Ni tuhuma tu Lowassa kumbe si Fisadi!!

Ni tuhuma tu Lowassa kumbe si Fisadi!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
25,838
Reaction score
50,541
Kila siku tunaambiwa ni kwa nini CHADEMA walikubali kumpokea Lowassa mtu waliyekuwa wanamtuhumu kwa ufisadi wakati akiwa CCM. Hoja hii ya kukera inayoshabikiwa na kundi la watu ya aina ya Mzee Mwanakijiji na Nyani Ngabu siyo tu ni dhaifu bali pia inakera.

Siasa si nasaba ya kiasili (Gene) kwamba ukizaliwa CCM basi ukoo wako milele utakuwa ni CCM ama CHADEMA, bali ni mchezo ambao kanuni yake kubwa ni kufanikisha Agenda inayokubaliwa na chama husika cha siasa. Lowassa alipokuwa CCM alikuwa ni kihimili cha mfumo wa chama hicho, kina Kikwete na wenzake walikuwa anamtumia Lowassa kuunganisha nguvu za wanaopingana ndani ya chama hicho.

Mtu mwenye nguvu kama hiyo ndani ya chama cha siasa unatarajia vipi wapinzani wake wasimshambulie. Halafu CHADEMA walikuwa wanatumia taarifa za Kamati ya Mwakyembe kumshambulia Lowassa na wala si nje ya taarifa hizo. Kusema kwamba kwa kuwa CHADEMA walisema Lowassa ni fisadi basi anakuwa fisadi ni jambo la kustaajabisha kabisa.

Hoja kubwa ya CHADEMA wakati ule na hata sasa ni kuwa kama kina Mwakyembe waliona Lowassa kaitia hasara nchi kwenye Kandarasi ya kufua umeme iliyohusisha Kampuni ya Richmond, kwa nini asifikishwe mahakamani? Kina Mnyika na Lema kwa kutumia mbinu za kisiasa walikuwa wanasema kuwa inakuwaje wezi wa kuku wako magerezani wakati Lowassa yupo mtaani anadunda?

Swali la Msingi kama ufisadi wa Lowassa ulitokana na CHADEMA kusema ni fisadi wao CCM kama chama msimamo wao wakati ule ulikuwaje, walikuwa wanaona kwamba Lowassa ni fisadi ama si fisadi? Ajabu kubwa kuliko yote ni ukiwauliza wana CCM ufisadi wa Lowassa ni upi wanaishia kusema waliosema Lowassa ni fisadi ni CHADEMA!!

Mpaka sasa Lowassa anatuhumiwa tu kwamba ni Fisadi lakini hakuna hoja au ushahidi mahsusi kuonesha kwamba yeye kweli ni Fisadi. Na inawezekana akawa "fisadi" kwa kutumia mbinu na sheria kama za Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kina siye ndiyo tutakuwa Fethulla Gulen wa zama hizo!!

Hoja kwamba CHADEMA ndiyo "walisema" kuwa Lowassa ni fisadi ni za uwezo wa chini sana katika kujenga hoja. Tunataka mtu aje atuambie yeye anaposema kuwa Lowassa ni fisadi basi na atuambie kuwa ufisadi wake ni upi. Tumechoka kuishi kwa uvumi!!
 
Tangu lini CCM wakawa na uwezo wa kujenga hoja? Zaidi ya fitina, majungu, Umbea, hasa hasa na kubwa zaidi ni WIZI na mbaya zaidi vijana wao sasa ndio wamekua wezi tena majambazi! Wamewezaje kuuza ardhi? Jamani ardhi sio pipi ujue! Yaani walipata wapi guts za kufanya hivi bila kuwaona wazee wao wakiiba?? CCM ni wezi wa kila kitu hadi pumzi
 
Kila siku tunaambiwa ni kwa nini CHADEMA walikubali kumpokea Lowassa mtu waliyekuwa wanamtuhumu kwa ufisadi wakati akiwa CCM. Hoja hii ya kukera inayoshabikiwa na kundi la watu ya aina ya Mzee Mwanakijiji na Nyani Ngabu siyo tu ni dhaifu bali pia inakera.

