Ni nani huyu Cool 9 Jamani?

Namkumbuka marehemu Cool 9, baunsa wa mabaunsa,
Enzi zile iliaminika kwamba yeye ndo mababe wa Iringa nzima enzi ile,
Japokuwa kulikuwa kuna mtu anaitwa Shetani aliyebarikiwa ambaye bado hakufua dafu kwa Cool 9
Niliishi nae mtaa mmoja Kitanzini Iringa, aliishi nyumba ya pili kutoka kwetu
Nakumbuka mechi ya Lipuli na Simba aliua mbwa mbili za Polisi kwa mpigo
Na polisi wengine walijeruhiwa na kuwahishwa hospitali kama majeruhi
Hivyo baadae polisi walimtumia kusaidia ulinzi wakati wa mechi uwanja wa Samora

Baadae alihamia Mkoa wa Dar es Salaam, pia nilisikia ubabe uliendelea kama kawaida.

Kwa wenye ufahamu zaidi huko Dar watujuze tafadhali.
Hawa wakina Cool Nine, Hayat, Taulat na Ally Tungu walikuwa WEZI SANA, Nasikia kati yao kuna waliouawa, unaweza kujua nani mzima na nani aliuawa?
 
walifariki wote ndugu yangu, ally tungu aliumwa sana akafa,
Ila Hayat alipigwa risasi kule mlandege walienda kuiba,
ni kweli kaka walikuwa wezi sana ila underground ilikuwa
 
Ndio nimedikia hivyo hivyo pia.......sasa huyo jamaa kwa nini aliwauwa.......?.......na wafanyakazi wao walikuwa wapi.......?
​ndugu yangu alikuwa mbabe sana huyu jamaa, kiasi cha kwamba polisi walikuwa wanamuogopa, ni kama enzi za power mabula kenye vitabu
 
walifariki wote ndugu yangu, ally tungu aliumwa sana akafa,
Ila Hayat alipigwa risasi kule mlandege walienda kuiba,
ni kweli kaka walikuwa wezi sana ila underground ilikuwa
Huyu Ally Tungu,Huenda Wewe na watoto wa Kitanzini nimecheza nao mpira sana pale uwanja Msikitini Madrasa Kitanzini.Unamkumbuka Deo Tagalile? alikuwa mshikaji wangu sana tukisoma wote Gangilonga, alikuwa bingwa wa Kuchora akikuona anakuchola kama ulivyo.
 
​daahh kwa maelezo haya ni 100% kaka, mmi nilikuwa naishi nyumba ya pili baada ya kina Cool 9, pembeni ya kwa mzee Juma Kalinga, Deo Tagalile namkumbuka snaaa, mmi nilikuwa Wilolesi kaka
 
Hii mada ilishajadiliwa sana humu ndani, nami namkumbuka sana huyu jamaa nami nimeishi line polisi pale iringa mjini. Huyu jamaa alikuwa anawatemea sana mate askari polisi na walikuwa hawamfanyi kitu chochote. Shetani aliyebarikiwa alikuwa anaishi makanyagio, huyu jamaa hakuwa mbabe kivile pia kilikuwa kimbaumbau tu kinapenda kuvaa nguo za vitenge. Ubaya wake ilikuwa anauwezo sana wa kupiga mateke hasa sehemu zenye uchochoro yaani huku ukuta na huku ukuta ndiyo anakubamizia maukutani, lakini ukimpleka sehemu za wazi unamsharaza vibao tu mana mwili wake ulikuwa dhaifu sana hakuna pa kupiga ngumi, kiufupi alikuwa kibaka na mkorofi mkorofi ila sio baunsa kama cool 9
 
​akhsante
 
ahhhhhhnyie frelimo kuna jamaa alikuwa anaitwa uncle miki alikuwa anshinda stand kina cool 9 walikuwa wanakaaa.sema hao waburushi walikuwa wezi walipigwa risasi katika godown la RTC mlandege enzi hizo.ila aya mastori niyazamani sana mkuu
 
Back
Top Bottom