Ni tuhuma tu Lowassa kumbe si Fisadi!!

Ni tuhuma tu Lowassa kumbe si Fisadi!!

Allen kwa nini uwe na mgombea wako wa miakamingi then all over a sudden uchukue mtuhumiwa wako mwenyewe utake kumpa madaraka makubwa kabisa ya nchi?ili iweje?
Nataka tu uniambie hicho chama aliuziwa shilingi ngapi, hizo hela zilitoka benki au nyumbani kwake, na je kama serikali nayo ilipataka kodi yake kwenye hiyo biashara iliyofanyika. Halafu biashara hiyo ya kuuziana CHADEMA ilifanyikia wapi?
 
Wanajua wao wenyewe na pia kumbe wamekwepa kodi?hebu niambie alihukumiwa wapi na chadema kuthibitisha sio fisadi tena?
 
Unataka kuhamisha magoli wewe.

CHADEMA waliposema Lowasa ni fisadi walitoa ithibati gani?

Na mwaka jana ikawaje akawa si fisadi tena ilhali miaka nenda rudi mmeimba kuwa yeye ni fisadi?

Mbona ameshakujibu kwamba waliegemea kwenye report ya mwakyembe
 
kama unajua mahakama ndio yenye wajibu kwa nini wewe umejichukulia jukumu la kumsafisha mtu kwa wananchi! kwa mamlaka yapi ya kisheria. suala lingekuwa ni kuendelea kushinikiza sheria ichukue mkondo wake. tatizo watu wamekamba michuzi sasa wanatafuta namna ya ku justify na kuweka mazingira sawa.

Sio kweli chadema hawakukulupuka kumchukua Lowasa aliitwa akahojiwa na kamati kuu na yeye akatoka mbele ya waandishi wa habari na kusema nani muhisika wa RICHMOND.so kwenye level ya kuwajibika katika umma amefaulu.sasa kama kuna mtu anamashaka na na usafi wa LOWASA njia rahisi ya kuthibisha ni mahakamani tu katika hili CHADEMA wako safe side na mtoa mada yuko sahihi
 
Uliyeleta bandiko nakuona kama mtu mwenye uwezo finyu sana wa kujenga hoja na sii ccm kama unavyodai.

Kufikiri kwako kwa kutumia tumbo,kunakusahaulisha kwamba Chadema ni wajinga kuliko ccm kwa kupokea taarifa ya mwakyembe na kuifanyia kazi bila kujiridhisha.

Kwa hiyo nawapima chadema na kupata majabu kwamba ninyi ni ngao ya wezi na majangiri wa mali za umma.
 
Kila siku tunaambiwa ni kwa nini CHADEMA walikubali kumpokea Lowassa mtu waliyekuwa wanamtuhumu kwa ufisadi wakati akiwa CCM. Hoja hii ya kukera inayoshabikiwa na kundi la watu ya aina ya Mzee Mwanakijiji na Nyani Ngabu siyo tu ni dhaifu bali pia inakera.

Siasa si nasaba ya kiasili (Gene) kwamba ukizaliwa CCM basi ukoo wako milele utakuwa ni CCM ama CHADEMA, bali ni mchezo ambao kanuni yake kubwa ni kufanikisha Agenda inayokubaliwa na chama husika cha siasa. Lowassa alipokuwa CCM alikuwa ni kihimili cha mfumo wa chama hicho, kina Kikwete na wenzake walikuwa anamtumia Lowassa kuunganisha nguvu za wanaopingana ndani ya chama hicho.

Mtu mwenye nguvu kama hiyo ndani ya chama cha siasa unatarajia vipi wapinzani wake wasimshambulie. Halafu CHADEMA walikuwa wanatumia taarifa za Kamati ya Mwakyembe kumshambulia Lowassa na wala si nje ya taarifa hizo. Kusema kwamba kwa kuwa CHADEMA walisema Lowassa ni fisadi basi anakuwa fisadi ni jambo la kustaajabisha kabisa.

