Ni nani huyu Cool 9 Jamani?

Ha ha ha ha ha ha haaaaa......Ukatoka Mbio Kujiokoa ha ha ha ha ha...Ni kweli Huyu Bingwa nilishamuona (RIP) alikuwa Mwamba..... Mtu mwingine akisikia anaona utani Ila sisi vijana wa enzi hizo tunajua nini tunaongea.
Kuna siku pale Iringa Ruaha international alitokea na baiskeli yake sport... Kulikuwa kuna kundi la vijana magangwe walipomuona walitahayari na kutawanyika mbio za kujiokoa! Alisimamisha baiskeli yake akatisika kichwa... Akawaita na kuwaambia hana soo na yeyote kati yao.... Ila kuna mbaya wake anamsaka....
 
Jamaa alikuwa maarufu sana dar na iringa na mbeya na morogoro,yeyote mkongwe dar lazima amjue huyu mtu mana alikuwa maarufu sana pale magomeni,manzese na ubungo na dar kwa ujumla.
Iringa namkumbuka sana miaka ya themanini na tisa tisini hapo nikiwa sekondari alikuwa maarufu kwa mkono pale stendi kuu iringa hakuna asiyejua jina hilobwakati huo cool 9
 
Kiboko msheli lilikuwa kundi la Magomeni enzi hizo, huyu Cool 9 alikuwa Manzese
Pia kulikuwa na gangwe mmoja akijulikana kama KALA MZUVENDI maeneo ya Magomeni makanya, kondoa, kagera nk.
 
Kiboko msheli lilikuwa kundi la Magomeni enzi hizo, huyu Cool 9 alikuwa Manzese
Pia kulikuwa na gangwe mmoja akijulikana kama KALA MZUVENDI maeneo ya Magomeni makanya, kondoa, kagera nk.

kweli enzi hizo ilikuwa nomaa!!
 
bado mzima sana tu, anaendelea kuuza mitumba, utampata maeneo ya kariakoo na mara zingine manzese palepale kwawaulize watakuonehsa anapopatikana.
 
Umenikumbusha mbali sana enzi za wababe wa mkoa,nakumbuka pale Singida miaka hiyo kulikuwa na mtu mmoja anaitwa Ndovu,mtoto wa mtemi Senge,huyu alikuwa mbabe balaa,tuliambia anapiga mkoa mzima,pia alikuwa na uwezo wa kukamata simba mzimamzima!
 
Umenikumbusha mbali sana enzi za wababe wa mkoa,nakumbuka pale Singida miaka hiyo kulikuwa na mtu mmoja anaitwa Ndovu,mtoto wa mtemi Senge,huyu alikuwa mbabe balaa,tuliambia anapiga mkoa mzima,pia alikuwa na uwezo wa kukamata simba mzimamzima!

hahahaa!!! alikuwa mtoto wa mzee MCLYPSY wa ubungo.
 
kweli bongo tumepiga hatua. hayo yalitokea zamani. siku hizi huwezi sikia mambo ya gangwe mob.
cha ajabu, wenzetu Marekani bado wana mambo haya hadi leo. Tena % kubwa ni waafrika.

kwa wale walioishi Kinondoni miaka ya 80, tupeni magangwe wa enzi hizo.
 

Nasikia Dame aliwahi kumshushia kipondo Kalapina? Mchezo ulikuwa hivi, Dame alikuwa amekaa ndani ya gari huku kaachia muziki mkubwa mitaa ya Block 41, Pina kusikia hivyo si akaanza kulifuata lile gari huku anaporomosha matusi ya nguoni, akisema ... ni ( tusi ) gani huyo anatupigia kelele za ki..( tusi ), alipofika kwenye gari akakuta kumbe ni Dame, nasikia akanywea sana na kupiga magoti akiomba msamaha, sijui kitu gani kilitokea baadaye ila nasikia alimpiga makofi pina, pina hakukubali akautenga mkono, mwisho wa siku Dame akampa pina kipigo cha mbwa mwizi
 
Namkumbuka marehemu Cool 9, baunsa wa mabaunsa,
Enzi zile iliaminika kwamba yeye ndo mababe wa Iringa nzima enzi ile,
Japokuwa kulikuwa kuna mtu anaitwa Shetani aliyebarikiwa ambaye bado hakufua dafu kwa Cool 9
Niliishi nae mtaa mmoja Kitanzini Iringa, aliishi nyumba ya pili kutoka kwetu
Nakumbuka mechi ya Lipuli na Simba aliua mbwa mbili za Polisi kwa mpigo
Na polisi wengine walijeruhiwa na kuwahishwa hospitali kama majeruhi
Hivyo baadae polisi walimtumia kusaidia ulinzi wakati wa mechi uwanja wa Samora

Baadae alihamia Mkoa wa Dar es Salaam, pia nilisikia ubabe uliendelea kama kawaida.

Kwa wenye ufahamu zaidi huko Dar watujuze tafadhali.
 
Namkumbuka marehemu Cool 9, baunsa wa mabaunsa,enzi zile iliaminika kwamba yeye ndio mbabe wa Iringa nzima enzi ile,Japokuwa kulikuwa kuna mtu anaitwa shetani aliyebarikiwa ambaye bado hakufua dafu kwa Cool 9.

Niliishi nae mtaa mmoja Kitanzini Iringa, aliishi nyumba ya pili kutoka kwetu,nakumbuka mechi ya Lipuli na Simba aliua mbwa mbili za polisi kwa mpigo na polisi wengine walijeruhiwa na kuwahishwa hospitali kama majeruhi.

Hivyo baadae polisi walimtumia kusaidia ulinzi wakati wa mechi uwanja wa Samora,baadae alihamia mkoa wa Dar es salaam, pia nilisikia ubabe uliendelea kama kawaida.


Kwa wenye ufahamu zaidi huko Dar es salaam watujuze tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…