Ni tuhuma tu Lowassa kumbe si Fisadi!!

Ni tuhuma tu Lowassa kumbe si Fisadi!!

patrickcharles nanichokisema na wewe ndiyo unakirudia. Wewe unaamini kwamba Lowassa ni fisadi kwa kuwa tu kina Lema, Msigwa, Mnyika na wenzake walisema kuwa ni Fisadi. Hilo tu ndiyo linalokufanya umwite Lowassa fisadi?
Allen acha ujinga bana. hao viongozi waliokuwa wanatamka hayo unataka kutuambia hawana weledi wowote. watu tunawaamini wameenda shule hawawezi kuja na kutoa blabla kwenye mambo ya kitaifa. hatufanyi utani na mambo yakitaifa. tafadhali kama huna kazi nyingine ya kufanya bora upotezee tu hii mada yako. kama umelipwa fedha uje ulete propaganda zako humu. umedunda. hum.shawishi mtu yoyote. ingekuwa ni vizuri ukaenda ukaulizana na viongozi wakikupa majibu ya kutosha na kama watakukubalia mawazo yako, waje watuambie wajipime wenyewe kama wanaweza kuwa viongozi wa kitaifa. basi wajiuzuru. tena mimi ningekuwa lowasa ningewapeleka wote mahakamani ambao wamekuwa wakinitukana na kunifedhehesha na baadae kunipaka mafuta na kunisafisha. upuuz mtupu
 
Mahakama ndiyo yenye wajibu wa kuthibitisha!!
kama unajua mahakama ndio yenye wajibu kwa nini wewe umejichukulia jukumu la kumsafisha mtu kwa wananchi! kwa mamlaka yapi ya kisheria. suala lingekuwa ni kuendelea kushinikiza sheria ichukue mkondo wake. tatizo watu wamekamba michuzi sasa wanatafuta namna ya ku justify na kuweka mazingira sawa.
 
Kila siku tunaambiwa ni kwa nini CHADEMA walikubali kumpokea Lowassa mtu waliyekuwa wanamtuhumu kwa ufisadi wakati akiwa CCM. Hoja hii ya kukera inayoshabikiwa na kundi la watu ya aina ya Mzee Mwanakijiji na Nyani Ngabu siyo tu ni dhaifu bali pia inakera.

Siasa si nasaba ya kiasili (Gene) kwamba ukizaliwa CCM basi ukoo wako milele utakuwa ni CCM ama CHADEMA, bali ni mchezo ambao kanuni yake kubwa ni kufanikisha Agenda inayokubaliwa na chama husika cha siasa. Lowassa alipokuwa CCM alikuwa ni kihimili cha mfumo wa chama hicho, kina Kikwete na wenzake walikuwa anamtumia Lowassa kuunganisha nguvu za wanaopingana ndani ya chama hicho.

Mtu mwenye nguvu kama hiyo ndani ya chama cha siasa unatarajia vipi wapinzani wake wasimshambulie. Halafu CHADEMA walikuwa wanatumia taarifa za Kamati ya Mwakyembe kumshambulia Lowassa na wala si nje ya taarifa hizo. Kusema kwamba kwa kuwa CHADEMA walisema Lowassa ni fisadi basi anakuwa fisadi ni jambo la kustaajabisha kabisa.

Hoja kubwa ya CHADEMA wakati ule na hata sasa ni kuwa kama kina Mwakyembe waliona Lowassa kaitia hasara nchi kwenye Kandarasi ya kufua umeme iliyohusisha Kampuni ya Richmond, kwa nini asifikishwe mahakamani? Kina Mnyika na Lema kwa kutumia mbinu za kisiasa walikuwa wanasema kuwa inakuwaje wezi wa kuku wako magerezani wakati Lowassa yupo mtaani anadunda?

