Ni nani anayetaka kuweka maisha yake hatarini kwa sababu ya kuhoji tu?

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Nauliza hili swali hapa, ila nina uhakika hakuna atakaekuwa tayari kujitokeza kunijibu. Hii ni kwa sababu wengi wanatumiwa ili mkono uende kinywani, lkn umafia wa yule anaewatumia wanaujua vizuri sana.

Hapa nazungumzia ule upande wa kondoo kutembea kichwa chini (usihoji chochote kuhusu mwenyekiti) ambapo mtu akijifanya mbuzi kunyanyua kichwa juu (kuhoji kuhusu mwenyekiti) anakumbana na hatari mbele yake.

Makamu mwenyekiti anaeishi Ulaya na familia yake, juzi amejaribu kuwatoa watu uoga wa kuhoji au kukosoa, lkn mpaka sasa watu bado wanaogopa kuanza kukosoa, au kujitokeza kuhoji haswa wakikumbuka yale yaliomtokea Chacha Wangwe, Zito Kabwe na wengine wengi wa aina hiyo.

Sio kwamba wanachama wao hawajui kuwa mwenyekiti wao chama kishamshinda, na juhudi zake za kukijenga chama bila kuwa na makamu wake karibu zimeshindikana. Au sio kwamba wanachama wao hawakumbuki ile kauli ya mwenyekiti wao kuwa ataachia kiti cha uenyekiti mwaka huu wa 2023, baada ya kupigiwa kelele huko nyuma na wenye uchungu na chama ajiuzulu, lahasha.

Wanajua na wanakumbuka sana, lkn nani atakaekuwa tayari kumchalenge Mafia wa chama ili mchalenjiji huyo aweke maisha yake na ya familia yake hatarini?

Wengi wanajiuliza, ikiwa makamu ambae yuko Ulaya anaogopa kumface mwenyekiti, na badala yake anatumia mafumbo ya hapa na pale, je wao ambao wapo karibu na mwenyekiti huyo watatoa wapi ujasiri wa kuhoji na kuuliza siku rasmi ya mwenyekiti kuachia ofisi?
 
Ndio ulivyotumwa na mwenezi wenu?
Acha propanda za kindezi hizo hazina msaada wa moja kwa moja kwenye maisha ya watanzania wengi.
Imagine hapa nilipo lita moja ya Diesel ni 3510.
Vyakula bei juu kila kitu bei juu..
Lita 1 ya Diesel ni 3510, na vyakula bei juu, alaf mwenyekiti anataka kila mkutano azunguke kwa chopa.

Kwanini hiyo hela ya kuzunguka na chopa asiitumie kuwasaidia nyie chawa wake masikini kwa kuwanunulia japo kilo mbili mbili za unga na moja moja ya sukari ili iwe chachu ya watu kukichagua chama chake katika uchaguzi mkuu?
 
Kila kitu bei juu kweli, hadi mwenyekiti kaamua kupandisha bei ya kukodi chopa kutoka 15 m hadi 30 m kwa siku.
 
Kumbuka Nicolaus Copernicas aliweka maisha yake rehani alipopindua imani ya kanisa kuwa "jua ndilo linalozunguka dunia" mpaka sasa "dunia ndio inayozunguka jua". Waliojaribu kuhoji waliuwawa ila yeye kajitoa mhanga ili kupata ukweli.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Ulichoandika kinamantiki sana ila sasa wanachama wengi, au naweza kusema wote ni waoga wanahofia lile litakaloweza kuwakuta endapo watafungua midomo yao kuhoji.

Fikiria mpaka makamu anakumbushia kwamba kuhoja ni jambo la msingi kwa demokrasia yoyote. Akimaanisha kwamba wale watakaohoji mwenyekiti kuendelea kukalia kiti kwa miaka takriban 20 wasishughulikiwe na alie juu ya chama.
 
