Ni tuhuma tu Lowassa kumbe si Fisadi!!

Ni tuhuma tu Lowassa kumbe si Fisadi!!

Inakera wakilala wakiamka wanakuja na hoja kwamba CHADEMA "ilishindwa" mwaka jana kwa kuwa ilimsimamisha Lowassa. Chama kilichoongeza Madiwani, wabunge na kura za Rais kinakuwaje kimeshindwa. Malengo ya CHADEMA kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 wao CCM waliyajua?
Sasa kama malengo sio kushika Dola, si viongozi walitakiwa waseme malengo yao kuongeza viti vya ubunge na madiwani yameanikiwa kwa % ngap..? Na kuwaambia kuwa lengo letu lilikuwa hili.
 
Kusema kweli tukio la CDM kumpokea Lowasa....limewabomoa sana kisiasa kwa wenye akili huru na kufikiria vyema......iwe kweli Lowasa ni fisadi au hata kama sio fisadi......!!!???
Ni kweli mkuu CDM wamebomoka kisiasa baada ya kumpokea lowasa LAKINI CCM inaendelea kuporomoka kwa kasi ya ajabu baada ya kushindwa kuwawajibisha na kuwafikisha mahakamani mafisadi 10 ambao walitajwa na cdm na bado wapo ccm mpaka leo hii....fanya utafiti na utatambua hilo mkuu
 
Allen acha ujinga bana. hao viongozi waliokuwa wanatamka hayo unataka kutuambia hawana weledi wowote. watu tunawaamini wameenda shule hawawezi kuja na kutoa blabla kwenye mambo ya kitaifa. hatufanyi utani na mambo yakitaifa. tafadhali kama huna kazi nyingine ya kufanya bora upotezee tu hii mada yako. kama umelipwa fedha uje ulete propaganda zako humu. umedunda. hum.shawishi mtu yoyote. ingekuwa ni vizuri ukaenda ukaulizana na viongozi wakikupa majibu ya kutosha na kama watakukubalia mawazo yako, waje watuambie wajipime wenyewe kama wanaweza kuwa viongozi wa kitaifa. basi wajiuzuru. tena mimi ningekuwa lowasa ningewapeleka wote mahakamani ambao wamekuwa wakinitukana na kunifedhehesha na baadae kunipaka mafuta na kunisafisha. upuuz mtupu
Mkuu kama unatambua kuwa viongozi wa kitaifa wa cdm hawakuwa na utani wakati wanawataja mafisadi akiwemo lowasa,Ni sahihi kabisa.Je,Unatambua na kuamini kuwa wale watu 10 waliobaki ccm mpaka leo nao ni mafisadi kama lowasa?.Je,lowasa ni fisadi kwa kuwa alitajwa na cdm au ni fisadi tangu akiwa ccm?.Je,wale watu 10 waliotajwa na cdm na bado wamo ndani ya ccm,Ni mafisadi au siyo mafisadi?.........babeli naomba jibu ili tuendelee.
 
Wewe ama una mtindio wa ubongo au msahaulifu sana. Mwaka 2007 pale Mwembe Yanga nani alitoa Orodha ya Mafisadi? Lowassa hakuwemo?? Ina maana CDM ni chama cha waongo?? Inakuwaje MTU mliyemtangaza kwa miaka 8 kuwa fisadi Leo hii mnadai so fisadi kwa hoja tu kwamba hakupekekwa Mahakamani?? Au sio Fisadi kwa kuwa katoka CCM??Umepoteza muda ujaza kurasa kwa hoja za kijinga zilizojaa mahaba na mihemuko yenge makengeza na ulitima wa busara!! Aibu sana!!
Mkuu,Unaweza kuniambia ni kwa nini fisadi lowasa hajafikishwa mahakamani mpaka leo licha ya kutajwa na cdm Mwaka 2007 mwembe yanga?.Je,wale wengine 10 waliotajwa pamoja na lowasa watachukuliwa hatua za kisheria lini au walisingiziwa ufisadi na cdm?.....naomba majibu mkuu.
 
Ndugu Yangu, ili kutetea uamuzi wa Chadema kumsimamisha Lowasa kuwa mgombea uraisi mwaka jana inabidi ujitoe ufahamu, huu ndiyo ukweli japo hamtaki kuukubali.
Ongeza na hii"''Ni sawa na kuiamini ripoti ya mwakyembe ya richmond huku mwakyembe huyohuyo akiwasingizia polisi kuwa wanamfualia ili wamuue"''
 
Kila siku tunaambiwa ni kwa nini CHADEMA walikubali kumpokea Lowassa mtu waliyekuwa wanamtuhumu kwa ufisadi wakati akiwa CCM. Hoja hii ya kukera inayoshabikiwa na kundi la watu ya aina ya Mzee Mwanakijiji na Nyani Ngabu siyo tu ni dhaifu bali pia inakera.

