitwe fisadi mpaka wewe sasa hivi useme kumbe?? Ebu niambie hapo nani kashikiwa akili.
 
Mahakama ndo yenye wajibu wa kuthibitisha?

Kanuni ya wapi hiyo?

MKUU KAWEKA ALAMA YA MSHANGAO(!), HAMAANISHI MAHAKAMA IDHIBITISHE(AMESHNGAA),
NIVIZURI KUELEWA HOJA YA MWENZIO USIJIBU KAMA HUJAJUA LUGHA ALIYOTUMIA
 
Wewe aliyekwambia kuwa kumbe lowassa sio fisadi ni nani?? Kwa nini unasema kumbe?? Ni nani amesababisha aitwe fisadi mpaka wewe sasa hivi useme kumbe?? Ebu niambie hapo nani kashikiwa akili.
Baada ya kufuatilia watu wote wanaomwita Fisadi ndani ya hoja zao wanaonesha kumbe wanamtuhumu tu hakuna mwenye kuelezea hasa ufisadi wake ni nini!!
 
Kila siku tunaambiwa ni kwa nini CHADEMA walikubali kumpokea Lowassa mtu waliyekuwa wanamtuhumu kwa ufisadi wakati akiwa CCM. Hoja hii ya kukera inayoshabikiwa na kundi la watu ya aina ya Mzee Mwanakijiji na Nyani Ngabu siyo tu ni dhaifu bali pia inakera.

Siasa si nasaba ya kiasili (Gene) kwamba ukizaliwa CCM basi ukoo wako milele utakuwa ni CCM ama CHADEMA, bali ni mchezo ambao kanuni yake kubwa ni kufanikisha Agenda inayokubaliwa na chama husika cha siasa. Lowassa alipokuwa CCM alikuwa ni kihimili cha mfumo wa chama hicho, kina Kikwete na wenzake walikuwa anamtumia Lowassa kuunganisha nguvu za wanaopingana ndani ya chama hicho.

Mtu mwenye nguvu kama hiyo ndani ya chama cha siasa unatarajia vipi wapinzani wake wasimshambulie. Halafu CHADEMA walikuwa wanatumia taarifa za Kamati ya Mwakyembe kumshambulia Lowassa na wala si nje ya taarifa hizo. Kusema kwamba kwa kuwa CHADEMA walisema Lowassa ni fisadi basi anakuwa fisadi ni jambo la kustaajabisha kabisa.

Hoja kubwa ya CHADEMA wakati ule na hata sasa ni kuwa kama kina Mwakyembe waliona Lowassa kaitia hasara nchi kwenye Kandarasi ya kufua umeme iliyohusisha Kampuni ya Richmond, kwa nini asifikishwe mahakamani? Kina Mnyika na Lema kwa kutumia mbinu za kisiasa walikuwa wanasema kuwa inakuwaje wezi wa kuku wako magerezani wakati Lowassa yupo mtaani anadunda?

Swali la Msingi kama ufisadi wa Lowassa ulitokana na CHADEMA kusema ni fisadi wao CCM kama chama msimamo wao wakati ule ulikuwaje, walikuwa wanaona kwamba Lowassa ni fisadi ama si fisadi? Ajabu kubwa kuliko yote ni ukiwauliza wana CCM ufisadi wa Lowassa ni upi wanaishia kusema waliosema Lowassa ni fisadi ni CHADEMA!!

Mpaka sasa Lowassa anatuhumiwa tu kwamba ni Fisadi lakini hakuna hoja au ushahidi mahsusi kuonesha kwamba yeye kweli ni Fisadi. Na inawezekana akawa "fisadi" kwa kutumia mbinu na sheria kama za Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kina siye ndiyo tutakuwa Fethulla Gulen wa zama hizo!!

Hoja kwamba CHADEMA ndiyo "walisema" kuwa Lowassa ni fisadi ni za uwezo wa chini sana katika kujenga hoja. Tunataka mtu aje atuambie yeye anaposema kuwa Lowassa ni fisadi basi na atuambie kuwa ufisadi wake ni upi. Tumechoka kuishi kwa uvumi!!
tapatalk_1471253548150.jpeg
tapatalk_1470400069628.jpeg
 
Kusema kweli tukio la CDM kumpokea Lowasa....limewabomoa sana kisiasa kwa wenye akili huru na kufikiria vyema......iwe kweli Lowasa ni fisadi au hata kama sio fisadi......!!!???
 