Kila kitu bei juu kweli, hadi mwenyekiti kaamua kupandisha bei ya kukodi chopa kutoka 15 m hadi 30 m kwa siku.
Hahaha. Bei imepanda hadi katika ukodishaji wa chopa.

Na bado atajiongezea mshahara kwa kisingizio cha gharama ya maisha imepanda 🤣🤣🤣
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Nauliza hili swali hapa, ila nina uhakika hakuna atakaekuwa tayari kujitokeza kunijibu. Hii ni kwa sababu wengi wanatumiwa ili mkono uende kinywani, lkn umafia wa yule anaewatumia wanaujua vizuri sana.

Hapa nazungumzia ule upande wa kondoo kutembea kichwa chini (usihoji chochote kuhusu mwenyekiti) ambapo mtu akijifanya mbuzi kunyanyua kichwa juu (kuhoji kuhusu mwenyekiti) anakumbana na hatari mbele yake.

Makamu mwenyekiti anaeishi Ulaya na familia yake, juzi amejaribu kuwatoa watu uoga wa kuhoji au kukosoa, lkn mpaka sasa watu bado wanaogopa kuanza kukosoa, au kujitokeza kuhoji haswa wakikumbuka yale yaliomtokea Chacha Wangwe, Zito Kabwe na wengine wengi wa aina hiyo.

Sio kwamba wanachama wao hawajui kuwa mwenyekiti wao chama kishamshinda, na juhudi zake za kukijenga chama bila kuwa na makamu wake karibu zimeshindikana. Au sio kwamba wanachama wao hawakumbuki ile kauli ya mwenyekiti wao kuwa ataachia kiti cha uenyekiti mwaka huu wa 2023, baada ya kupigiwa kelele huko nyuma na wenye uchungu na chama ajiuzulu, lahasha.

Wanajua na wanakumbuka sana, lkn nani atakaekuwa tayari kumchalenge Mafia wa chama ili mchalenjiji huyo aweke maisha yake na ya familia yake hatarini?

Wengi wanajiuliza, ikiwa makamu ambae yuko Ulaya anaogopa kumface mwenyekiti, na badala yake anatumia mafumbo ya hapa na pale, je wao ambao wapo karibu na mwenyekiti huyo watatoa wapi ujasiri wa kuhoji na kuuliza siku rasmi ya mwenyekiti kuachia ofisi?
Nini hii,toka bwana nenda zako
 
Nasemaje? Na uzee huo kuning'iniza vichupi ukiuzaa mtaani haifai, miaka 65 kaa nyumbani ule mafao😂
Ndio maana tunapambana ili kumpata mtu sahihi atakaesaidia kuwatoa hawa wanaosababisha wazee tuning'inize hizo chupi mtaani.

Huyu aliepo sasa kazi kubwa ni kuzunguka na chopa kwa milioni 30 hadi 60 kwa siku huku akiwaacha nyie mnaompania mitandaoni mkishindia maji.
 
Lita 1 ya Diesel ni 3510, na vyakula bei juu, alaf mwenyekiti anataka kila mkutano azunguke kwa chopa.

Kwanini hiyo hela ya kuzunguka na chopa asiitumie kuwasaidia nyie chawa wake masikini kwa kuwanunulia japo kilo mbili mbili za unga na moja moja ya sukari ili iwe chachu ya watu kukichagua chama chake katika uchaguzi mkuu?
Kwa taarifa yako muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm umeshaisha, acha hii tarehe aliyosema hata kabla ya mwaka huu. Lakini kusema eti ataweza kumfanyizia atakayehoji hizo ni propaganda za kiduwanzi. Hakuna kiongozi wa chama Cha upinzani anayeweza kuendesha kikundi Cha kimafia kwenye nchi ambayo ni adui wa serekali akaachwa. Kama mliweza kumbambikia kesi, ndio mngemuacha akiwa na vikundi vya uhalifu? Katafute mafala boss.
 
Ndio maana tunapambana ili kumpata mtu sahihi atakaesaidia kuwatoa hawa wanaosababisha wazee tuning'inize hizo chupi mtaani.

