Maryam Malya
Senior Member
- Nov 29, 2021
- 115
- 258
Ameandika Dr. Sisimizi
Bado viongozi wa Chadema wameendelea kuwashangaza wanachama wao na hasa hatua yao ya kusitisha Oparesheni za chama walizokua wakizifanya kwa kutaja sababu ya uongo kuwa walisubiri darasa la 4 wamalize mtihani wa taifa na wakati licha ya wanafunzi kumaliza mtihani, bado chama hicho kimeendelea kukaa kimya.
Kinachowashangaza zaidi hata vikao vya kikatiba vya Kamati Kuu, vimeshindwa kufanyika bila wajumbe wake kuambiwa sababu ya msingi inayoshawishi kikao hicho muhimu cha maamuzi kisifanyike.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati Kuu alijaribu kuhoji kwenye grupu la chama nini sababu haswa ya chama kutofanya shughuli yeyote kwa sasa na ukizingatia ni muda mchache tu umesalia kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025, bahati mbaya Katibu Mkuu John Mnyika alimjibu atulia apunguze Speed
Baada ya malumbano ya hoja ya ukimya wa chama kuibuka kwenye Grupu rasmi la Chama, ikabidi ifanyike igizo maalum la kuwatuliza wanachama na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ambao wengi wao walianza kuhisi kuwepo kwa pande mbili baina ya Tundu Lissu na Mwenyekiti Freeman Mbowe, ndiyo likaanyika igizo Mbowe kuwaita baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na kukutana nao kwenye jumba lake la kifahari Machame ili kuwazuga watanzania na wanachama wao kuwa chama kinaendelea na shughuli zake za kila siku lakini uhalisia hakuna kinachofanyika.
Kiufupi kwa sasa Chadema ni kama imesimama kwa muda, Vikao vya Chama havifanyiki, Mikutano ya hadhara haifanyiki, Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu amekua msafiri, Mwenyekiti Mbowe anajipongeza kwa kumalizia ujenzi wa Nyumba ya Milioni 500.
Swali la msingi ambalo wanajiuliza wanachadema Je Chadema imeshakufa.? au viongozi wamesusa kuiongoza.?