Ni sahihi Mkuu wa Majeshi(CDF) kufanya Press conference?

Ni sahihi Mkuu wa Majeshi(CDF) kufanya Press conference?

Kaongelea usalama wetu... nahisi igp hakuwepo nchini

Sent using Jamii Forums mobile app
Ninachofahamu Huyu ni MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA so sometimes anauvaa Upolisi na Muda mwingi anashinda na u Jwtz so yupo right.IGP ana report kwa CDF/anawajibika kwa CDF na ndiyo Maana ikitokea Mission ngumu CDF huchanganya Wafia Chama Tawala na watekeleza ya Chama na wote wanaenda kutetea Wakereketwa huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo alizofanya sana Shimbo.pinto akiwa mnadhimu. Haki yoyote inayoweza kuleta taharuki ya jamii na kutakatisha usalama, vyombo vyote cha ulinzi vinatumika. Tulioa jinsi Kibiti ilivyodhibitiwa baada ya kulishirikisha jeshi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
CDF naye, by virtue of being CDF, ni msemaji wa jeshi, hata kama si kwa title.

Kwa sababu huyo msemaji wa jeshi mwenyewe anapitisha mambo kwa CDF kabla ya kusema.

Ulichosemani kama unashangaa rais kufanya press conference badala ya Msigwa.

Kama rais anaweza kufanya press conference, kwa nini CDF asiweze?

Tatizo tumewafanya wanajeshi wetu kama miungu watu, we need to humanize them.

Hapo kafanya press conference tu hivyo, angeenda mashuleni kupigisha gwaride future recruits?
Issue hapa sio CDF kufanya press conference, bali issue ni content ya kile alichokizungumza. Bahati mbaya wengine tuko mbali hatujui nini alizungumza. Nimeona mtu mmoja amegusia kuwa alichozungumza kilipaswa kuzunguzwa pengine na IGP kwa kuwa alizungumzia mambo yanayohusu usalama wa raia, akimaanisha aliyozungumza ni mambo yanayoshughulikiwa na jeshi la polisi. Nadhani huyu ana hoja.

Na hoja yake inaweza kuwa na nguvu zaidi kwa wale ambao wameanza kuhisi kuwa awamu hii nchi inapelekwa "kijeshijeshi! Mnaona kilamkuu anapoenda sehemu anazungukwa na wakuu wa vyombo vya usalama, naye mara nyingi katika hotuba zake anatoa vitisho akisema vyombovya usalama vipo tayari kuwashughulikia, nakadhalika nakadhalika.

Kama CDF alifanya press conference kwa ajili tu ya kuzungumzia matukio ya ujambazi, basi inaweza kuwa ni katika mwendelezo huwa huo huo wa "kuijeshisha nchi"!
 
Una matatizo wewe, kila Jeshi lina mkuu wake. Fanya homework kidogo
Hujui kitu umekurupuka huyu ninae muulizia Mimi haitwi mkuu wajeshi huyu anaitwa mkuu wa majeshi ya ulinzi aukiswahili hujuwi mtu unapo ullizwa swali kwanza tulia ili ujibu vizuri sasa hapo mwenyematatizo Mimi au wewe
 
Kumbuka major general kavamiwa na kupigwa risasi hivyo sio ishu yeye kuja na kulizungumzia hilo tukio na kutuliza hali inayoendelea nchini

Major general mtu mkubwa ase jeshini nadhani lengo haswa ya press ilichagizwa na major general kuvamiwa kwa bunduki

Weka neno "Mstaafu"
 
Ndio ni lazima.
Bora wewe umejibu kuna jamaa amekurupuka kajibu oh kila jeshi lina mkuu wake wakati huyu haitwi mkuu wajeshi huyu anaitwa mkuu wa majeshi yaulinzi lakini ujasema sababu kwanini hutoka jwtz tu kila teuzi kwanini asitoke police,magereza,uhamiaji,zimamoto,usalama wataifa au mgambo ndio swali langu
 
Kwa mara ya kwanza toka niwe na ufahamu leo ndiyo nimeshuhudia mkuu wa Majeshi ya Tanzania akifanya press conference badala ya msemaji wa jeshi.