Huyu aliepo sasa kazi kubwa ni kuzunguka na chopa kwa milioni 30 hadi 60 kwa siku huku akiwaacha nyie mnaompania mitandaoni mkishindia maji.
Mimi sio team Mbowe wala nani.

Naunga mkono mtu mzalendo.

Mbowe alifanya kazi nzuri lakini kwasasa ame expaya
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Nauliza hili swali hapa, ila nina uhakika hakuna atakaekuwa tayari kujitokeza kunijibu. Hii ni kwa sababu wengi wanatumiwa ili mkono uende kinywani, lkn umafia wa yule anaewatumia wanaujua vizuri sana.

Hapa nazungumzia ule upande wa kondoo kutembea kichwa chini (usihoji chochote kuhusu mwenyekiti) ambapo mtu akijifanya mbuzi kunyanyua kichwa juu (kuhoji kuhusu mwenyekiti) anakumbana na hatari mbele yake.

Makamu mwenyekiti anaeishi Ulaya na familia yake, juzi amejaribu kuwatoa watu uoga wa kuhoji au kukosoa, lkn mpaka sasa watu bado wanaogopa kuanza kukosoa, au kujitokeza kuhoji haswa wakikumbuka yale yaliomtokea Chacha Wangwe, Zito Kabwe na wengine wengi wa aina hiyo.

Sio kwamba wanachama wao hawajui kuwa mwenyekiti wao chama kishamshinda, na juhudi zake za kukijenga chama bila kuwa na makamu wake karibu zimeshindikana. Au sio kwamba wanachama wao hawakumbuki ile kauli ya mwenyekiti wao kuwa ataachia kiti cha uenyekiti mwaka huu wa 2023, baada ya kupigiwa kelele huko nyuma na wenye uchungu na chama ajiuzulu, lahasha.

Wanajua na wanakumbuka sana, lkn nani atakaekuwa tayari kumchalenge Mafia wa chama ili mchalenjiji huyo aweke maisha yake na ya familia yake hatarini?

Wengi wanajiuliza, ikiwa makamu ambae yuko Ulaya anaogopa kumface mwenyekiti, na badala yake anatumia mafumbo ya hapa na pale, je wao ambao wapo karibu na mwenyekiti huyo watatoa wapi ujasiri wa kuhoji na kuuliza siku rasmi ya mwenyekiti kuachia ofisi?
Umenena vyema kabisa,

Mwenyekiti hamtaki PM ila anaogopa kumwambia wazi, inabidi amtumie Mwenezi.😀😀
 
Tafuta cha maana, usilete maneno ya wakosaji jukwaani.
Kila mtu ana uhuru wa kuandika akitakacho. Hivyo kama mimi sikuandika cha maana, haikuzuii wewe kuandika hicho cha maana unachokitaka.

Haya ndio maneno aliyosema makamu mwenyekiti huko Ulaya. Kwamba kuna mtu ana genge lake mitandaoni (nahisi wewe ni mmoja wa wale vijana wa genge lake) hawataki mkuu huyo akosolewe kwa baya au zuri. Yani akikosolewa tu wanachukia na kuanza kumvamia mkosoaji kana kwamba yeye ni Mungu ambae peke yake huwa hakosei.
 
Kwa taarifa yako muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm umeshaisha, acha hii tarehe aliyosema hata kabla ya mwaka huu. Lakini kusema eti ataweza kumfanyizia atakayehoji hizo ni propaganda za kiduwanzi. Hakuna kiongozi wa chama Cha upinzani anayeweza kuendesha kikundi Cha kimafia kwenye nchi ambayo ni adui wa serekali akaachwa. Kama mliweza kumbambikia kesi, ndio mngemuacha akiwa na vikundi vya uhalifu? Katafute mafala boss.
Hahaha... Aisee inashangaza sana kuona mtu unaejifanya mjanja mitandaoni mpaka leo unashindwa kutumia ujanja wako kumsoma Mbowe na kumjua kuwa ni mtu gani, na wa aina gani ndani ya chama 🤣🤣🤣

Kifupi jamaa kawekwa hapo (sio kujiweka mwenyewe au chama kama mnavyoaminishwa) kwa Kazi maalum.

