Ni sahihi mke kufua boxer/kufuli la mume wake?

Unamkuta kabisa mwanaume anatoka bafuni ameacha boxer kwenye ndoo hii ni haki kweli? Kwanini Maudie boxer na ma kufuli yenu?
Mke wangu ana haki wa kufua kila kilicho changu kinachohitaji kufuliwa!

Huu ni mgawanyo wa majukum ambao kwa jamii zetu hilo jukumu linawaangukia wanawake! Hivyo ni sahihi kabisa na inabidi iwe hivyo!
 
Kama haupo radhi kufua boxer ya mumek tena KWA UPENDO MKUBWA (yaani unaifua ukiwa unawaza mnavyoridhishana), basi una hasara! Huyo mumeo ataishia kwa mchepuko au hata 'amtaifishe' beki tatu. Na kama unaona uzito sa-a-na kufua boxer ya mumeo humpendi. Mbona sisi tunawafulia wake zetu zao na wanatupenda kupindukia kwa sababu tunawaonyesha kuwajali?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni kuona boxer ni nguo fulani ya siri,uchafu...vinginevyo ungefua tu kama unavyomfulia suruali. Kuepuka yote hayo nunua washing machine.
 
Penzi lenu linaendeleaje mkuu ?
Hongera sana mpaka nimeingiwa na wivu.

Mungu ni mwema na kila siku linazidi kunawiri.Imagine una mke,unatoka kazini unamkuta na yeye amefika mda si mrefu,amemaliza kukamua maziwa ya mtoto kwaajili ya kesho,lakini anakuomba uvue nguo ulizotoka nazo kazini anaenda kuzifua mwenyewe,hasemi amechoka wala haoni uvivu.Wakati mwingine najishtukia mpaka nakuwa mkali na kumwambia acha tutafua weekend ila hataki.

Mke Mwema hutoka kwa Bwana,ila mwanamke mtiifu unamtengeneza mwenyewe.
 
Kama ni upendo basi na mimi niweke zangu Tena zile za kwenye safari to the moon afue
Sasa hapo ni kushindana, kuna mambo ambayo kama mwanamke unapaswa uyafanye si tu kwa sababu mwanaume hawezi, hapana ni sababu ni jukumu lako kama ilivyo kupika au hata kutenga chakula mezani. Si kwamba mwanaume hawezi kupika au kutenga chakula anaweza lakinii mwanamke ni jukumu lako. Na akiamua kujitengea au kujifulia nguo za ndani ni kwa mapenzi yake kwako....

Mie nitafua tuu
 
Akiwa mgonjwa sawa lakini si akiwa mzima ana watch TV Mimi ni afya viboxer vyake
Usipende kuhesabu unayomfanyia mwenzio kwani nae akianza kuhesabu anayokufanyia mtafika kweli mfanyiane kwa ajili ya upendo eti yeye anaangalia tv kwanini asifue Itakuwa nyumba ya mashindano sasa
Mbona kufua boxer ni kitu kidogo sana sijaona tatizo au cha kukufanya ulalamike

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom