Ni nini kazi ya Katibu Mkuu Kiongozi?

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,886
Katibu mkuu kiongozi anafanya kazi gani? Kuna umuhimu wa mtu kuwepo kufanya kazi hiyo?
 
Katibu mkuu kiongozi anafanya kazi gani? Kuna umuhimu wa mtu kuwepo kufanya kazi hiyo?
Kikatiba ni mtumishi wa umma lakini kiutendaji ni mtu wa karibu mno na kiongozi wa nchi .Ni mkono wa kulia wa Rais.Yeye ndiye mkuu wa watumishi wa umma,ndiye kiongozi wa makatibu wakuu wote,NI KATIBU WA BARAZA LA MAWAZIRI (Baraza la mawaziri ndiyo serikali yenyewe).Kwa ujumla baada ya Rais ndiye mtu wapili kujua mambo actually karibu yote ya serikali.
SI MTU MDOGO HATA KIDOGO!!
 
Katika utendaji wake na wa waziri mkuu, utofauti wao ni nn?
 
Katika utendaji wake na wa waziri mkuu, utofauti wao ni nn?
Cabinet Act No.15 of 1984 Art.9 60.
There shall be a Secretary to the Cabinet who shall be the chief executive officer in the office of the Cabinet, and he shall discharge the following functions, in compliance with the general or specific directions issued to him by the President, that is to say: (a) to work out a programme for Cabinet meetings and prepare the agenda for each meeting;
(b) to record minutes and maintain a record of Cabinet meetings;
(c) to notify and explain the decisions of the Cabinet to every person or public institution concerned with any such decision; and (d) to discharge any other duties and functions as shall be directed 41 from time to time by the President.
Kikatiba Waziri Mkuu ni kubwa kwa maana ya kuwa ikiwa Rais na Makamu wa Rais hawapo waziri Mkuu ndiye anyeweza kuwa Mwenyekiti wa Baraza la mawaziri.Kiutendaji Katibu Mkuu kiongozi yupo karibu mno na Rais (Jana umesikia kuwa kuna wakati akitaka kutumbua Kijazi alikuwa akimwomba apoe kidogo,sidhani kuwa katika tumbua na tengua kuna ushauriano na Waziri Mkuu.TUJADILI
 
Kikatiba ni mtumishi wa umma lakini kiutendaji ni mtu wa karibu mno na kiongozi wa nchi .Ni mkono wa kulia wa Rais.Yeye ndiye mkuu wa watumishi wa umma,ndiye kiongozi wa makatibu wakuu wote,NI KATIBU WA BARAZA LA MAWAZIRI (Baraza la mawaziri ndiyo serikali yenyewe).Kwa ujumla baada ya Rais ndiye mtu wapili kujua mambo actually karibu yote ya serikali.
SI MTU MDOGO HATA KIDOGO!!
Kwa hiyo ni kama katibu wa serikali. Ana kazi muhimu sana. Kwa nini hii kazi asiifanye waziri mkuu na badala yake PM anazururazurura tu?
 
Hii article (c) ndo hua inanichanganya. Nashindwa kumtofautisha na prime minister as all we know prime minister has mandate of give directions and instructions to any institution in the country the same applies to chief secretary.
Kwa jinsi nilivyoelewa. Huyu katibu mkuu hatoi maelekezo bali anafafanua maamuzi ya baraza la mawaziri kwa watu na taasisi.
 
Yaani ni kama Mungu na mwanae wa pekee, Yesu Kristo, ukaribu wa Mkuu wa nchi na Katibu Mkuu kiongozi. Sijui umeelewa? Maana tukikupa vifungu vya sheria ujue wajibu wa CS, hutajua vema. Umeelewa au bado umelewa?
 
Katibu Mkuu Kiongozi Kwa mujibu wa Kifungu cha 4(2) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298, Katibu Mkuu Kiongozi ndiye Mkuu wa Utumishi wa Umma. Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 4(3)(d) ni Mamlaka ya Nidhamu kwa watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais. Kifungu cha 4(4) kinampa katibu Mkuu Kiongozi uwezo wa kuwa Mamlaka ya Nidhamu ya juu katika Utumishi wa Umma. Hivyo, anaweza kumchukulia hatua za kinidhamu mtumishi mwingine yeyote kwa kadri atakavyoona inafaa. Watumishi wa Umma ambao Mamlaka yao ya Nidhamu ni Katibu Mkuu Kiongozi watakata rufaa kwa Rais.

Sheria hiyo ya Utumishi wa Umma Sura 298, ilifanyiwa marekebisho katika Kifungu cha 4(3) kupitia Kifungu cha 69 cha Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali namba 13 ya Mwaka 2019 kwa kumpa Katibu Mkuu Kiongozi Mamlaka ya Mwisho ya Uhamisho.

MAREKEBISHO yaliyofanyika katika Sheria ya Utumishi wa Umma Sura 298, yamempa Katibu Mkuu Kiongozi mamlaka ya mwisho ya uhamisho wa watumishi wa umma, hivyo kutopingwa au kutotenguliwa na mamlaka nyingine.
 
Attachments

  • 1572961503___MISINGI YA SHERIA KATIKA KUSIMAMIA HAKI NA WAJIBU WA WATUMISHI WA UMMA.pdf
    264.3 KB · Views: 64
4(3)(d) ni Mamlaka ya Nidhamu kwa watumishi wa Umma wanaoteuliwa na Rais.

Kwenye hiyo sehemu hapo juu. Anaweza wajibisha mawaziri? Au hayo mamlaka yake yanaishia wapi?
 
Kikatiba ni mtumishi wa umma lakini kiutendaji ni mtu wa karibu mno na kiongozi wa nchi .Ni mkono wa kulia wa Rais.Yeye ndiye mkuu wa watumishi wa umma,ndiye kiongozi wa makatibu wakuu wote,NI KATIBU WA BARAZA LA MAWAZIRI (Baraza la mawaziri ndiyo serikali yenyewe).Kwa ujumla baada ya Rais ndiye mtu wapili kujua mambo actually karibu yote ya serikali.
SI MTU MDOGO HATA KIDOGO!!
Mkuu samahani,ukilinganisha na government ya u.s.a,
Huyu ni kama chief of staffs au ?
 
Back
Top Bottom