Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 18,190
- 29,937
Nimeona mtandsoni waziri Wa Ujenzi, Bw Ulega akijipigia sound at serikali itajenga Flyover Mwenge na Morocco.
Kama mkazi wa Dar, nikikumbuka hizi sinkelele za kwanzankuzisikia.
Zaidi ya miaka mitano iliyopita tulisikia kuwa kuna Flyover tano zitajengwa Dar. Flyover hizo ni Mwenge, Morocco, Magomeni, Kwa Mkuu wa Mkoa na Buguruni.
Hizi zote zilikuwa ahadi hewa.
Kumbukumbu zangu nafikiri(sina uhakika) Mkuu wa Mkoa wa Dar ndiyo alitoboa.
Kwa sasa nasema kwa uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Japan ni hatihati.
Kama kwa miradi hiyo fedha itatoka Japan basi tusahau.
Pengine waziri Ulega hajatonywa kuwa kuna madeni makubwa kampuni za kijapani zinadai kurejeshewa malimbikizo ya makato ya VAT toka TRA.
Madsibhayo yapo kwa muda mrefu, TRA wamedinda kurudisha makato ya VAT.
Za uvunguni naxipata ni kwamba serikali ya Japan inafikitia kukata kabisa hii misaada.