Ulisema hivyo wakati CHADEMA wanasema yeye ni fisadi?
Na pengine inakera kwa sababu ina ukweli mwingi ndani yake.
Ukweli mara nyingi hukera wale wasiopenda kuusikia.

Kwani wakati CHADEMA wanamtuhumu kuwa fisadi walitoa ithibati gani juu ya hayo madai yao?

Wakati CHADEMA wanasema kwamba Lowasa ni fisadi uliwakosoa na kuwaambia kwamba hoja zao ni za watu wenye uwezo wa chini sana katika kujenga hoja? Au ndo ulipaza sauti kuimba mapambio ya Lowasa ni fisadi?

Nyie wakati mnasema ni fisadi mlituambia ufisadi wake ni upi? Na kama mlituambia, ikawaje tena mwaka jana mkabadili gia angani?
Ni fisadi akiwa CCM lakini akiwa kwenu ni msafi?
Nyie kubalini tu kuwa mlichemsha.
Majibu murua
 
Kila siku tunaambiwa ni kwa nini CHADEMA walikubali kumpokea Lowassa mtu waliyekuwa wanamtuhumu kwa ufisadi wakati akiwa CCM. Hoja hii ya kukera inayoshabikiwa na kundi la watu ya aina ya Mzee Mwanakijiji na Nyani Ngabu siyo tu ni dhaifu bali pia inakera.

Siasa si nasaba ya kiasili (Gene) kwamba ukizaliwa CCM basi ukoo wako milele utakuwa ni CCM ama CHADEMA, bali ni mchezo ambao kanuni yake kubwa ni kufanikisha Agenda inayokubaliwa na chama husika cha siasa. Lowassa alipokuwa CCM alikuwa ni kihimili cha mfumo wa chama hicho, kina Kikwete na wenzake walikuwa anamtumia Lowassa kuunganisha nguvu za wanaopingana ndani ya chama hicho.

Mtu mwenye nguvu kama hiyo ndani ya chama cha siasa unatarajia vipi wapinzani wake wasimshambulie. Halafu CHADEMA walikuwa wanatumia taarifa za Kamati ya Mwakyembe kumshambulia Lowassa na wala si nje ya taarifa hizo. Kusema kwamba kwa kuwa CHADEMA walisema Lowassa ni fisadi basi anakuwa fisadi ni jambo la kustaajabisha kabisa.

Hoja kubwa ya CHADEMA wakati ule na hata sasa ni kuwa kama kina Mwakyembe waliona Lowassa kaitia hasara nchi kwenye Kandarasi ya kufua umeme iliyohusisha Kampuni ya Richmond, kwa nini asifikishwe mahakamani? Kina Mnyika na Lema kwa kutumia mbinu za kisiasa walikuwa wanasema kuwa inakuwaje wezi wa kuku wako magerezani wakati Lowassa yupo mtaani anadunda?

Swali la Msingi kama ufisadi wa Lowassa ulitokana na CHADEMA kusema ni fisadi wao CCM kama chama msimamo wao wakati ule ulikuwaje, walikuwa wanaona kwamba Lowassa ni fisadi ama si fisadi? Ajabu kubwa kuliko yote ni ukiwauliza wana CCM ufisadi wa Lowassa ni upi wanaishia kusema waliosema Lowassa ni fisadi ni CHADEMA!!

Mpaka sasa Lowassa anatuhumiwa tu kwamba ni Fisadi lakini hakuna hoja au ushahidi mahsusi kuonesha kwamba yeye kweli ni Fisadi. Na inawezekana akawa "fisadi" kwa kutumia mbinu na sheria kama za Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kina siye ndiyo tutakuwa Fethulla Gulen wa zama hizo!!

Hoja kwamba CHADEMA ndiyo "walisema" kuwa Lowassa ni fisadi ni za uwezo wa chini sana katika kujenga hoja. Tunataka mtu aje atuambie yeye anaposema kuwa Lowassa ni fisadi basi na atuambie kuwa ufisadi wake ni upi. Tumechoka kuishi kwa uvumi!!