Swali la Msingi kama ufisadi wa Lowassa ulitokana na CHADEMA kusema ni fisadi wao CCM kama chama msimamo wao wakati ule ulikuwaje, walikuwa wanaona kwamba Lowassa ni fisadi ama si fisadi? Ajabu kubwa kuliko yote ni ukiwauliza wana CCM ufisadi wa Lowassa ni upi wanaishia kusema waliosema Lowassa ni fisadi ni CHADEMA!!

Mpaka sasa Lowassa anatuhumiwa tu kwamba ni Fisadi lakini hakuna hoja au ushahidi mahsusi kuonesha kwamba yeye kweli ni Fisadi. Na inawezekana akawa "fisadi" kwa kutumia mbinu na sheria kama za Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kina siye ndiyo tutakuwa Fethulla Gulen wa zama hizo!!

Hoja kwamba CHADEMA ndiyo "walisema" kuwa Lowassa ni fisadi ni za uwezo wa chini sana katika kujenga hoja. Tunataka mtu aje atuambie yeye anaposema kuwa Lowassa ni fisadi basi na atuambie kuwa ufisadi wake ni upi. Tumechoka kuishi kwa uvumi!!
unejitahidi kumtetea mzee wako. umelipwa kiasi gani kamanda. unasafisha kitu kilichoota kutu. kutu iliyoanzishwa na makamanda viongozi kwa miaka kadhaa. eti leo unasema tusi judge kutokana na maneno yao.khaaa.basi tunaweza sema walikuwa wapumbaf na malofa kipindi hicho. na ujinga huu hatuutaki kwa maslahi ya taifa. na ndio maana wananchi wakawapiga chini. jamani hizi ni zama nyingine. za ukweli na uwazi sio kuja kudanganywa danganywa kama watoto. eti oohh hawakuwa wanamaanisha sijui nini. hivi ukisoma statement ya kila kiongozi wa upinzani kuhusu Lowasa na kutafakari, unawezaje kugeuza maneno kama ulivyofanya hapa.
 
Mzee kashasema, Mwenye ushahidi aende Mahakamani.
ushahidi si walisema kina Mnyika wanao. hata hivyo uliza kamati ya bunge ambayo ilikuwa na wabunge wote. ccm na upinzani walikuwemo.
 
Zilikuwa ni fununu na zitaendelea kuwa fununu ila Mzee ni Msafi kama zilivyo nywele zake nyeupe..kinachotutesa watanzania ni ujinga,wivu hasa wanaume wamerithi kwa wanawake,na kuwa na mtindio wa ubongo ambao umeathiri sana vijana wa CCM na Baadhi ya wazee na wao pia kuwaambukiza wabugia vumbi
 
Babeli nyie CCM kumbe kwa vigezo vyenu hamjawahi kuwaza wala kujua kama Lowassa alikuwa fisadi!?
 
Allen Kilewella,
mimi nilikuwa ni mmoja wa watanzania nilioamini kuwa Lowassa ni fisadi kipindi hicho mambo hayo yakiwa addressed na Chadema, na hiyo imani niliibeba kwasababu Chadema niliiona kama chama makini ambacho hakikurupuki ktk ishu zao.
Ila baada ya Chadema kubadili uelekeo wa upepo basi nikaona kuwa siasa zenu zimegubikwa na UNAFIKI, UROHO WA MADARAKA NA UCHONGANISHI baina ya viongozi wa serikali na wananchi wao.

Ni wazi kuwa sasa Chadema nakiona kama chama kilichojaa hulka za UNAFIKI na kwahili sintoweza kuja kukisapoti kwa namna yoyote ile.

MMELIDANGANYA TAIFA, MMELILAGHAI TAIFA, MMEGUBIKWA NA UNAFIKI,,,,kwahili litawatafuna kwa muda mrefu sana.
 
Lini mahakama ilimhukumu? Mpelekeni mahakani mizoga nyie!
Kuna hoja imeongezwa hapa na MALIGANYA MALIMBE kwamba CHADEMA haikumtaja Lowassa peke yake kwamba ni fisadi, wamo na wengine kama kina Jakaya Kikwete, Andrea Chenge na wengineo wengi tu ambao bado wapo CCM. Swali wanaloulizwa CCM na hawalijibu ni kwa nini wanapomtaja Lowassa kwamba ni fisadi kwa kuwa tu katajwa na CHADEMA mbona na hao wengine waliotajwa na CHADEMA kuwa ni mafisadi CCM haiwashadidii kama wanavyofanya kwa Lowassa?
 
Kila siku tunaambiwa ni kwa nini CHADEMA walikubali kumpokea Lowassa mtu waliyekuwa wanamtuhumu kwa ufisadi wakati akiwa CCM. Hoja hii ya kukera inayoshabikiwa na kundi la watu ya aina ya Mzee Mwanakijiji na Nyani Ngabu siyo tu ni dhaifu bali pia inakera.

Siasa si nasaba ya kiasili (Gene) kwamba ukizaliwa CCM basi ukoo wako milele utakuwa ni CCM ama CHADEMA, bali ni mchezo ambao kanuni yake kubwa ni kufanikisha Agenda inayokubaliwa na chama husika cha siasa. Lowassa alipokuwa CCM alikuwa ni kihimili cha mfumo wa chama hicho, kina Kikwete na wenzake walikuwa anamtumia Lowassa kuunganisha nguvu za wanaopingana ndani ya chama hicho.

Mtu mwenye nguvu kama hiyo ndani ya chama cha siasa unatarajia vipi wapinzani wake wasimshambulie. Halafu CHADEMA walikuwa wanatumia taarifa za Kamati ya Mwakyembe kumshambulia Lowassa na wala si nje ya taarifa hizo. Kusema kwamba kwa kuwa CHADEMA walisema Lowassa ni fisadi basi anakuwa fisadi ni jambo la kustaajabisha kabisa.

Hoja kubwa ya CHADEMA wakati ule na hata sasa ni kuwa kama kina Mwakyembe waliona Lowassa kaitia hasara nchi kwenye Kandarasi ya kufua umeme iliyohusisha Kampuni ya Richmond, kwa nini asifikishwe mahakamani? Kina Mnyika na Lema kwa kutumia mbinu za kisiasa walikuwa wanasema kuwa inakuwaje wezi wa kuku wako magerezani wakati Lowassa yupo mtaani anadunda?

Swali la Msingi kama ufisadi wa Lowassa ulitokana na CHADEMA kusema ni fisadi wao CCM kama chama msimamo wao wakati ule ulikuwaje, walikuwa wanaona kwamba Lowassa ni fisadi ama si fisadi? Ajabu kubwa kuliko yote ni ukiwauliza wana CCM ufisadi wa Lowassa ni upi wanaishia kusema waliosema Lowassa ni fisadi ni CHADEMA!!

Mpaka sasa Lowassa anatuhumiwa tu kwamba ni Fisadi lakini hakuna hoja au ushahidi mahsusi kuonesha kwamba yeye kweli ni Fisadi. Na inawezekana akawa "fisadi" kwa kutumia mbinu na sheria kama za Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kina siye ndiyo tutakuwa Fethulla Gulen wa zama hizo!!

Hoja kwamba CHADEMA ndiyo "walisema" kuwa Lowassa ni fisadi ni za uwezo wa chini sana katika kujenga hoja. Tunataka mtu aje atuambie yeye anaposema kuwa Lowassa ni fisadi basi na atuambie kuwa ufisadi wake ni upi. Tumechoka kuishi kwa uvumi!!
 
Kila siku tunaambiwa ni kwa nini CHADEMA walikubali kumpokea Lowassa mtu waliyekuwa wanamtuhumu kwa ufisadi wakati akiwa CCM. Hoja hii ya kukera inayoshabikiwa na kundi la watu ya aina ya Mzee Mwanakijiji na Nyani Ngabu siyo tu ni dhaifu bali pia inakera.