Siasa si nasaba ya kiasili (Gene) kwamba ukizaliwa CCM basi ukoo wako milele utakuwa ni CCM ama CHADEMA, bali ni mchezo ambao kanuni yake kubwa ni kufanikisha Agenda inayokubaliwa na chama husika cha siasa. Lowassa alipokuwa CCM alikuwa ni kihimili cha mfumo wa chama hicho, kina Kikwete na wenzake walikuwa anamtumia Lowassa kuunganisha nguvu za wanaopingana ndani ya chama hicho.

Mtu mwenye nguvu kama hiyo ndani ya chama cha siasa unatarajia vipi wapinzani wake wasimshambulie. Halafu CHADEMA walikuwa wanatumia taarifa za Kamati ya Mwakyembe kumshambulia Lowassa na wala si nje ya taarifa hizo. Kusema kwamba kwa kuwa CHADEMA walisema Lowassa ni fisadi basi anakuwa fisadi ni jambo la kustaajabisha kabisa.

Hoja kubwa ya CHADEMA wakati ule na hata sasa ni kuwa kama kina Mwakyembe waliona Lowassa kaitia hasara nchi kwenye Kandarasi ya kufua umeme iliyohusisha Kampuni ya Richmond, kwa nini asifikishwe mahakamani? Kina Mnyika na Lema kwa kutumia mbinu za kisiasa walikuwa wanasema kuwa inakuwaje wezi wa kuku wako magerezani wakati Lowassa yupo mtaani anadunda?

Swali la Msingi kama ufisadi wa Lowassa ulitokana na CHADEMA kusema ni fisadi wao CCM kama chama msimamo wao wakati ule ulikuwaje, walikuwa wanaona kwamba Lowassa ni fisadi ama si fisadi? Ajabu kubwa kuliko yote ni ukiwauliza wana CCM ufisadi wa Lowassa ni upi wanaishia kusema waliosema Lowassa ni fisadi ni CHADEMA!!

Mpaka sasa Lowassa anatuhumiwa tu kwamba ni Fisadi lakini hakuna hoja au ushahidi mahsusi kuonesha kwamba yeye kweli ni Fisadi. Na inawezekana akawa "fisadi" kwa kutumia mbinu na sheria kama za Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kina siye ndiyo tutakuwa Fethulla Gulen wa zama hizo!!

Hoja kwamba CHADEMA ndiyo "walisema" kuwa Lowassa ni fisadi ni za uwezo wa chini sana katika kujenga hoja. Tunataka mtu aje atuambie yeye anaposema kuwa Lowassa ni fisadi basi na atuambie kuwa ufisadi wake ni upi. Tumechoka kuishi kwa uvumi!!
Ufisadi wa Lowassa haukuanzia Richmond, huu ni mdoogo kabisa na umefanyika mwishoni mwishoni wa maisha yake kisiasa. Aliyemtuhumu Lowassa kwanza kabisa alikuwa ni Nyerere, wakati huo Richmond wala haijasikika. Alianzia akiwa DG wa AICC, ghafula bin vuu, kijana mdogo, hana elimu yoyote wala taaluma inayozaa ukwasi (linganisha na topnotch Lawyer kama Chenge, wa Harvard. Lowassa kasoma nini? Wapi?) akajikuta anamiliki viwanja na majengo Arusha maeneo prime. Ikaongezeka maradufu alipokuwa Waziri wa Ardhi kajimilikisha prime areas nchi nzima.

Nchi ikapata njaa akapewa kazi ya kuagiza mchele toka Vietnam, walipokutana na VIP Engineering ya James Rugemarila miaka 20 kabla ya escrow. Yakaja mashangingi ya Wabunge, yumo. Haya yanafahamika kwa CCM na Watanzania na wikileaks. Majumba yake yanafahamika yanakaliwa na Balozi mbalimbali Oysterbay na Balozi za Tanzania huko nje. Hapo hujataja Richmond, wala Dr Slaa alichosema ni hela ya halmashauri na hela za AICC alizosena Lema wakimnadi Nassari. Slaa hadi akasema huyu si mwanaume kwa mila za Kimeru (???). Hakukanusha. Mchungaji Msigwa akafunga kazi kwa kusema yeyite anayemshabikia Lowassa apelekwe Mirembe kupimwa.

Ukitaka kumnasua Lowassa tuhuma za ufisadi kazi yako ni pevu. Richmond ni jambo dooogo sana na mwenyewe anajua.
 
Mpelekeni MAHAKAMANI mbona serikali yenu mnashindwa nini kumkamata?
 
