A
Anonymous
Guest
Kuna jambo la naona wengi tunalalamika ila hakuna linapofika.
Miezi kadhaa iliyopita Hospitali ya Muhimbili ilianzisha tozo za parking ambazo ilikuwa ukikaa chini ya nusu saa ni bure ila ukizidisha utalipa Shilingi 1,000 kama utakaa chini ya saa tatu.
Kisha wakasema ikiongezeka hapo kila baada ya saa mbili (Dakika 120) utalipia Shilingi 1,000 nyingine. Japo nayo ilikuwa ni ghali kiasi ila walau tulikuwa tunaweza kuimudu kwa kiwango flani.
Sasa hivi wamebadilisha tozo na imekuwa ukikaa chini ya nusu saa ni bure ila ukizidi kila saa moja unalipia Shillingi 1000.
Just imagine kuna huduma gani unaweza kwenda kuifata Muhimbili na ukatumia dakika 20?
Ukienda na mgonjwa wako pale iwe anaumwa au clinic jiandae kupoteza zaidi ya saa tano na pengine inaweza kiwa siku nzima.
Sasa hii inakuwaje, Hospitali ya Serikali tena ya Taifa inatoza wagonjwa wake parking fees zilizo ghali hivi? Hatukatai kuweka parking charges ila hizi zilizobadilishwa sasa ni kali, uwezekano wa kuacha Shilingi 12,000 kila siku ukienda kupata huduma ni mkubwa.
Soma pia Wanaopaki magari Hospitali ya Muhimbili kuanza kulipia