Siasa si nasaba ya kiasili (Gene) kwamba ukizaliwa CCM basi ukoo wako milele utakuwa ni CCM ama CHADEMA, bali ni mchezo ambao kanuni yake kubwa ni kufanikisha Agenda inayokubaliwa na chama husika cha siasa. Lowassa alipokuwa CCM alikuwa ni kihimili cha mfumo wa chama hicho, kina Kikwete na wenzake walikuwa anamtumia Lowassa kuunganisha nguvu za wanaopingana ndani ya chama hicho.

Mtu mwenye nguvu kama hiyo ndani ya chama cha siasa unatarajia vipi wapinzani wake wasimshambulie. Halafu CHADEMA walikuwa wanatumia taarifa za Kamati ya Mwakyembe kumshambulia Lowassa na wala si nje ya taarifa hizo. Kusema kwamba kwa kuwa CHADEMA walisema Lowassa ni fisadi basi anakuwa fisadi ni jambo la kustaajabisha kabisa.

Hoja kubwa ya CHADEMA wakati ule na hata sasa ni kuwa kama kina Mwakyembe waliona Lowassa kaitia hasara nchi kwenye Kandarasi ya kufua umeme iliyohusisha Kampuni ya Richmond, kwa nini asifikishwe mahakamani? Kina Mnyika na Lema kwa kutumia mbinu za kisiasa walikuwa wanasema kuwa inakuwaje wezi wa kuku wako magerezani wakati Lowassa yupo mtaani anadunda?

Swali la Msingi kama ufisadi wa Lowassa ulitokana na CHADEMA kusema ni fisadi wao CCM kama chama msimamo wao wakati ule ulikuwaje, walikuwa wanaona kwamba Lowassa ni fisadi ama si fisadi? Ajabu kubwa kuliko yote ni ukiwauliza wana CCM ufisadi wa Lowassa ni upi wanaishia kusema waliosema Lowassa ni fisadi ni CHADEMA!!

Mpaka sasa Lowassa anatuhumiwa tu kwamba ni Fisadi lakini hakuna hoja au ushahidi mahsusi kuonesha kwamba yeye kweli ni Fisadi. Na inawezekana akawa "fisadi" kwa kutumia mbinu na sheria kama za Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kina siye ndiyo tutakuwa Fethulla Gulen wa zama hizo!!

Hoja kwamba CHADEMA ndiyo "walisema" kuwa Lowassa ni fisadi ni za uwezo wa chini sana katika kujenga hoja. Tunataka mtu aje atuambie yeye anaposema kuwa Lowassa ni fisadi basi na atuambie kuwa ufisadi wake ni upi. Tumechoka kuishi kwa uvumi!!
Anaandika Mtatiro kabla hajanunuliwa na Lowassa
NINI KINAWEZA KUMWANGUSHA?

Mambo matano yanaweza kumwangusha Lowassa. La kwanza ni makundi. Kama nilivyoeleza, yeye ndiye mtu mwenye kundi kubwa kuliko wagombea wote ndani ya CCM, ikiwa chama hicho kitaamua kumpata mtu wa kati ‘neutral’ ili kukifanya chama kisitetereke, yeye ndiye atakayekuwa wa kwanza kuenguliwa.

Lakini jambo la pili ni kashfa ya Richmond. Tangu kashfa hiyo ilipotokea, Lowassa hakuwahi kuiongelea tena na hajawahi kuwaeleza Watanzania alihusikaje na kama yeye hakuhusika ni kina nani waliohusika kwa majina. Ukweli ni jambo muhimu kwa mtu anayehitaji kuongoza nchi. Ukituhumiwa kwa kashfa kubwa kama ya Lowassa halafu unasema tu hukuhusika bila kueleza nani walihusika huku wewe ndiye ulikuwa Waziri Mkuu, inajenga taswira kuwa kuna jambo kubwa unalificha na husemi ukweli kwa jamii yako. Hili linaweza kumhukumu. CCM inaweza kumuondoa Lowassa ili kuondokana na mgombea mwenye madoa hata kama haina uthibitisho na madoa hayo kwa asilimia 100.