Mkuu kama unatambua kuwa viongozi wa kitaifa wa cdm hawakuwa na utani wakati wanawataja mafisadi akiwemo lowasa,Ni sahihi kabisa.Je,Unatambua na kuamini kuwa wale watu 10 waliobaki ccm mpaka leo nao ni mafisadi kama lowasa?.Je,lowasa ni fisadi kwa kuwa alitajwa na cdm au ni fisadi tangu akiwa ccm?.Je,wale watu 10 waliotajwa na cdm na bado wamo ndani ya ccm,Ni mafisadi au siyo mafisadi?.........babeli naomba jibu ili tuendelee.
kamanda tunachoangalia kama umetamkwa fisadi ni fisadi tu. kwa sababu aliyetamka ana ushahidi wote. haijalishi yupo ccm au upinzani. la msingi tunasema katika nafasi ya urais ni mwiko kupeleka mtuhumiwa au fisadi. hizi nafasi za pembezoni ambazo hazina direct impact na utendaji wa serikali hazina nguvu. wataendelea kutolewa si suala la muda. unafikiriane mtu fisadi alafu unampa nafasi ya urais. na hasa kwa jinsi nafasi hiyo inavyompa madaraka makubwa rais. ni hatari. mtauzwa. na ukizingatia kuwa fisadi ni lazima ana kundi la washirika wenzake nao pia wana washirika wengine. hivi unaona sawa tukizungukwa na network ya wapigaji kutoka juu mpaka chini
 
Ongeza na hii"''Ni sawa na kuiamini ripoti ya mwakyembe ya richmond huku mwakyembe huyohuyo akiwasingizia polisi kuwa wanamfualia ili wamuue"''
kamanda acha ujinga. unajua wajumbe waliokuwemo kwenye kamati ile. kuna wa ccm na upinzani wamo. ni kamati iliyoaminiwa na bunge ikatumwa kazi ikaifanya kwa weledi. be careful na matamshi, fikiri kabla ya kusema. ukitaka kupata taarifa kamili chukua mjumbe mmoja baada ya mwingine halafu wadadavue. wangekuwa ccm peke yao ningekuelewa. lakini na upinzani wamo! !
 
Ni kweli mkuu CDM wamebomoka kisiasa baada ya kumpokea lowasa LAKINI CCM inaendelea kuporomoka kwa kasi ya ajabu baada ya kushindwa kuwawajibisha na kuwafikisha mahakamani mafisadi 10 ambao walitajwa na cdm na bado wapo ccm mpaka leo hii....fanya utafiti na utatambua hilo mkuu
wewe ni mmoja wa wale waliofaidika na ujio wa lowasa chadema. unachojaribu kutetea hata kichaa hawezi kukuelewa. mafisadi wanasafishwa na vyombo vya dola lakini sio watu tu wanajihukulia jukumu la kuwasafisha watu kwa intetest zao na sio za nchi. ni hatari kwa chama kama hiki kupewa uongozi wa nchi.hizi ni zama mpya jamani. lakini najua mpaka leo hamjaelewa lengo la lowasa kuja chadema. in short ni kuua upinzani.... angalia ajenda zote zenye nguvu zimezikwa. na hizo ndio zenye nguvu popote duniani. fanya research. usiwe mvivu kufikiri. chama sasa hakina mwelekeo, wameshaona hawana ajenda sasa ndio wanazuka na vitu vya ajabu ajabu, eti shikilia UKUTA. ujinga mtupu. huwezi kupambana na Magufuli kwa staili hiyo. mngekuwa na akili mngefuata ushauri wa Dr Kitila Mkumbo. alisema siasa za uanaharakati kwa uongozi wa Magufuli hazina mashiko. kwa sababu ni mtendaji wa ukweli na anatumikia wananchi kama wanavyotaka. sssa unataka nini zaidi ya hapo. siasa uchwara hizi za UKUTA hazitatufikisha popote. sana sana tutakuja jilaumu tena baada ya miaka 100 kuwa tumefikaje wakati tukiwa bado maskini. ni kwa sababu tunapotezeana muda kwa mambo ambayo si ya msingi kwa ujenzi wa uchumi wetu kitaifa na mtu mmoja mmoja. wajameni tuwe waangalifu
 
Kigezo gani unatumia kujiita CHADEMA asilia, maana inaonekana kama vile kuna haki fulani umejipa ya kuwa na uasili wa chama kitu ambacho kwa sisi wengine tunaona unawaya waya tu!!
Allen acha hizo. hivi wewe umeingia chadema lini. labda juzijuzi. hujui kazi kubwa tuliojitoa katika kutengeneza mifumo ikiyonyooka toka enzi hizo kabla hatujavamiwa na majamba wazi. tumejitoa kwa hali na mali lakini mwishowake tumeambulia kuvamiwa na mafisadi na kuua kabisa mfumo uliokuwepo. basi kwa sababu wewe ni mmoja wa wale waliofaifika na ujio wao basi. piga kazi kijana. you cant fight them so you have decided to join them. sio kosa lako
 
