Ni sahihi Mkuu wa Majeshi(CDF) kufanya Press conference?

Ni sahihi Mkuu wa Majeshi(CDF) kufanya Press conference?

Hata tulipopigana na Idd Amin Dada sikumsikia Generali Twalipo akifanya press conference
'mungumtu' anamshirikisha kila ghafla,hivyo naona ameona atoke aonyeshe naye yumoyumo katika kiti cha enzi
 
cdf ache ukabila Kuwait msukuma haina mana kushusha hadhi ya jeshi
Inawezekana wewe ndiye uliyelipandisha sana hadhi jeshi kama bado tuko enzi za Uhuru na Mzalendo, wakati leo ni enzi za kidigitali.

Sema CDF kakosea neno hili au lile, lakini CDF kuongea katika press conference si kosa.

Waandishi wa habari wanalalamika sana kwamba viongozi hawapatikani kuulizwa maswali.

Huyu ni kiongozi wa wapiganaji wa watu,sasa anapotaka kuongea moja kwa moja na waandishi wa habari ambao wanawapasha habari watu, waandishi wanatimiza wajibu wao na watu wanapata haki yao ya kupata habari, tatizo liko wapi?

Ulitaka viongozi wajifungie hawapatikani waandishi washindwe hata kuuliza maswali moja kwa moja?
 
Kwa mara ya kwanza toka niwe na ufahamu leo ndiyo nimeshuhudia mkuu wa Majeshi ya Tanzania akifanya press conference badala ya msemaji wa jeshi.

Sikuishuhudia hii kipindi cha Mwamunyange, waitara nk.

Je ni nini kimemsukuma Jenerali Venance Mabeyo kufanya alivyofanya leo?
Wala Mboma,,,ht mimi pamoja na umri wangu huu mkubwa sijawai ona
 
Kumbuka major general kavamiwa na kupigwa risasi hivyo sio ishu yeye kuja na kulizungumzia hilo tukio na kutuliza hali inayoendelea nchini

Major general mtu mkubwa ase jeshini nadhani lengo haswa ya press ilichagizwa na major general kuvamiwa kwa bunduki
Bora angeongelea hayo mambo ya Meja Jeneral...ila kaongelea mambo ya Kibiti..wapi na wapi..

Ops za kijeshi huwa ni chini kwa chini..kimya kimya...raia wanaona matokeo tu
 
Tena anasema "sitaki kuingia hukoo".. (kwenye politics). Kwa mbali akili yake inamwambia anachofanya si sawa kabisa yet anaendelea kukifanya. Hayo ya kuwatoa hofu ati vyombo vya ulinzi vipo kazini ilipaswa kuwa kazi ya mtu kama Waziri wa Mambo yetu ya kule ndani. Watu wameona ombwe na sasa wanakamata fursa.
 
Tena anasema "sitaki kuingia hukoo".. (kwenye politics). Kwa mbali akili yake inamwambia anachofanya si sawa kabisa yet anaendelea kukifanya. Hayo ya kuwatoa hofu ati vyombo vya ulinzi vipo kazini ilipaswa kuwa kazi ya mtu kama Waziri wa Mambo yetu ya kule ndani. Watu wameona ombwe na sasa wanakamata fursa.
Maana yake kalazimishwa kuongea aliyoongea kutoka mamlaka za juu
 
Bora angeongelea hayo mambo ya Meja Jeneral...ila kaongelea mambo ya Kibiti..wapi na wapi..

Ops za kijeshi huwa ni chini kwa chini..kimya kimya...raia wanaona matokeo tu
Tatizo umesikiliza video iliyokatwa yenye dakika 2 tu ,tafuta full video


Kumbuka ile ni press kuna maswali hivyo kama yeye mkuu wa majeshi yote ikiwepo police alisema haina haja ya kupanic na kugusia kibiti sijaona tatizo
 
Ni sahihi Kabisa CDF kurelease Press, Kumbuka huyo ni Acting Leader akitoka Raisi anakuja CDF kwa Maamuzi hao kina Prime minister, VP ni Ceremonial figures mbele ya CDF

Sent using Jamii Forums mobile app

Simaanishi kwamba watu ni kuku, ila kama kawaida napenda kuandika kwa mifano ili point ieleweke vizuri.

Kuku aliyezoea kufungwa kamba mguuni, hata siku ukiiondoa ile kamba anakuwa haamini na haelewi kwamba ile kamba imefunguliwa.

Anacheza pale pale alipozoea.

Ukimfukuza aende kucheza mbali, anakataa.Anarudi pale pale alipozoea.

Tumezoea kuwa na jeshi lililo detached. CDF anaonekana kama Mungu mtu fulani ambaye hatakiwi kuongea na waandishi wa habari.

Akija CDF anayetaka kuwapa watu habari moja kwa moja,tunashangaa na kuhoji.

Kama kuku ambaye alizoea kufungwa kambamguuni anavyokataa kucheza mbali na sehemu aliyozoea, hata baada ya kufunguliwa kamba.

Wanajeshi waliosoma siku hizi wanajua umuhimu wa kuwa karibu na media. Wanajua umuhimu wa kuonyesha a human face of the armed forces.

Nimepita Brooklyn Marcy Projects nimekuta polisi wanaendesha baiskeli huku wamevaa vipensi, wanacheza mpira na vitoto vya uswahilini Brooklyn.

Kesho kukitokea uhalifu, polisi akija uswahilini anaonekana huyu si mgeni, alikuja jana tumecheza naye mpira, mtu poa sana, watu wanamuamini, wanampa nyeti.

Sisi CDF anataka kuwa karibu na waandishi wa habari na wananchi, baada ya waandishi kulalamika sana kwamba hawapatiwi habari directly, wananchi wanahoji na kushangaa.
 
Back
Top Bottom