Na hiyo kazi ashaifanya (moja wapo) ni ile ya 2015, na zingine za sirini ambazo sio rahisi mtu ambae hatumii akili iliyohuru kuzijua.

Kesi za kubumba bumba (ili kuwafubazeni) aliyopewa Mbowe, na baada ya kuachiwa tu kukimbilia ikulu fasta siku hiyo hiyo kupewa pole na yule aliemfunga, inamfanya mtu alie huru kimawazo kufikiria mara mbili mbili kama kweli jamaa ni mpinzani thabiti kama Yule aliekumbilia Ulaya au ni jamii ya hawa hawa kina Mrema, Cheo, Lipumba, Zito nk.

Hata swala la kuharibiwa mashamba limezubaza wengi akili, huku mwamba akiwa kalipwa double kupitia njia za siri. Kinachomkuta Mbowe au kile anachokifanya katika chama hadi nyie kupiga makelele kwamba atoke sio cha bahati mbaya, bali ni moja kati ya majukumu yake aliyopewa na wenye mamlaka ili kuhakikisha vyama vyote vipya na vya zamani vitaendelea kuwa vya upinzani tu na kupewa wabunge wawili watatu kama walivyokubaliana katika mapatano yao na CCM.

Mrema alianza vizuri, baada ya muda akajigeuza sultan wa chama ili asijitokeze mwanamageuzi wa kweli wa kuichalenge serikali. Mwisho chama kikaanza kupoteza ushawishi taratibu, na baadae kubaki jina.

Mara akaja Lipumba akaiteka bara na visiwani watu wakamuona ni mwana mageuzi wa kweli, mchumi na mwenye elimu kubwa duniani hadi kupelekea watu kufa na kufungwa katika maandamano na vurugu mbali mbali. Pia kama mwenzake, na yeye akaanzisha mfumo wa kubaki yeye tu uongozini, ili kuhakikisha hatokei mtu mwenye mawazo, na plan ya kweli ya kukitoa chama tawala madarakani. Chama kikaanza kupoteza mvuto na wanachama, wazee wakahamia Chadema, wakamuweka Mbowe, jamaa akaanza kama wenzake pengine yeye akawa zaidi ya hata Lipumba kwa ushawishi. Mambo yakaenda vizuri, ila kama ilivyo ada na yeye akabadili sheria makusudi ili watu kama kina Lisu wanaoonekana ni wapinzani halisi wasije kukalia kiti na kuichalenge serikali. Jamaa kang'ang'ania hadi leo bila kujali boko aliyotoa mwaka 2015 japo wengi tunafahamu kuwa ni moja kati ya majukumu aliyopewa na waliomuweka pale, lkn angeona aibu na kujiuzulu kutokana na kelele za watu kwake.

Anyway watanzania wengi hawana upeo, hivyo acha jamaa atumikie ofisi mbili kwa wakati mmoja. Kama tukiwa hai, hayo ya kutumikia ofisi mbili tutakuja kuyajua katika wasifu wake siku Mungu atapoamua kumchukua kama ilivyokuwa kwa kina Mrema, Membe nk.
 
Umenena vyema kabisa,

Mwenyekiti hamtaki PM ila anaogopa kumwambia wazi, inabidi amtumie Mwenezi.😀😀
Ila mwenezi kaongea na hakuna aliemchacha wagwe.

Ila upande wa pili jamaa yupo Belgium lkn anamuogopa Mafia alie bongo.
Inaonekana mwenyekiti ana sera za Kagame. Ukihoji chochote kuhusu yeye basi anakumaliza huko huko Ulipo. Haijalishi ni Ulaya au Africa 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom