Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,403
- 40,331
Aliyefiwa na mke au mume; ni baada ya muda gani ndio anaruhusiwa kuoa/kuolewa?
Maisha ya ndoa huwa ni matamu sana, hasa kwa wale wachache waliobahatisha kupata mtu sahihi.
Inafikia kipindi, wanakuwa na mfanano fulani; unaweza kuwa wa sura, kuongea, au tabia.
Inapotokea mmoja wapo anafariki, inakuwa ni pigo kubwa sana kwa aliyebaki. Inaweza kuchukua muda mrefu kuwa katika hali ya majonzi, huku akikumbukia namna walivyoishi na mwenzake.
Mnavyojua tena; kuwa na majonzi muda wote inakuwa haifai; kwa sababu aliyeondoka ameshaondoka, na hawezi kurudi tena; na maisha yanatakiwa yaendelee.
Ndipo pale, hitaji la kuziba pengo hutokea.
Sasa wakuu, nauliza; ni muda gani ambao ni sahihi, kwa mfiwa kuoa/kuolewa na mtu mwingine?