Ni Tanzania Pekee (only in Tanzania)

Ni Tanzania Pekee (only in Tanzania)

Ni Tanzania tu pekee siasa hazina ukomo muda wote ni siasa
 
Ni kweli na hiyo nikutokana na walio wengi mafisadi wa Mali za umma sasa akionekana amekosa ana amua ata kutengana na watu
 
Ni Tanzania pekee nchi hakuna watu kupanda madaraj ya vyeo kazini mpaka bwana yule aamue.
 
ni Tanzania pekee ambapo timu ya soka inamuuza mchezaji kwa USD 10000,,lakn kwenye hyo timu amecheza mechi 3 mwaka mzima,,lakn ile timu iliyomuuza yule mchezaji inataka tena kumnunua kwa USD 120,000,,,ni tz pekee
 
1. Ni Tanzania pekee ambapo principal pass ya kwenda chuo ni D mbili badala ya E mbili

2. Ni Tanzania pekee ambapo wakat Wa kufanya mtihani pass ni nyingine Baada ya kufanya mtihani Na matokeo kutoka inabadilishwa Na kupandishwa ghafla

3. Ni Tanzania pekee ambapo wahitimu wanafikiria kuajiriwa tuu

4. Ni Tanzania pekee ambapo wananchi wake wanakosea Kosa lilelile kila Baada ya miaka 5
 
Ni Tanzania pekee ambapo viongoz wa kiserikal hufanya kazi kwa matukio na matamko yasiyotekelezeka.
 
Hiyo ya PHD kutoweza kuongea kiingereza si Tanzania pekee..

Maprof wa urusi na china sio wote wanajua english, na hawaoni kama ni shida
Shida inakuja wao PhD zao hawakuzisoma kwa kiingereza, vipi aliyeipata PhD kwa lugha ya kiingereza?
 
Kuna haka kamsemo " ni Tanzania Pekee a.k.a Only in Tanzania" nimekuwa nikikutana nako kwenye nyuzi mbalimbali humu JF. Nimetumia muda mrefu kutafakari haka kamsemo na nimegundua kweli ni only in Tanzania kuna mambo mengi yanatokea yakushangaza kama si kutuaibisha watanzania.

Ifuatayo ni sehemu ambazo nimekuta huu msemo ukitumika.

Ni Tanzania pekee Tanzanite inachimbwa lakini soko kuu la Tanzanite ni Kenya na India.

Ni Tanzania pekee mwizi wa mali ya uma anajulikana lakini hachukuliwi hatua yeyote.
b4b3d1b37e190d66c0fad46d3c95f223.jpg

Ni Tanzania pekee mtu ana PHD lakini hawezi ongea kingereza.

Ni Tanzania pekee Mwenyekiti anajiuzuru tena kwa barua na mbwembwe tele kwenye media ila baada ya mwaka anarudi kwa ubabe nakudai na yeye ndiye Mwenyekiti halali.

Ni Tanzania pekee pesa za maafa/rambirambi zinageuka kuwa za lambalamba.

Ni Tanzania pekee Waziri Mkuu anaulizwa swali anajibu Naibu Spika.

Ngoja niishie hapo mengine mtaongeza wenyewe, maana ni Tanzania pekee ukiongea ukweli unaitwa mchochezi.
Huyo lipumba ni sawa na jiwe lilowashinda waash anatumika kuvuruga tu
 
2) Mramba na Yona umewasahu?

Vipi Sioi, Shose na Kitilaya hawajambo?

Na bado, ile ya kina Mramba wakati wa Kikwete ilikuwa pati-gazeti, sinema kamili mtaiona karibuni.
Ni tanzania pekee ambapo kabla moja linachukia kabila lingine kwa kuwa limewazidi kimaendeleo,
Ni tanzania pekee ambapo dini moja iko mbele kielimu na nyingine imeachwa nyuma sana
 
Back
Top Bottom