Ni rahisi sana Afrika (Tanzania) kurudi utumwani

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,030
12,353
Kwa jinsi bara la Afrika linavyo endeshwa hasa kusini mwa jangwa la sahara.

Huwa naumia sana nikiona kwa jinsi tunajirudisha tena utumwani na kwenye ukoloni.

Nchi yangu Tanzania kwa nini viongozi wanarudisha wajukuu zetu kwenye utumwa na ukoloni kila dalili za kurudi kwenye ukoloni zina onekana wazi wazi.

Kwa hiyo tumeamua kuipuuza historia ya utumwa na ukoloni ya kale na sisi tunataka kutengeneza ya kwetu mpya ?

Katika jambo linalo niumiza na kuwa kama laana kwangu basi mimi kuzaliwa mwafrika hii ni laana kubwa sana kwangu mpaka sasa.

Nimezaliwa katika bara la ajabu ambalo halijali kuhusu future ya vizazi vyake bali matumbo yenye njaa.

Hata kama mimi nimekataa kupata mtoto Afrika lakini naona huruma kwa ndugu zangu kurudishwa utumwani na kwenye ukoloni tena.

Hatujifunzi, kwa nini hatujifunzi ? na kwa nini hatukaki kujifunza ?

Tunaidharirisha ngozi nyeusi duniani kote kuonekana ya kipumbavu na inastahili kubaguliwa kwa kiwango cha juu, kama sio laana Afrika ina nini cha kuifanya isionekane imelaanika.

Afrika ndio bara pekee population kubwa haijitambui kabisa ipo usingizini.

R.I.P Abushiri
R.I.P Kinjekitile
R.I.P Mkwawa

KUZALIWA AFRIKA NA KUWA MWAFRIKA NI LAANA KUBWA SANA
 
Kwa jinsi bara la Afrika linavyo endeshwa hasa kusini mwa jangwa la sahara.

Huwa naumia sana nikiona na kwa jinsi tunajirudisha tena utumwani na kwenye ukoloni.

Nchi yangu Tanzania kwa nini viongozi wanarudisha wajukuu zetu kwenye utumwa na ukoloni kila dalili za kurudi kwenye ukoloni zina onekana wazi wazi.

Kwa hiyo tumeamua kuipuuza historia ya utumwa na ukoloni ya kale na sisi tunataka kutengeneza ya kwetu mpya ?

Katika jambo linalo niumiza na kuwa kama laana kwangu basi mimi kuzaliwa mwafrika hii ni laana kubwa sana kwangu mpaka sasa.

Nimezaliwa katika bara la ajabu ambalo halijali kuhusu future ya vizazi vyake bali matumbo yenye njaa.

Hata kama mimi nimekataa kupata mtoto Afrika lakini naona huruma kwa ndugu zangu kurudishwa utumwani na kwenye ukoloni tena.

Hatujifunzi, kwa nini hatujifunzi ? na kwa nini hatukaki kujifunza ?

Tunaidharirisha ngozi nyeusi duniani kote kuonekana ya kipumbavu na inastahili kubaguliwa kwa kiwango cha juu, kama sio laana Afrika ina nini cha kuifanya isionekane imelaanika.

Afrika ndio bara pekee population kubwa haijitambui kabisa ipo usingizini.

R.I.P Abushiri
R.I.P Kinjekitile
R.I.P Mkwawa

KUZALIWA AFRIKA NA KUWA MWAFRIKA NI LAANA KUBWA SANA

Baada ya miaka 50, 100. Wamiliki wa hili bara la Afrika watakuwa Wachina, Wahindi, Wazungu na Waarabu.

Kama ilivyo Afrika Magharibi kwa sasa. Mauritania, Egypt, Morocco, Tunisia Algeria, Libya, Au Afrika kusini sasa, USA kwa sasa, America ya kusini kwa kiasi kikubwa.

