Sheffield United FC ya Magomeni Mapipa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,265
SHEFFIELD UNITED FC MAGOMENI MAPIPA

Dar es Salaam ya miaka ya 1960 ulikuwa mji wa vilabu vya mpira vya mitaani vya vijana wadogo wanaoinukia katika mchezo huo.

Vilabu vilikuwapo na viwanja vya kucheza mpira pia vilikuwa vingi sana.

Dar-es-Salaam yote na vitongoji vyake haikuwa na uhaba wa viwanja.

Moja ya vilabu hivi ilikuwa Sheffield United ya Magomeni Mapipa.

Club hii bado ipo hadi leo ingawa wanachama na wachezaji wa miaka hiyo sasa ni watu wazima.

Lakini club ipo ukipita hapo utawakuta wamekaa nje ya club yao wanazungumza.

Leo nimepita Sheffield United usiku muda mfupi baada ya Isha na kama kawaida yao nimewakuta hapo wanachama wa Sheffield FC wamekaa barzani wanazungumza.

Nikawaatolea salamu.
Wakaniitikia lakini nataka kupita nikasikia jina langu linaitwa.

Alikuwa Mheshimiwa Juma Simba Katibu wa Mkoa wa CCM Dar-es-Salaam.

"Mbona unatupita kwa haraka."

Ikawa sasa nimesimama nikaingia ndani ya kundi lile nawapa mikono mmoja mmoja.

"Julio yule kule umemuona?"
Juma Simba ananiambia.

Kiwelu alikuwa kakaa mlangoni unaweza kusema pembeni kizingitini kuingia ndani club anazungumza na simu.

Hapo nje pembeni walikuwa jamaa wengine ndani club patupu watu wanakimbia joto kali la Dar-es-Salaam.

Msimu wa joto Dar-es-Salaam unatesa wakazi wa jiji hili.
Nikawaomba niwapige picha.

Mandhari ya Sheffield United FC wakati wa usiku yanapendeza sana.

Unaona magari yanayopita Morogoro Road na waenda kwa miguu wanaotembea pembeni wake kwa waume.

Sheffield United FC by night.
Inapendeza kwa hakika.

Sheffield United FC ilikuwa club ya rafiki yangu marehemu Mwarami Segumba.

Baba yake Mwarami Mzee Habib Segumba alikuwa Patron wa Sunderland Football Club na akifahamiana na baba yangu toka ujana wao.

Mwarami tulisoma pamoja St. Joseph's Convent School Dar-es-Salaam lakini mimi nilimtangulia.

Tukaja kukutana Bandarini East African Cargo HandlingServices.

Mwarami akicheza mpira mzuri kama beki Sheffield na Hydra timu ya Cargo.

Kila nipitapo hapo kuna kumbukumbu hunijia kwanza ni Mwarami na utanashati wake.

Mwarami alikuwa kijana wa nyakati.

Namkumbuka na marehemu Arthur Mambeta akiishi jirani na hapo.

Mpira wa Arthur Mambeta.
Hii ni habari nyingine kabisa.

Arthur Mambeta alikuwa mmoja wa wachezaji wa timu ya Afrika ya Mashariki iliyocheza na Westbromwich Albion kutoka Uingereza.

Namkumbuka pia na Shomvi na mgahawa wake, "Michuzi Mikali," ambae alikuwa jirani na hapo.

Mgahawa wake ulikuwa maarufu kwa kuku wa kukaanga ambae utakula kwa wali au ugali.

Kilichowapendeza sana wateja wake ilikiwa ile pilipili yake aliyokuwa anawatengenezea kulia kuku.

Hapa Kwa Shomvi palikuwa maarufu kwa wachezaji mpira wa miaka ya 1970.

Ukifika Kwa Shomvi utawaona mastaa wote wa Simba na Yanga wakiwa mahali pamoja.

Shomvi alikuwa mshabiki mkubwa wa Yanga lakini hii haikuwazuia wachezaji wa Simba kumpenda na kuipenda hoteli yake.

Zile zilikuwa nyakati nyingine.
Hakika zile zilikuwa nyakati nyingine.

1704571323019.png

1704571394241.png
1704571444364.png
 
Sparta FC ya Mwananyamala Kwa kopa (Uwanja makaburini)

Kuna ile team kubwaa iliyokuwa inatokea mitaa ya makumbusho (uwanja wa Shule ya msingi Makumbusho)

Hizi team zilikua ni balaaa.

#YNWA
Ipi hiyo? Rungwe iliyokuwa chini ya udhamini wa Ex Director wa Uhamiaji? Or unasema kaka zao na hawa Rungwe,SMaLL TIGER ya pale sokoni Makumbusho?..Hili (Small Tiger) ndio haswa lilikuwa chama langu
Wapi Moshi Mujungu,
Wapi White?
Wapi Tonsa na mdogo wake Kingsray+ Dauda
Hapo Samson Mwamanda kijana mdogo..Njale, Dick West Gwivaha..dah those dayz...
 
Back
Top Bottom