Mkuu, ulishaambiwa Lowasa hasafishiki kaka...
Jambo hapa si kuwa Lowasa ni fisadi au lah...
Swala hapa ni kwamba Chadema ni cham kisichoeleweka kinasimamia nini hasa...
Jana walisema kuwa yeye ni Fisadi, leo unatuambia kuwa hapana jamaa ni msafi.. Je kwa mwenye uelewa mpana( asiyefunikwa na mapenzi ya chama kama wewe) huwa anakosa asimamie kipi, je huyu ni fisadi au sio fisadi?
Alafu pia mtu mwenye uelewa atajiuliza, kama jana chama na viongozi wake walikomaza mishipa, wakasema makubwa kuwa ccm ni mafisadi hasa Fulani na Fulani ( Lowasa akiwa ni Fisadi Papa ). Alafu leo chama hichohicho na viongozi walewale wanasema hapana, yule fisadi papa sasa kasafishika ni Msafi papa,... Wewe ungekiamini tena chama hicho au viongozi hao?
Bado naendelea kusema, chama kikiwa na itikadi ya kuchafuana, na kukejeriana badala ya kujenga hoja kwa ajili ya maendeleo ya Taifa huwa inavuna mazao haya ya haibu.
Leo hii chadema inakosa sehemu ya kusimamia kama zamani... Sasa inadakia mada zisizokuwa na mashiko kwa watu wa chini kabisa, mara ukuta, mara kuziba midomo, mara udicteta n.k.
Zamani chadema ilikuwa ikiaminiwa kwa kukemea ufisadi, na ikijinasibu kuwa Lowasa ni fisadi namba moja katika ccm. Ila leo hamna chama hakina cha kusema tena kama zamani...
Kwahiyo kijana, hapa chadema ndio wanaotakiwa wajibu, je pale zamani walikuwa wanatuongopea kuhusu Lowasa kuwa fisadi? Na kama walituongopea je kwanini tiwaamini sasa hivi? Tuna uwakika gani kuwa kwa sasa hawatungopei? Na je hawa jamaa hawatatubadilia gia angani tena?
Kaa kimya kaka.... Watu inatuuma sana Lowasa kusafishwa kwa sasa na haohao waliotujengea chuki juu yake siku za nyuma...
 
Kila siku tunaambiwa ni kwa nini CHADEMA walikubali kumpokea Lowassa mtu waliyekuwa wanamtuhumu kwa ufisadi wakati akiwa CCM. Hoja hii ya kukera inayoshabikiwa na kundi la watu ya aina ya Mzee Mwanakijiji na Nyani Ngabu siyo tu ni dhaifu bali pia inakera.

Siasa si nasaba ya kiasili (Gene) kwamba ukizaliwa CCM basi ukoo wako milele utakuwa ni CCM ama CHADEMA, bali ni mchezo ambao kanuni yake kubwa ni kufanikisha Agenda inayokubaliwa na chama husika cha siasa. Lowassa alipokuwa CCM alikuwa ni kihimili cha mfumo wa chama hicho, kina Kikwete na wenzake walikuwa anamtumia Lowassa kuunganisha nguvu za wanaopingana ndani ya chama hicho.

Mtu mwenye nguvu kama hiyo ndani ya chama cha siasa unatarajia vipi wapinzani wake wasimshambulie. Halafu CHADEMA walikuwa wanatumia taarifa za Kamati ya Mwakyembe kumshambulia Lowassa na wala si nje ya taarifa hizo. Kusema kwamba kwa kuwa CHADEMA walisema Lowassa ni fisadi basi anakuwa fisadi ni jambo la kustaajabisha kabisa.

Hoja kubwa ya CHADEMA wakati ule na hata sasa ni kuwa kama kina Mwakyembe waliona Lowassa kaitia hasara nchi kwenye Kandarasi ya kufua umeme iliyohusisha Kampuni ya Richmond, kwa nini asifikishwe mahakamani? Kina Mnyika na Lema kwa kutumia mbinu za kisiasa walikuwa wanasema kuwa inakuwaje wezi wa kuku wako magerezani wakati Lowassa yupo mtaani anadunda?

Swali la Msingi kama ufisadi wa Lowassa ulitokana na CHADEMA kusema ni fisadi wao CCM kama chama msimamo wao wakati ule ulikuwaje, walikuwa wanaona kwamba Lowassa ni fisadi ama si fisadi? Ajabu kubwa kuliko yote ni ukiwauliza wana CCM ufisadi wa Lowassa ni upi wanaishia kusema waliosema Lowassa ni fisadi ni CHADEMA!!

Mpaka sasa Lowassa anatuhumiwa tu kwamba ni Fisadi lakini hakuna hoja au ushahidi mahsusi kuonesha kwamba yeye kweli ni Fisadi. Na inawezekana akawa "fisadi" kwa kutumia mbinu na sheria kama za Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kina siye ndiyo tutakuwa Fethulla Gulen wa zama hizo!!

Hoja kwamba CHADEMA ndiyo "walisema" kuwa Lowassa ni fisadi ni za uwezo wa chini sana katika kujenga hoja. Tunataka mtu aje atuambie yeye anaposema kuwa Lowassa ni fisadi basi na atuambie kuwa ufisadi wake ni upi. Tumechoka kuishi kwa uvumi!!
Taarifa ya Mwakyembe ni ya ukweli ama uongo? Na kama ya uongo tupe ushahidi usio na mashaka kuthibitisha uongo huo
 
Mahakama ndiyo yenye wajibu wa kuthibitisha!!
Huwa nawasikia watu waliochafuliwa majina wakitoa muda wa majina yao kusafishwa.....la watawaburuta wanaowachafua mahakamani

Sijui kwa nini Lowassa hawapeleki mahakamani wanaomchafua
 
Nyani Ngabu, huwa naheshimu sana hoja zako nyingi. Ninaomba unitie moyo niendelee kuheshimu kwa kuonyesha ukweli.

CHADEMA, ni chama cha upinzani hakina dola wala hakiongozi serikali. Report ya Mwakyembe imebainisha kwamba Lowasa ni fisadi. Tena kwa taarifa zaidi kwamb kuna mengine yamehifadhiwa kwa usalama wa nchi. Wewe ulitaka CHADEMA waseme kwamba Lowasa ni safi, kabla hajasafishwa mahakama??

Watanzania wakategemea kwamba mafisadi hao waliotajwa Lowasa, na wenzake wengi tu watapelekwa mahakamani ili

wahukumiwe kwa mujibu wa sheria, lakini kimya kikaendelea. Siyo kwa Lowasa bali kwa watuhumiwa wote wa ufisadi hadi leo tunaona keusi na kekundu.

Huo ukweli mwingi unaoujua wewe, kama ndivyo ilivyo, kwa nini hapelekwi mahakamani? Akiwa ccm alikuwa ni ajali za kisiasa, lakini baada ya kuamua kuondoka kwa hiyari yake, sasa kawa fisadi? Nidyo tuseme ni fisadi, kwa nini hapelekwi mahakamani?

Vipi mafisadi wa ESCROW, Lugumi na wengine wengi wanaofugwa ccm na serikali yake. Mnasubiri waondoke ndipo muanze kuimba wimbo wa ufisadi wao? Adhabu ya fisadi ni kutokuondoka Ccm? Hukumu ya fisadi ni kuzomewa? Kwa sheria zipi Nyangi ngabu?

Unaposema walichemsha, nani aliyechemsha? CHDEMA waliosema ni fisadi kwa sababu ya taarifa ya tume ya Mwakyembe?
Kamati ya Mwakyembe iliyosema Lowasa ni fisadi? Ccm kumsafisha kwamba ilikuwa ni ajali ya kisiasa? Srikali kukosa ujasiri wa kumpeleka mahakani au ccm kuanz akuimba wimbo wa ufisadi kipumbavu bila kurejea taarifa ya Mwakyembe na kuaishi kusema CHDEMA walisema?

Naomba uwe serious.

Ok. Lowasa ni fisadi, kwa nini Serikali haimpeleki mahakani? Pengine tuanzie hapa!
Objection ur honor.

Lowassa hakuondoka kwa hiari......aliondoka baada ya kukatwa na ccm.

Hiari ingekuwa kabla ya kinyang'anyiro cha kumpata mgombea wa ccm.

Dr Slaa nae alisisitiza kama kweli Lowassa ana mahaba na cdm aje kabla ya kinyang'anyiro.

Maana ile staili ilikuwa ya makombo.[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Back
Top Bottom