Na wataandika historia yao kwamba walikuwepo toka miaka 5000 iliyopita. Historia inaandikwa siku zote na mshindi. Marehemu, kaburi haliwezi kujitetea.
 
Sisi tutakuwa tumeganyika tukiwa asilimia ndogo ya wananchi hizi kama ilivyo USA, South Amerika, North Afrika, Europe.

Kwahiyo tutakuwa minority kila sehemu, sera za kufikia hayo malengo ni vita ya wenyewe kwa wenyewe, uzazi wa mipango, magonjwa, ugumu wa maisha
nk.
 
Kwa asilimia kubwa wananchi wa hili bara wanatanguliza kabila, ukanda, dini, familia, ukoo, ubinafsi zaidi ya uzalendo na maslahi ya Taifa. Sio kama miaka 40 iliyopita.
 
Kazi iendelee

Tatizo letu wabongo ni kujifariji tu hatuna tofauti na wale wanawake wanaokutana sehemu kwa ajili ya kupiga umbea au kumuongelea mtu fulan ambae hata baada ya kumwongelea yale maneno hayatombadilisha kwa lolote sasa naona nanyi mnaiongelea serikali ilhali mnajua kuwa hakuna hatua yoyote itachukuliwa kwanin msikae kmy ili yajayo yawafurahishe siku mkijikuta asubuh mnaambiwa ni safari ya kwenda china najua wengi huwa mna ndoto mfike nchi za wenzetu sasa hamuoni kuwa hiyo ni fursa

MUNGU IBARIKI NCHI YANGU
 
Angalia Niger, Mali na Bukina Faso,Jeshi limewaondoa Maraisi Wao wapenda rushwa na vibaraka wa Magharibi, sasa badala ya kutafuta kiongozi mwema na kumsimika, wanaenda Urusi(East) kuomba msaada wa kusaidiwa ili Wao wabaki madarakani. Yaani nilichoka, alafu Brother Prigoziny kabla hajadunguliwa ma Putin kajirusha mtandaoni anasema kabisa tupo Africa kuifanya Urusi kuwa KUBWA. Kwanini sisi Waafrica( Ham/Cush) atustuki kwamba Japhet(Magharibi) na Shem(Mashariki) wanatuchezea kwa kubadilishana ukoloni?. Je atuwezi ishi bila ya US, China au Russia?
 
Kwani ni lini Afrika ilipata Uhuru! Bado tuko utumwani.
Tuanze harakati za kujikomboa.
Kwa Mikataba hii ya madini na bandari unadhani Sisi ni watu huru? Aibu sana
 
Hakuna baraka bali bara hili limejaa laana
Unaona ktk uono hafifu!!

1. Madini yote,yanatoka Africa,

2. Malighafi zote hutoka Africa, ambazo hutumika kuzalisha bidhaa na vifaa vyote adimu.

3. Hata kabla ya mashine kugunduliwa, watumwa walitoka Africa kwenda kuzijenga Nchi maskini za ulaya na kuzitajirisha.

4. Mali asili ,misitu mizuri na Kila fursa zipo Africa.

5. Ni bara pekee ambapo unaweza kufanya KILIMO msimu mzima, mabara mengine ni barafu ktk baadhi ya misimu.

Narudia kusema Bila Africa, mabara mengine yasingekuwa yalivyo Leo, hivyo Africa ni BARAKA.

Hao unaowaona wamebarikiwa ndo chanzo Cha Umaskini wa Africa.

Naipenda Africa, Najivunia Kuzaliwa Africa,

Naipenda Nchi yangu nzuri TANZANIA, pia Najivunia Kuzaliwa Tanzania.

Aamen.
 
Ilibidi wafanye hivyo kujilinda kwa muda baadaye watawaambia warudi nyumbani. Ufaransa na USA wana majeshi nchi jirani na maslahi muhimu kwenye hivi nchi kama Uranium, madini. Inasemekana boko haram na vikundi vingine vya kigaidi vina support ya hizi nchi kisirisiri.
 
Back
Top Bottom