Ni nini hatma ya Mahakama ya Mafisadi?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
Hii mahakama iliasisiwa na Mwendazake Pombe Magufuli John alipokuwa Rais kwa kulazimisha wa awamu ya tano.
Haipo kikatiba
Haipo kisheria
Haipo kwenye ilani ya chama. Iliasisiwa kwa maono kimo cha mbilikimo! Kwa kutumia nguvu kubwa na maarifa kidogo.

Sikumbuki kuona kesi zilizohukumiwa na hii Mahakama (nakubali kukosolewa). Nyingi ushahidi umekuwa ni changamoto hivyo kufanya zisuesue. Nyingi ni za kisiasa na kukomoana. Nyingine zilikuwa za visasi na kubambikiwa.

Matendo ya Mungu si ya binadamu. Pombe Magufuli hatunaye tena na zimeshatimia siku 100 na ushee toka atwaliwe kutoka maisha haya. Mama Samia Rais wa sasa ameonesha nia njema ya kutofautiana na mtangulizi wake. Walioitwa mafisadi na kupewa kesi kubwa kubwa za uhujumu uchumi wanafutiwa mashtaka na kuachiwa huru.

Waliokuwa wamehukumiwa kisiasa na kulipishwa faini za dhuluma wanarudishiwa pesa zao! Huu ni mwanzo wenye nia njema..Kazi bado ni pevu na kuna mengi ya kuweka sawa. Na mojawapo ya hayo ni hii mahakama ya mafisadi! Tunasubiri kuona hatima yake na hasa ikivunjiliwa mbali na kuokoa kodi zetu

Mama unapitapita huku. Naamini utasoma na hili.
 
Mkuu unatutafutia Nini kwani? Fisadi gani ambae angekamatwa wakati Kama tu Chenge tu mdogo tumeshindwa kumtia hatiani vipi wenye hela zao ? Ikiwa wenye vijisenti tumeshindwa😭😭😭😭
 
Huyu mama ataishi miaka mingi sana kama ilivyo kuwa watawala wa kiislamu baada ya kuwatendea watu makuu.Hakuna zawadi yenye thamani duniani kama kuwaunganisha watu tena waliotenganishwa na familia zao kwa dhuluma na uonevu baada ya kugoma kuisujudia Sanamu wakabambikwa kesi.
 
Neno " fisadi" au "mafisadi", hapa Tanzania linatumika na wanasiasa ili kujinufaisha wao.

Kwahiyo neno hili hutumika kuwatukana watu kisiasa.
 
Hii mahakama ya mafisadi Ingekuwa active kama mafisadi wangekuwa ni wapinzani.Aliianzisha bila kuwaza wateja wake wakuu wangekuwa ndugu zake ccm.
Ndio maana kampani ya sabaya inaumia sana sasa hivi ikiona mafisadi wa kweli ndio wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria
 
Katika kampeni ya Urais Magufuli akiwa na Samia walituahidi watanzania kuwa wataanzisha mahakama ya mafisadi.
Ahadi ya Wagombea Urais ni swala la kiilani vile vile.
 
I wish angekuwepo ili nimuulize kuhusu matokeo ya ile tume iliyo ongozwa na "Mjamaa na Comrade" Dr. Bashiru Ally akishirikiana na Wajumbe wake akina Albert Chalamila, kuchunguza mali za chama!

Sijawahi kusikia kuna Kigogo yoyote ndani ya chama akifikishwa kwenye hiyo mahakama kwa ufisadi, ubadhirifu, matumizi mabaya ya madaraka, nk.
 
Wote walikuwa 'wenzetu'
 
Haha. Kwamba mafisadi wajiachie? Ila nyiee watanzania hamutakaa mukapiga hatua Moja mbele maana mnapenda kurudi rudi nyuma Sana.
 
Back
Top Bottom