Nakala ya kwanza ya kitabu cha Magufuli yauzwa Malawi

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Kutoka Lilongwe - Malawi
IMG-20230710-WA0008.jpg


Nakala ya Kwanza ya Kitabu Kipya Cha Hayati Rais Magufuli Kama kilivyoandikwa na Profesa wa Chuo kikuu Cha Hebron Nchini Malawi Prof Malango Chinthenga kimeuzwa kwa USD 600 sawa na Tsh 1,450,000/= kwa Mwananchi wa Kawaida wa Malawi ambaye alijitokeza katika Uzinduzi wa Kitabu hicho jijini Lilongwe, Kitabu hicho chenye kurasa 461 na Chapter zipatazo 48 kimeanza kuwa Gumzo Kubwa Barani Afrika

Kitabu kinaitwa "AFRICA MAGUFULI AND CHANGE" an integrated Approach in abolishing Africa's modern economic Slavery",

kwa tafisiri isiyo Rasmi Ni "AFRIKA MAGUFULI NA MABADILIKO" Namna, Njia ya Kutokomeza Utumwa wa Kisasa wa Afrika Kiuchumi"

Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Kitabu Hicho jijini Lilongwe Dr Grace Kumchulesi ambaye Ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Maendeleo ya Serikali ya Malawi anasema:

Kutokea Hapa Malawi tutajitahidi kusambaza Kitabu Hiki katika Vyuo vyetu Vyote kwa ajili ya Vijana wetu Kujifunza Nini Maana ya Uongozi na Ukombozi wa Bara la Afrika kutoka katika Ukoloni Mambo leo na Utumwa wa Kiuchumi Afrika, tutasambaza Kitabu Hiki Afrika Nzima na Kitatafsiriwa kwa Lugha Mbali Mbali kulingana na Nchi Husika, na kwa Upande wa Tanzania ambako ndipo Shujaa huyu wa Afrika alipozaliwa tumeomba Kitafsiriwe kwa Kiswahili, na Tayari Mawasiliano yamefanyika Kati ya Profesa Chinthenga na Tanzania Publications House (TPH) kwa ajili ya kuchapwa kwa Lugha ya Kiswahili na Kitatafsiriwa na Chuo Kikuu Kimoja Nchini Tanzania - Dr Grace Kumchulesi.

Kwa Uchache hizi Ni Baadhi ya Chapters ktk Kitabu Hicho ambacho generally kinaelezea Namna Ambavyo Africa inapaswa Kujiondoa katika Utumwa na Ukoloni Mamboleo.

Chapter 10 - inaelezea Namna Utegemezi wa Misaada na Mikopo isiyo ya Lazima inavyoua Nchi za Afrika.

Chapter 23 - inaelezea Falsafa Mpya iitwayo "MAGUFULIFICATION" inavyofaa Kutumika kulikomboa Bara zima la Afrika kutoka katika Minyororo ya Utumwa na Ukoloni Mamboleo.

Chapter 48 - inahitimisha kwa kusema Kwamba Afrika imepoteza Nguzo na Mfano wa kuigwa katika Uongozi, Afrika ingetamani ipate Magufuli Mwingine "Wish for a New Magufuli" for whom "We can not wait to find One".
 
Huu uzi hautopata wachangiaji kwa sababu ni anasifiwa JPM, lakini ingekuwa ni Mbowe/Lissu ungekuta huu uzi una page 100+ mana hata uongozi wa JF wangeupigia debe.
 
Back
Top Bottom