Ulisema hivyo wakati CHADEMA wanasema yeye ni fisadi?
Na pengine inakera kwa sababu ina ukweli mwingi ndani yake.
Ukweli mara nyingi hukera wale wasiopenda kuusikia.

Mpaka sasa Lowassa anatuhumiwa tu kwamba ni Fisadi lakini hakuna hoja au ushahidi mahsusi kuonesha kwamba yeye kweli ni Fisadi. Na inawezekana akawa "fisadi" kwa kutumia mbinu na sheria kama za Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kina siye ndiyo tutakuwa Fethulla Gulen wa zama hizo!!

Kwani wakati CHADEMA wanamtuhumu kuwa fisadi walitoa ithibati gani juu ya hayo madai yao?

Hoja kwamba CHADEMA ndiyo "walisema" kuwa Lowassa ni fisadi ni za uwezo wa chini sana katika kujenga hoja.
Wakati CHADEMA wanasema kwamba Lowasa ni fisadi uliwakosoa na kuwaambia kwamba hoja zao ni za watu wenye uwezo wa chini sana katika kujenga hoja? Au ndo ulipaza sauti kuimba mapambio ya Lowasa ni fisadi?

Tunataka mtu aje atuambie yeye anaposema kuwa Lowassa ni fisadi basi na atuambie kuwa ufisadi wake ni upi. Tumechoka kuishi kwa uvumi!!

Nyie wakati mnasema ni fisadi mlituambia ufisadi wake ni upi? Na kama mlituambia, ikawaje tena mwaka jana mkabadili gia angani?
Ni fisadi akiwa CCM lakini akiwa kwenu ni msafi?
Nyie kubalini tu kuwa mlichemsha.
 
Mpaka sasa naona hata mahakama ya mafisadi haimuhusu pamoja na kelele zote zile
Inakera wakilala wakiamka wanakuja na hoja kwamba CHADEMA "ilishindwa" mwaka jana kwa kuwa ilimsimamisha Lowassa. Chama kilichoongeza Madiwani, wabunge na kura za Rais kinakuwaje kimeshindwa. Malengo ya CHADEMA kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 wao CCM waliyajua?
 
Inaonekana hujui tifauti Kati ya waziri mkuu na wazri wa wzara flan,, elewa pia mipaka na mahamuzi ya wazri mkuu katika kulinda usalama wa nchi,, ukiyajua hayo,, fatilia vzuri uzaifu wa upinzani walivyo shindwa kutumia kete hyo kimatendo kuliko maneno kujijenga
 
Hiyo mipaka na hizo tofauti za Waziri Mkuu na mawaziri wengine hapa zinasaidia nini katika kutaka kujua ufisadi wa Lowassa ni upi hasa?
 
Ulisema hivyo wakati CHADEMA wanasema yeye ni fisadi?

Na pengine inakera kwa sababu ina ukweli mwingi ndani yake.

Ukweli mara nyingi hukera wale wasiopenda kuusikia.

Kwani wakati CHADEMA wanamtuhumu kuwa fisadi walitoa ithibati gani juu ya hayo madai yao?

Wakati CHADEMA wanasema kwamba Lowasa ni fisadi uliwakosoa na kuwaambia kwamba hoja zao ni za watu wenye uwezo wa chini sana katika kujenga hoja? Au ndo ulipaza sauti kuimba mapambio ya Lowasa ni fisadi?

Nyie wakati mnasema ni fisadi mlituambia ufisadi wake ni upi? Na kama mlituambia, ikawaje tena mwaka jana mkabadili gia angani?

Ni fisadi akiwa CCM lakini akiwa kwenu ni msafi?

Nyie kubalini tu kuwa mlichemsha.
Mbona longolongo nyingi afu husemi kuwa ni FISADI au sio FISADI
 
Uko sahihi Kamanda, waambie na hawa[emoji116] [emoji116] waje wakanushe na kumuomba msamaha Mh. Wazari Mkuu mstaafu. Refer his words: "Nitawashinda wapinzani wangu ndani na nje ya chama (CCM) "-Mh Lowasa

1471547892088.jpg
 
Kila siku tunaambiwa ni kwa nini CHADEMA walikubali kumpokea Lowassa mtu waliyekuwa wanamtuhumu kwa ufisadi wakati akiwa CCM. Hoja hii ya kukera inayoshabikiwa na kundi la watu ya aina ya Mzee Mwanakijiji na Nyani Ngabu siyo tu ni dhaifu bali pia inakera.

Siasa si nasaba ya kiasili (Gene) kwamba ukizaliwa CCM basi ukoo wako milele utakuwa ni CCM ama CHADEMA, bali ni mchezo ambao kanuni yake kubwa ni kufanikisha Agenda inayokubaliwa na chama husika cha siasa. Lowassa alipokuwa CCM alikuwa ni kihimili cha mfumo wa chama hicho, kina Kikwete na wenzake walikuwa anamtumia Lowassa kuunganisha nguvu za wanaopingana ndani ya chama hicho.

Mtu mwenye nguvu kama hiyo ndani ya chama cha siasa unatarajia vipi wapinzani wake wasimshambulie. Halafu CHADEMA walikuwa wanatumia taarifa za Kamati ya Mwakyembe kumshambulia Lowassa na wala si nje ya taarifa hizo. Kusema kwamba kwa kuwa CHADEMA walisema Lowassa ni fisadi basi anakuwa fisadi ni jambo la kustaajabisha kabisa.

Hoja kubwa ya CHADEMA wakati ule na hata sasa ni kuwa kama kina Mwakyembe waliona Lowassa kaitia hasara nchi kwenye Kandarasi ya kufua umeme iliyohusisha Kampuni ya Richmond, kwa nini asifikishwe mahakamani? Kina Mnyika na Lema kwa kutumia mbinu za kisiasa walikuwa wanasema kuwa inakuwaje wezi wa kuku wako magerezani wakati Lowassa yupo mtaani anadunda?

Swali la Msingi kama ufisadi wa Lowassa ulitokana na CHADEMA kusema ni fisadi wao CCM kama chama msimamo wao wakati ule ulikuwaje, walikuwa wanaona kwamba Lowassa ni fisadi ama si fisadi? Ajabu kubwa kuliko yote ni ukiwauliza wana CCM ufisadi wa Lowassa ni upi wanaishia kusema waliosema Lowassa ni fisadi ni CHADEMA!!

Mpaka sasa Lowassa anatuhumiwa tu kwamba ni Fisadi lakini hakuna hoja au ushahidi mahsusi kuonesha kwamba yeye kweli ni Fisadi. Na inawezekana akawa "fisadi" kwa kutumia mbinu na sheria kama za Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kina siye ndiyo tutakuwa Fethulla Gulen wa zama hizo!!

Hoja kwamba CHADEMA ndiyo "walisema" kuwa Lowassa ni fisadi ni za uwezo wa chini sana katika kujenga hoja. Tunataka mtu aje atuambie yeye anaposema kuwa Lowassa ni fisadi basi na atuambie kuwa ufisadi wake ni upi. Tumechoka kuishi kwa uvumi!!
Umezunguka weeeeeee lakini umerudi pale pale. Maswali yote hayo mngeanza kujibu CHADEMA kwanza. Halafu uwa mnalichukulia hili suala kama mzaha lakini litawaharibia sana uchaguzi ujao.
 
Chief!ni Sawa na kumtudikia drip maiti it's to late bro!lowasa is politically dead !mwacheni MZEE akachunge ngombe !mmemtia shombo wenyewe sasa mnahaha nini?
 
patrickcharles nanichokisema na wewe ndiyo unakirudia. Wewe unaamini kwamba Lowassa ni fisadi kwa kuwa tu kina Lema, Msigwa, Mnyika na wenzake walisema kuwa ni Fisadi. Hilo tu ndiyo linalokufanya umwite Lowassa fisadi?
 
Back
Top Bottom