Jambo la tatu linaloweza kumchuja Lowassa ni afya yake. Pamoja na kuwa afya ni jambo binafsi na siri ya mtu lakini kwa kiongozi, kila jambo lake ni mali ya umma. Rais Kikwete alipougua tezi dume aliutangazia umma na hakuficha. Kwa kipindi kirefu Lowassa amekuwa akionekana kama mgonjwa na si siri kuwa amekuwa akipata matibabu katika hospitali za kimataifa nje ya nchi.

Anapaswa awaeleze Watanzania nini kinamsibu, la asipofanya hivyo wapinzani wake kisiasa wanaweza kuendelea kulitumia jambo hili ipasavyo na chama chake kikaona lina mantiki na kikalitumia kumsulubu kama “unfit person to lead the nation”. Kila chama kinahitaji mgombea urais wake awe na afya bora, isiyofichwa na inayoeleweka. Anapaswa kujitokeza na kufafanua hili haraka na hasa ikizingatiwa muda umekwenda sana.

Michango ya kujitolea kila kukicha katika taasisi mbalimbali, harambee, nyumba za ibada na maeneo mengine ni jambo jingine linaloweza kumhukumu. Lowassa amejitolea mno katika eneo hili. Chama chake kinaweza kujiuliza kwa nini mtu anayejiandaa kugombea urais ajitolee kwa kiwango hiki kusaidia kuchangisha fedha na hata yeye mwenyewe kuchangia kila panapotokea matukio makubwa?

Je, nia yake ni sahihi? Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa “Ikulu hakuna biashara” na CCM inaweza kujitathmini ikiwa mgombea wa namna hii akiingia Ikulu hataanza kutafuta mbinu ya kujirudishia fedha alizokuwa akichangia. Eneo hili si salama kwa Lowassa.

Jambo la tano ni madai kuwa kuna maelewano hafifu na Rais Kikwete. Jambo hilo hakuna aliyethibitisha, lakini huwezi kulidharau moja kwa moja. Katika siasa, ukishindana na walioshikilia “mpini” unaweza kuanguka mahali usipotarajia. Pamoja na kuwa “hawakukutana barabarani”, ukweli ni kuwa Lowassa na Kikwete wa sasa si wale ‘ma-comrade’ wa 2008 kurudi nyuma. Hawa wa sasa ni watu tofauti na duru za ndani ya Serikali zinaonyesha kuwa haziivi.

Kama hivyo ndivyo basi, karata za Lowassa zinaweza kuingia shakani kwa sababu ya kutoimarisha uhusiano wake na Rais anayeondoka madarakani, maana kwa siasa za kurithishana kwa kujuana katika vyama tawala barani Afrika, lazima tukubali ukweli kuwa, Rais aliyeko madarakani ana mchango na ushawishi mkubwa katika kutengeza rais ajaye.

ASIPOCHAGULIWA (MPANGO B)

Namuona Lowassa akiwa na mipango mitatu ikiwa hatapitishwa kugombea urais:

Mpango wa kwanza ni kuendelea kuihamasisha jamii kimaendeleo katika taasisi za kidini, za kiraia, makundi ya vijana, wazee na wanawake kwa mtindo huuhuu ambao amekuwa akiufanya kati ya 2008 –2015 na hata kutoa michango yake na marafiki zake kwa jamii.

Mpango wa pili ni kuishauri Serikali katika maeneo mbalimbali ya kisera na kiusimamizi. Kwa sababu alipokuwa Waziri Mkuu alionyesha usimamizi mzuri na ufuatiliaji imara katika ofisi za umma, anaweza kuifanya kazi hiyo kiushauri.