Sikuishuhudia hii kipindi cha Mwamunyange, waitara nk.

Je ni nini kimemsukuma Jenerali Venance Mabeyo kufanya alivyofanya leo?
Swali hili sasa sijui ujibiweje,we mwenyewe umeshasema huyi ni mkuu wa majeshi alafu unauliza swali eti ni kama unashangaa.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Flashback 2010...

Wangapi wanakumbuka kilichotokea tukielekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010? Zilikuwa zimebakia siku 30 tuingie kwenye uchaguzi CCM ikiwa imekabwa koo na Chadema and guess what? Ghafla akajitokeza Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Kanali Abdulrahman Shimbo na huku akiwa amezungukwa na maafisa wa juu wa Polisi na TISS akatoa kauli ya vitisho kwa wananchi akiwataka wawe tayari kupokea matokeo yoyote yale yatakayotangaza na tume.

pic.jpg

​
Hili lilikuwa ni tukio la kushangaza lililowaacha wanachi mdomo wazi wakijiuliza Jeshi na Siasa wapi na wapi. Hata hivyo saluti zimwendee aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya ulinzi wakati huo Jenerali Davis Mwamunyange kwa kutojiingiza katika kinachoweza kutafsiriwa tu kama mbinu ya kuwatia woga wapiga kura.

Fast Forward 2017...

Safari hii Mkuu mwenyewe wa Jeshi Jenerali Venance Mabeyo kajitokeza kuongea na vyombo vya habari akiwatahadharisha wananchi, je kulikoni? Naambiwa na huko Bungeni Spika Ndugai kawa mbogo anawatisha hadi Wabunge na tayari Mbunge moja wa Upinzani Mh. Tundu Lissu tayari anapigania uhai wake mwili wake ukiwa na majeraha ya risasi kumi! Watanzania tunaelekea wapi? Je kwa mwendo huu tutafika?
Kwa tathmini yako unadhani mnadhimu alichukua hatua binafsi na Mwamnyange hakujua. Kweli hii JF imejaa vyura baada ya GT
 
Amefanya hivyo ni kwaajili ya kuhakikisha amani yetu haiharibiwi.But sayansi ya akili inasema kuwa amani huwa ktk nafsi ya mtu,hivyo basi njia ya kudumu ktk kuleta amani ya kudumu ni kutibu mawazo ya wengi.Maana bila kufanya hivyo kutakuwa na utulivu wa muda mfupi.
 
Kwa tathmini yako unadhani mnadhimu alichukua hatua binafsi na Mwamnyange hakujua. Kweli hii JF imejaa vyura baada ya GT
Wapi nimesema hivyo? Nilichosema ni kuwa aliyejitokeza kuongea na wanndishi wa habari ni mnadhimu wa Jeshi. Uzuri wa vyura ni kwamba hawana unafiki na hawapakatwi na madikteta uchwara.
 
Ni Mambo ya usalama wa raia ambayo yapo chini ya Polisi.
is petty issues kuwa discussed na yeye
Usalama wa raia hauko chini ya polisi.. sema unasimamiwa.. na polisi.

Kwan jwtz kazi yake nin?

Sent from "La -Vista"
 
Wapi nimesema hivyo? Nilichosema ni kuwa aliyejitokeza kuongea na wanndishi wa habari ni mnadhimu wa Jeshi. Uzuri wa vyura ni kwamba hawana unafiki na hawapakatwi na madikteta uchwara.
Kasome vizuri ulichokiandika. Halafu ndiyo ulete kashfa mkuu. Mimi ni muungwana situkani nakupa nafasi ya kujirudi.
 
Kumbuka major general kavamiwa na kupigwa risasi hivyo sio ishu yeye kuja na kulizungumzia hilo tukio na kutuliza hali inayoendelea nchini

Major general mtu mkubwa ase jeshini nadhani lengo haswa ya press ilichagizwa na major general kuvamiwa kwa bunduki

Hali isipotulia nani atafanya press conference?? Zaidi yake??
 
Back
Top Bottom