Ni nani aliyeanzisha biashara ya parking Muhimbili?

Nilimsikia yule Professa Janabi akisema wamefanya hivyo kwa sababu magari mengi yaliyokuwa yanapaki pale ni ya watu wasio na wagonjwa..

Yani mtu anaona kuliko akalipie parking Kariakoo au Posta, ni bora akapaki kigari chake pale kisha anashika mwendokasi chap kufanya shughuli zake mjini kisha jioni anakipitia..

Wengine walikuwa wanaenda mbali hata kupaki magari yao pale kwa siku hadi wiki..
 
Huu upuuzi wameanzisha pia pale ST Vicent Mbinga pale Mbinga,sawa muhimbili walifanya hivo kwa sbb wayu walikuwa wanapark then wanaenda makazini na si wagonjwa haya niwaulize nyinyi nani anaacha gari pale akaenda kazini..ST VICENT MBINGA MASISTA HUO PIA NI WIZI MATIBABU GHARAMA KUBWA BADO TULIPIE NA PARKING FEE KWA LILE BANDA LAO KWANZA LIPO MBALI PILI BADO GARI ITAPIGWA JUA ALAFU WAMEWEKA WALINZI WOTE MPAKA KANTEEN MABUBU KAMA HUELEWI LUGHA YA ALAMA MTAISHIA KUKWAZANA TU NA HAKUNA MFASIRI
 
Nilimsikia yule Professa Janabi akisema wamefanya hivyo kwa sababu magari mengi yaliyokuwa yanapaki pale ni ya watu wasio na wagonjwa..

Yani mtu anaona kuliko akalipie parking Kariakoo au Posta, ni bora akapaki kigari chake pale kisha anashika mwendokasi chap kufanya shughuli zake mjini kisha jioni anakipitia..

Wengine walikuwa wanaenda mbali hata kupaki magari yao pale kwa siku hadi wiki..
Akili yake kweli ya kiprofesele
 
Kila Kinachofanyika ..... Kinapata Baraka na Serikali, Wa Kulaumiwa ni Mmoja tu msijifanye hamumjui....!

Tozo za kwenye miamala ya simu....

Mafuta kupanda bei....

Dola hakuna.....

Kizungumkuti cha Bandari.....

Mnadhani ni nani........?

Tusizunguke zunguke...!
 
Ni nani alieanzisha biashara ya parking MUHIMBILI?
Pesa inayopatikana inamnufaisha nani?
Ni haki kumtoza pesa mgonjwa kwa kupaki gari lake tu?
Ni kweli binadamu mtanzania amekosa utu na huruma kiasi Cha kutoza pesa WAGONJWA?
MAMBO ya bi Tozo, maana hata kwenda matibabu ni tarehe kwao.. Loh hii in hi hapana asee... Machichiem mmezidi sasa
 
Nilianzisha mimi, sababu mlikua mnapaki wengi halafu mnaondoka kwenda makazini kwenu, hatujui nani mgonjwa nani janja janja.. Ndo maana nikashusha hili rungu


Basi huna maarifa sahihi ya kukuongoza na hufai kuwepo hapo ulipo.


Getini kuna walinzi? Kazi yao ni nini?

Wagonjwa wana kadi? Kazi za kadi ni nini?

Hizo parking hazina walinzi? Kazi yao ni nini?
 
Jamani mmesahau katika somo la Political economy kila kitu ni bidhaa.Everything is a commodity katika capitalist economy na ndo mana hata gari ikikuzimikia sehemu jamaa wanakuja kukuuliza una ngapi ?? tukusukume !!!!
Hiyo ndio Tanzania mpya !!! kila siku tozo mpya pesa zaenda serekalini lakini hazitoshi iiii
Parking kila sehemu wanachukua pesa lakini wanashindwa kuweka mazingira mazuri ya hio parking ni vuluvulu tu !
HaoTARURA au City Council basi angalau wangechora michoro ya namna parking inavotakiwa iwe magari yapaki namna gani ??? hakuna kitu kama hicho wenyewe ni pesa mbele !!!
Haya ukienda City center kuna wahindi wanalipia parking lakini kwa ajili ya muda ule wa kazi baada ya hapo parking inakuwa free kwa public lakini wao wanadai mpaka muda wa nje ya kazi na wanaweka mgambo uchwara kukataza watu wasipaki.Hili nalo City council na TARURA hawana habari nalo !!!!!
 
Back
Top Bottom