Mwisho ni kurudi kwenye biashara. Lowassa ni mfanyabiashara katika sehemu kubwa ya maisha yake. Ikiwa hatagombea urais kwa tiketi ya CCM itakuwa muda muafaka kwake kurejea na kusimamia biashara zake na kuachana na siasa za majitaka kama alivyowahi kutamka mmoja wa marafiki zake.

HITIMISHO

Nguvu ya Lowassa ndani ya CCM haimithiliki na hofu ya chama hicho kuwa kumuacha nje ya ulingo kutakitetemesha haikwepeki. Lakini ukweli ni kuwa ndani ya CCM “kuna minofu mingi” ambayo inawazuia vigogo wakubwa wasiondoke na kuhamia vyama vingine hata kama hawakupitishwa kugombea urais. “There is too much stake to eat in CCM than going out”.

Ndiyo maana bado CCM ina nafasi ya kujichagulia mgombea inayemtaka na vigogo wanaotajwa kuitikisa kama Lowassa wakiogopa kuondoka kwa sababu wamekaa serikalini muda mrefu na sasa hawawezi kumalizia maisha bila mfumo huo waliouzoea.

Kwa hiyo, nadhani Lowassa ataendelea kuwa mwanachama mtiifu kwa CCM akiwa Rais au akiwa raia wa kawaida. Kama kuna vyama vya upinzani vilikuwa “vinamtumbulia” macho kama fisi asubirivyo mkono wa binadamu udondoke, ni vyema vikajipanga kupata wagombea wake imara na vijijenge. Pamoja na yote haya namtakia kila la heri Mzee Edward Lowassa katika safari yake ya kisiasa.

KUHUSU MCHAMBUZI:

Julius Mtatiro ni Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa na Kijamii, ana uzoefu mkubwa wa uongozi wa kisiasa hapa Tanzania. Ana Cheti cha Juu cha Sarufi na Lugha, Shahada ya Sanaa “B.A” katika Elimu (Lugha, Siasa na Utawala), Shahada ya Uzamili ya Utawala na Uongozi (M.A) na ni mwanafunzi wa fani ya sheria (L LB) – Anapatikana kupitia +255787536759,(juliusmtatiro@yahoo.com) Uchambuzi na huu unatokana na utafiti na maoni binafsi ya mwandishi). (Uchambuzi huu umechapishwa na Gazeti la Mwananchi la Jumatatu, 11 Mei 2015).
 
Nyani Ngabu, huwa naheshimu sana hoja zako nyingi. Ninaomba unitie moyo niendelee kuheshimu kwa kuonyesha ukweli.

CHADEMA, ni chama cha upinzani hakina dola wala hakiongozi serikali. Report ya Mwakyembe imebainisha kwamba Lowasa ni fisadi. Tena kwa taarifa zaidi kwamb kuna mengine yamehifadhiwa kwa usalama wa nchi. Wewe ulitaka CHADEMA waseme kwamba Lowasa ni safi, kabla hajasafishwa mahakama??

Watanzania wakategemea kwamba mafisadi hao waliotajwa Lowasa, na wenzake wengi tu watapelekwa mahakamani ili

wahukumiwe kwa mujibu wa sheria, lakini kimya kikaendelea. Siyo kwa Lowasa bali kwa watuhumiwa wote wa ufisadi hadi leo tunaona keusi na kekundu.

Huo ukweli mwingi unaoujua wewe, kama ndivyo ilivyo, kwa nini hapelekwi mahakamani? Akiwa ccm alikuwa ni ajali za kisiasa, lakini baada ya kuamua kuondoka kwa hiyari yake, sasa kawa fisadi? Nidyo tuseme ni fisadi, kwa nini hapelekwi mahakamani?

Vipi mafisadi wa ESCROW, Lugumi na wengine wengi wanaofugwa ccm na serikali yake. Mnasubiri waondoke ndipo muanze kuimba wimbo wa ufisadi wao? Adhabu ya fisadi ni kutokuondoka Ccm? Hukumu ya fisadi ni kuzomewa? Kwa sheria zipi Nyangi ngabu?