Kuna hoja imeongezwa hapa na MALIGANYA MALIMBE kwamba CHADEMA haikumtaja Lowassa peke yake kwamba ni fisadi, wamo na wengine kama kina Jakaya Kikwete, Andrea Chenge na wengineo wengi tu ambao bado wapo CCM. Swali wanaloulizwa CCM na hawalijibu ni kwa nini wanapomtaja Lowassa kwamba ni fisadi kwa kuwa tu katajwa na CHADEMA mbona na hao wengine waliotajwa na CHADEMA kuwa ni mafisadi CCM haiwashadidii kama wanavyofanya kwa Lowassa?
suala hili limekuwa sana upande huu kwa sababu ya ile taasisi ya urais.fullstop. achana na watu wa pembezoni ambao hawana nguvu ya madaraka. kama tuliuvaa mkenge huko nyuma haimaanishi tuendelee nao. si lazima tunakaa tunajitafakari na tunasema jamani safari hii hatutaki kurudia makosa. na hivyo ndivyo wananchi waliamua. sasa unataka bado tuwapeleke mafisadi wakawe marais wetu? ??unataka tuendelee kuibiwa mpaka lini
 
Wewe uliingia lini CHADEMA? Mimi kadi yangu ni Namba 387, wewe ya kwako namba ngapi ili tujue nani aliingia juzi juzi CHADEMA.
hahhaha Allen unaona. kumbe nilikuwa sahihi. mimi kadi yangu ni ndani ya wale watu 100 wa mwanzo . ni mkongwe na niliyeona mengi sanaa. mengine tunayavumilia hatuyasemi! lakini ndio changamoto zilizokuwepo za kujenga upinzani wakati huo. lakini huu wa sasa si upinzani ni upingaji tu usiokuwa na mwelekeo. mmeuza chama hivihivi kwa wale jamaa. sijui mmebaki na nini.
 
Lowassa alitajwa kuwa fisadi kwa mara ya kwanza na CHADEMA pale Mwembeyanga kwenye list of shame mwaka 2007 kabla hata report ya Mwakyembe iliyosomwa 2008.

Sasa CHADEMA walitumia report ya Mwakyembe yupi hiyo 2007? Au Mwakyembe ana report ngapi juu ya Edo?

In fact nyie jamaa wapumbavu tu na mnadhani kila mtu ni mbumbumbu kama nyie.
 
Tumebaki na vitega uchumi vilivyotokana na fedha tulizopata kwa kuuza chama. Umefurahi?
hahaha hapo Allen sasa tunaenda sawa. sio suala la kufurahi ni hali ya kuwa na uzalendo tu kwa nchi baada ya kuweka ushabiki pembeni. panapobidi kutetea tutetee lakini penye fyongo tuseme ukweli bila aibu. ukweli utatuweka huru.lakini pia nikusahihishe hapo. embu uliza hivyo vitega uchumi vipo wapi. mikononi mwa chama au mwa watu binafsi. si afadhali tungekuwa na kitega uchumi walau kimoja. ofisi kuu ya chama tu tumeshindwa kujenga unategemea nini. haya wakati wa uchaguzi kila mgombea anaambiwa ajitegemee kifedha. pesa za ruzuku hatujui zinafanya nini. haya michango ya wafadhili yote hatujui inaenda wapi. michango tuliyochanga kupitia mitandao hatujui ipo mifukoni mwa nani. yaani abrakadabra tupu. ukihoji unaambiwa msaliti unafukuzwa chamani. hivi hiki ni chama au saccos ya watu wachache. jibu usiogope kufukuzwa. vyama vipo vingi usijali kamanda.
 
Lowassa alitajwa kuwa fisadi kwa mara ya kwanza na CHADEMA pale Mwembeyanga kwenye list of shame mwaka 2007 kabla hata report ya Mwakyembe iliyosomwa 2008.

Sasa CHADEMA walitumia report ya Mwakyembe yupi hiyo 2007? Au Mwakyembe ana report ngapi juu ya Edo?

In fact nyie jamaa wapumbavu tu na mnadhani kila mtu ni mbumbumbu kama nyie.
mkuu huu ni ukweliiii kabisa. si unajua watu wanatafuta hoja za kujihami. wanasahau hata miaka kama hivi. tena ina fwact wabunge wa upinzani walisaidia kuongezea hoja kwa kamati kwa sababu wapinzani walikuwa na data nyingi za huko nyuma. na walikuwa na hoja kwa nini walimwita fisadi
 
Back
Top Bottom