Ni Mtazamo tu!

Hahahahahah classics bana, mie nshapatwa sitafuti nilikuwa nanogesha mjadala 2 huoni watu wamechangia sred?

Poa Ciello, mimi napenda physical attack. Natumaini hukupatikana kupitia internet.
 
Kwan internet zililetwa za nini?

Kwa upande wako sio mbaya sana, lakini inaweza kuashiria mumewe kukosa ujasiri wa kuapproach wanawake. Au ile watu kufanya kama mzaha halafu ikawapelekea kwenye ndoa.
 
Acha tu tena ndoa za mzaha tamu weye, haya mambo ya kujifanya serious ka unaamua kesi za epa inaumiza ndoa nyingi lol
Kwa upande wako sio mbaya sana, lakini inaweza kuashiria mumewe kukosa ujasiri wa kuapproach wanawake. Au ile watu kufanya kama mzaha halafu ikawapelekea kwenye ndoa.
 

mkuu tafadhali usiishushie hadhi jf... kwa jf ni kama sehemu zozote zile ambazo watu hukutana na wakavutiana mwisho wa siku wakapenda na wakatengeneza familia
ngoja nikupe mfano mdogo kwa kutumia mfano wako.. umepropose watu wakutane.. basi katika kukutana mimi na wewe tukabadilishana contact kwa ajili ya business flan tofauti na mahusiano... na wakati huo mimu au wewe hatukuwa na interest hata kidogo isipokuwa kibiashara tu. in the long run ukavutiwa na mimi na ukanitaka nije kuwa mama watoto wako... je utazuia hisia zako kisa tulifahamiana via jf????
 

Mkuu charminglady huo mfano wako unawezekana. Usidhani mie nasema watu wa jf hawafai kiasi kwamba huwezi kupata mke au mme. Kwani jf ina watu ambao tunaishi nao na kufanya nao kazi, tena wengine labda ni ndugu, marafiki nk, kama jf ingekuwa haifai mimi nisingekuwepo humu.

Ninachoongelea ni ile kuanza kudate mtu kwa kuangalia jina na avatar. Ninaamini perfect partner pamoja na kuangalia vigezo vingine ni yule mtu unayemkubali kwanza machoni! Sasa kupanga kukutana na mtu usiyemjua hata sura yake ni kufanya mchezo wa kubahatisha kwenye maisha, which is seriously bad. Ikiwa hautamridhika, maana yake utaendelea na mchezo huu wa kudate mpaka utakapopata perfect partner (probability ya kupata anayekufaa ni ndogo, sanasana utachoka ukasema liwalo na liwe ukabeba mtu yeyote), au kitakachotokea ni kujengeana mazingira ya kujifanya mnaendana ili muoane, matokeo yake ndio zile ndoa za misimu. Tukikutana kwa dili zingine halafu nikaona unanifaa nakuvuta tu mkuu.
 

Mfano, mtu anaweza tu kusoma jina lako charminglady akapata hisia kwamba wewe ni charming, kumbe hata kucharm watu huwezi.
 
charminglady Ciello anakuambia ndoa za mzaha ni tamu, ina maana yeye amekuwa kwenye ndoa mara kadhaa, lah?
 
Sasa sisi wenye sura nyangau hatuoi wala kuolewa?

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums

Mkuu sura nyang'au simaanishi sura nzuri au mbaya, namaanisha sura ambayo haikuvutii wewe, ambayo inaweza kuwa na mvuto sana kwa mwingine. Kwa hiyo usihofu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…