Unaposema walichemsha, nani aliyechemsha? CHDEMA waliosema ni fisadi kwa sababu ya taarifa ya tume ya Mwakyembe?
Kamati ya Mwakyembe iliyosema Lowasa ni fisadi? Ccm kumsafisha kwamba ilikuwa ni ajali ya kisiasa? Srikali kukosa ujasiri wa kumpeleka mahakani au ccm kuanz akuimba wimbo wa ufisadi kipumbavu bila kurejea taarifa ya Mwakyembe na kuaishi kusema CHDEMA walisema?

Naomba uwe serious.

Ok. Lowasa ni fisadi, kwa nini Serikali haimpeleki mahakani? Pengine tuanzie hapa!
Lowasa kaanza kutuhumiwa na Chadema kabla hata ya Richmond, hivyo msitake kutuaminisha kashfa ya Lowasa ni Richmond tu. Kama mmesahau muulizeni hata Kubenea atawasaidia.
 
API Gravity sisi wengine tumezisahau hizo kashifa zingine itakuwa ni vizuri kama utatukumbusha. Wakudadavuwa huyu Mtatiro hajanunuliwa hata ukisoma bandiko lake anasema kosa la Lowassa ni kutofafanua nini hasa kilitokea kwenye kashifa ya Richmond. Lakini hakuna mahali Mtatiro alisema kuwa Lowassa anahusika na Kashifa ya Richmond. Usimlishe Mtatiro maneno mdomoni.

Kuhusu kutokusema kwa Lowassa tumesema kwa sasa yuko chini ya Kiapo cha Baraza la Mawaziri na kisheria akisema chochote kilichotokea chini ya kiapo hicho anaweza kushitakiwa kwa uhaini. Njia rahisi ashitakiwe ili aseme, kiapo chake kibatilishwe na mahakama na aseme kila anachokijua kuhusu Richmond. Ni lazima Lowassa ashitakiwe ili tumalizane na mzimu wa Richmond.
 
Kila siku tunaambiwa ni kwa nini CHADEMA walikubali kumpokea Lowassa mtu waliyekuwa wanamtuhumu kwa ufisadi wakati akiwa CCM. Hoja hii ya kukera inayoshabikiwa na kundi la watu ya aina ya Mzee Mwanakijiji na Nyani Ngabu siyo tu ni dhaifu bali pia inakera.

Siasa si nasaba ya kiasili (Gene) kwamba ukizaliwa CCM basi ukoo wako milele utakuwa ni CCM ama CHADEMA, bali ni mchezo ambao kanuni yake kubwa ni kufanikisha Agenda inayokubaliwa na chama husika cha siasa. Lowassa alipokuwa CCM alikuwa ni kihimili cha mfumo wa chama hicho, kina Kikwete na wenzake walikuwa anamtumia Lowassa kuunganisha nguvu za wanaopingana ndani ya chama hicho.

Mtu mwenye nguvu kama hiyo ndani ya chama cha siasa unatarajia vipi wapinzani wake wasimshambulie. Halafu CHADEMA walikuwa wanatumia taarifa za Kamati ya Mwakyembe kumshambulia Lowassa na wala si nje ya taarifa hizo. Kusema kwamba kwa kuwa CHADEMA walisema Lowassa ni fisadi basi anakuwa fisadi ni jambo la kustaajabisha kabisa.

Hoja kubwa ya CHADEMA wakati ule na hata sasa ni kuwa kama kina Mwakyembe waliona Lowassa kaitia hasara nchi kwenye Kandarasi ya kufua umeme iliyohusisha Kampuni ya Richmond, kwa nini asifikishwe mahakamani? Kina Mnyika na Lema kwa kutumia mbinu za kisiasa walikuwa wanasema kuwa inakuwaje wezi wa kuku wako magerezani wakati Lowassa yupo mtaani anadunda?

