Ni mkakati gani Azam tv umetumia kuteka soko?

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,418
9,209
Safari zangu mikoani nimeshangaa wingi wa madishi ya Azam tv kila ni endepo. Siyo siri tena Azam TV imeteka soko la TV ya malipo. Je ni mbinu ipi Azam umetumia kuteka soko hadi kuwaangusha DSTV, Zuku na kadhalika?
 
Ni pamoja na hayo matangazo na watu siku zote huwa wanaangali ni kitu gani kinatangazwa sana.
 
Safari zangu mikoani nimeshangaa wingi wa madishi ya Azam tv kila ni endepo. Siyo siri tena Azam tv imeteka soko la tv ya malipo. Je ni mbinu ipi Azam umetumia kuteka soko hadi kuwaungusha dstv zuku na kadhalika?
Mkuu nilikwenda dodoma nikabaki nashangaa, kila nyumba hata za nyasi juu kuna dishi ya Azam jamaa wako vizuri, tukatae tukubali!
 
Mimi nilienda lushoto Tanga sikuona madish mengine zaidi ya Azam Tv. Mi nadhani kuonesha mpira wa VPL hasa kuonesha michezo inayohusisha simba na yanga imechangia sana kununuliwa kwa hivi ving'amuzi. Kingine ni ubora wao wa picha yaani HD
 
Kinachowafanya Azam tv wauze kwa wingi Madishi yao ni kuoneshwa Live kwa Ligi kuu ya Tanzania -VPL, Taarifa zao za Habari pamoja na matukio mengine wanayoonesha Live kama vile Bunge na Uchaguzi Mkuu uliopita. Siku Azam wakichukua Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) Basi Multichoice na jamaa zake watafungasha virago.
 
Ubunifu katika soko,na hasa kujua mahitaji sahihi ya Watanzania.Kuonyesha ligi ya VODACOM kumeipaisha Azam Tv.Waingie mikataba mizuri na timu za ligi kuu kama shukrani kwa kuwini soka.
 
Kinachowafanya Azam tv wauze kwa wingi Madishi yao ni kuoneshwa Live kwa Ligi kuu ya Tanzania -VPL, Taarifa zao za Habari pamoja na matukio mengine wanayoonesha Live kama vile Bunge na Uchaguzi Mkuu uliopita. Siku Azam wakichukua Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) Basi Multichoice na jamaa zake watafungasha virago.
Siku Azam wataonyesha EPL watateka soko zima la Afrika Mashariki. Azam tv Kenya inayo ushindani mkubwa na zuku na bamba tv (free for life)
 
simba na yanga, kama huamini subiri mkataba wao uishe wachukue deal startimes, watafugia nyuki hivyo ving'amuz
 
Azam wasipo kuwa makini, basi naona Boss wa Info amejipanga kuwa piku akishirikiana na kampuni moja kutoka Mauritius - Mr.Mfuruki kichwa sana yule atakuja kubadiri soko hili beyond expectations za Wateja.

Tatizo la Azam TV si wabunifu, ni kweli wana vifaa vingi vya kisasa na studio nzuri - beyond that wanaendeleza mambo kama mashirika ya UMMA ya wacha liende - watu wabunifu wangepata facilities kama zile specifically studios wangezifanyia wonders! Siwasemi vibaya lakini tuwe wakweli hapa ubunifu hawana kabisa, nguvu zao zote zinaelekezwa zaidi kwenye masuala ya mipira ya hapa na Ulaya, sio kwamba nataka kuwaribia biashara - Nina uzoefu wa muda mrefu wa masuala haya nimeishi kwa nchi za wenzetu kwa miaka mingi sio kwamba nasema mambo ya kubuni tu, wanapaswa kujirekebisha.
 
Back
Top Bottom