Hoja kubwa ya CHADEMA wakati ule na hata sasa ni kuwa kama kina Mwakyembe waliona Lowassa kaitia hasara nchi kwenye Kandarasi ya kufua umeme iliyohusisha Kampuni ya Richmond, kwa nini asifikishwe mahakamani? Kina Mnyika na Lema kwa kutumia mbinu za kisiasa walikuwa wanasema kuwa inakuwaje wezi wa kuku wako magerezani wakati Lowassa yupo mtaani anadunda?

Swali la Msingi kama ufisadi wa Lowassa ulitokana na CHADEMA kusema ni fisadi wao CCM kama chama msimamo wao wakati ule ulikuwaje, walikuwa wanaona kwamba Lowassa ni fisadi ama si fisadi? Ajabu kubwa kuliko yote ni ukiwauliza wana CCM ufisadi wa Lowassa ni upi wanaishia kusema waliosema Lowassa ni fisadi ni CHADEMA!!

Mpaka sasa Lowassa anatuhumiwa tu kwamba ni Fisadi lakini hakuna hoja au ushahidi mahsusi kuonesha kwamba yeye kweli ni Fisadi. Na inawezekana akawa "fisadi" kwa kutumia mbinu na sheria kama za Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na kina siye ndiyo tutakuwa Fethulla Gulen wa zama hizo!!

Hoja kwamba CHADEMA ndiyo "walisema" kuwa Lowassa ni fisadi ni za uwezo wa chini sana katika kujenga hoja. Tunataka mtu aje atuambie yeye anaposema kuwa Lowassa ni fisadi basi na atuambie kuwa ufisadi wake ni upi. Tumechoka kuishi kwa uvumi!!
Bado unamchukulia hela hiyo mzee mpaka sasa! Huna huruma kabisa japo ni Fisadi, acha kummalizia vihela vilivyobaki.
 
Kusema kweli tukio la CDM kumpokea Lowasa....limewabomoa sana kisiasa kwa wenye akili huru na kufikiria vyema......iwe kweli Lowasa ni fisadi au hata kama sio fisadi......!!!???

Kwangu mimi naona ndio limewajenga kisiasa zaidi kwasababu wameingia kwenye new dimension of politics.kuthibisha limewajenga kisiasa kama unawaza vizuri utagundua amri ya kukataza mikutano ya kisiasa anayelengwa ni lowasa eti mbunge wa chadema akiiandaa mkutano wa kisiasa asimualike mtu kutoka nje ya eneo husika.jamaa anawatisha kama nini,lowasa ndio alisababisha ccm waisahau zanzibar wakakumbuka shuka kumekucha ndio yakatokea yaliyotokea
 
Na mm sion mantiki ya ALLEN kumsemea lowassa kana kwamba ni marehemu.

Mbivu na mbichi anatambua Lowassa...kama kweli ni msafi c aweke mezani facts na atwambie sasa kama c mwizi yy,ni nani mwizi.

Meanwhile lowassa ni mwizi tu sababu kama anajiita mwanamabadiliko ni vyema angebadili nafsi na chama kama alivyofanya.
 
Meanwhile lowassa ni mwizi tu sababu kama anajiita mwanamabadiliko ni vyema angebadili nafsi na chama kama alivyofanya.
Mimi si mtetei Lowassa ila unaposema NI Mwizi basi utueleze na siye unaotuambia kuwa ni mwizi kuwa kaiba nini?
 
Ufisadi wa Lowassa haukuanzia Richmond, huu ni mdoogo kabisa na umefanyika mwishoni mwishoni wa maisha yake kisiasa. Aliyemtuhumu Lowassa kwanza kabisa alikuwa ni Nyerere, wakati huo Richmond wala haijasikika. Alianzia akiwa DG wa AICC, ghafula bin vuu, kijana mdogo, hana elimu yoyote wala taaluma inayozaa ukwasi (linganisha na topnotch Lawyer kama Chenge, wa Harvard. Lowassa kasoma nini? Wapi?) akajikuta anamiliki viwanja na majengo Arusha maeneo prime. Ikaongezeka maradufu alipokuwa Waziri wa Ardhi kajimilikisha prime areas nchi nzima.

Nchi ikapata njaa akapewa kazi ya kuagiza mchele toka Vietnam, walipokutana na VIP Engineering ya James Rugemarila miaka 20 kabla ya escrow. Yakaja mashangingi ya Wabunge, yumo. Haya yanafahamika kwa CCM na Watanzania na wikileaks. Majumba yake yanafahamika yanakaliwa na Balozi mbalimbali Oysterbay na Balozi za Tanzania huko nje. Hapo hujataja Richmond, wala Dr Slaa alichosema ni hela ya halmashauri na hela za AICC alizosena Lema wakimnadi Nassari. Slaa hadi akasema huyu si mwanaume kwa mila za Kimeru (???). Hakukanusha. Mchungaji Msigwa akafunga kazi kwa kusema yeyite anayemshabikia Lowassa apelekwe Mirembe kupimwa.

Ukitaka kumnasua Lowassa tuhuma za ufisadi kazi yako ni pevu. Richmond ni jambo dooogo sana na mwenyewe anajua.

Ulichofanya bado unaendeleza tuhuma.kwa logic ya kawaida kabisa ukiwa waziri wa ardhi alafu usiwe na ardhi ni ujinga mkubwa.hata mkapa aliingia ikulu mtu wa kawaida lakin alipotoka unakumbuka ?
 
Na mm sion mantiki ya ALLEN kumsemea lowassa kana kwamba ni marehemu.

Mbivu na mbichi anatambua Lowassa...kama kweli ni msafi c aweke mezani facts na atwambie sasa kama c mwizi yy,ni nani mwizi.

Meanwhile lowassa ni mwizi tu sababu kama anajiita mwanamabadiliko ni vyema angebadili nafsi na chama kama alivyofanya.

Kumbe umesahau alishatoka akijiba tuhuma za richmond
 
Nyani Ngabu kwa ivo hata nyie hamujui huo ufisadi uliokuwa unasemwa na CHADEMA?
ilikuwa ni political game,mumteme ili na sisi tumchukue, tuliwaimbisha wimbo ambao hata hamujui mtunzi wake hasa ni nani. Siasa tamu sana, inahitaji maujanja mwingi kama wa Mbowe c lazima uwe na PHD ya kemia
 
Mbona ameshakujibu kwamba waliegemea kwenye report ya mwakyembe
kuna mwanasheria mkubwa tu kule anaitwa tundu lissu naye aliegemea huko huko?maana alikuwa mstari wa mbele,what l know mwanasheria anatakiwa kufanya research nzuri tu kabla ya kuropoka kwa kuegemea ripot ya mtu mwingine,hapan fungua akili kidogo usogee mbele ni mzuri tu kwa vile yupo chadema akitoka utasikia mengi sana,natamani angejaribu kutoka siku moja aone unafik uliopo kule,me sina chama lakini sipendi kushikiw aakili.
 
Usisaha kwamba chadema ni chama cha siasa na wala sio mahakama ya kisutu.they have to take advantage of every cirmustatnce
 
Usisaha kwamba chadema ni chama cha siasa na wala sio mahakama ya kisutu.they have to take advantage of every cirmustatnce
That is not taking advantage of every circumstance!its thinking people are too stupid to realise someone is fooling us!u cannot go public accusing someone of corruption which u dont have any evidence merely because u r taking advantage of a situation!no usitudanganye walipoteza mwelekeo!
 
Soma uelewe kwanza!!
Kubali makosa Hawa viongozi wa chadema ni 'waongo walimsingizia muheshimiwa Dr Eduard Ngoyai' kuwa ni fusadi then from there we start maana kuna swali nakuuliza in advance can you trust someone who lied to u again?
 
Usilifanye jambo hili la binafsi (don't take it Personal) litakuumiza sana!! Elewa maudhui ya Mada kisha changia. Maswali yako mengi yamejibiwa kwenye mabandiko yaliyopita, kama unaweza yapitie utaelewa.
 
Back
Top Bottom