Swali la Msingi kama ufisadi wa Lowassa ulitokana na CHADEMA kusema ni fisadi wao CCM kama chama msimamo wao wakati ule ulikuwaje, walikuwa wanaona kwamba Lowassa ni fisadi ama si fisadi? Ajabu kubwa kuliko yote ni ukiwauliza wana CCM ufisadi wa Lowassa ni upi wanaishia kusema waliosema Lowassa ni fisadi ni CHADEMA!!

Mpaka sasa Lowassa anatuhumiwa tu kwamba ni Fisadi lakini hakuna hoja au ushahidi mahsusi kuonesha kwamba yeye kweli ni Fisadi. Na inawezekana akawa "fisadi" kwa kutumia mbinu na sheria kama za Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kina siye ndiyo tutakuwa Fethulla Gulen wa zama hizo!!

Hoja kwamba CHADEMA ndiyo "walisema" kuwa Lowassa ni fisadi ni za uwezo wa chini sana katika kujenga hoja. Tunataka mtu aje atuambie yeye anaposema kuwa Lowassa ni fisadi basi na atuambie kuwa ufisadi wake ni upi. Tumechoka kuishi kwa uvumi!!
Wewe ama una mtindio wa ubongo au msahaulifu sana. Mwaka 2007 pale Mwembe Yanga nani alitoa Orodha ya Mafisadi? Lowassa hakuwemo?? Ina maana CDM ni chama cha waongo?? Inakuwaje MTU mliyemtangaza kwa miaka 8 kuwa fisadi Leo hii mnadai so fisadi kwa hoja tu kwamba hakupekekwa Mahakamani?? Au sio Fisadi kwa kuwa katoka CCM??Umepoteza muda ujaza kurasa kwa hoja za kijinga zilizojaa mahaba na mihemuko yenge makengeza na ulitima wa busara!! Aibu sana!!
 
API Gravity sisi wengine tumezisahau hizo kashifa zingine itakuwa ni vizuri kama utatukumbusha. Wakudadavuwa huyu Mtatiro hajanunuliwa hata ukisoma bandiko lake anasema kosa la Lowassa ni kutofafanua nini hasa kilitokea kwenye kashifa ya Richmond. Lakini hakuna mahali Mtatiro alisema kuwa Lowassa anahusika na Kashifa ya Richmond. Usimlishe Mtatiro maneno mdomoni.

Kuhusu kutokusema kwa Lowassa tumesema kwa sasa yuko chini ya Kiapo cha Baraza la Mawaziri na kisheria akisema chochote kilichotokea chini ya kiapo hicho anaweza kushitakiwa kwa uhaini. Njia rahisi ashitakiwe ili aseme, kiapo chake kibatilishwe na mahakama na aseme kila anachokijua kuhusu Richmond. Ni lazima Lowassa ashitakiwe ili tumalizane na mzimu wa Richmond.
Ndugu Yangu, ili kutetea uamuzi wa Chadema kumsimamisha Lowasa kuwa mgombea uraisi mwaka jana inabidi ujitoe ufahamu, huu ndiyo ukweli japo hamtaki kuukubali.
 
Time will tell, cha kushangaza ni pale hadi rais anaposema kuwa mafisadi wakati yeye ni amiri jeshi na ana mahakama ya mafisadi!!!!
 
Babeli nyie CCM kumbe kwa vigezo vyenu hamjawahi kuwaza wala kujua kama Lowassa alikuwa fisadi!?
Allen ntake radhi. mi sipo huko. labda wewe. ila ni bora tum support Magufuli kwa utendaji wake. chadema asilia wote tupo huko. tumewaacha chadema maslahi muendelee nayo
 
Lowassa ni fisadi itabaki hivyo hata kwenye Vitabu vya kumbukumbu !!;
Sema alishiriki nao ufisadi mkapa,kikwete na genge lao wapo ccm na wanaogopa kutikisa huyu jamaa kwani atakuja na mambo mazito kuusu hao watu!!!
 
Back
Top Bottom