Mtoboasiri.Kwa kawaida huwa sitoi maoni yangu kwa kila anachokisema huyu "msomi dr" Bana kwa kuwa sijawahi kumsikia akitoa maoni yeyote yanayo-justify hata kidogo kuwa nae ni msomi. Lakini hii ya leo imenikumbusha thread ya mjumbe mmoja hapa ukumbini aliehoji elimu yetu na jinsi watu wanavyopanda vyeo nchini kwetu.
Kusema ukweli lazima kuna uwalakini na mfumo mzima wa maisha yetu kwa ujumla (elimu, namna ya kupata viongozi, kupandisha watu vyeo and all that), otherwise iweje Bana akawa na PhD halafu akawa anatoa utumbo kila siku? Sitarajii mtu awe anatoa maoni yanayokubalika na wote siku zote, lakini kutoa utumbo tu kila siku???
I can't even begin to understand this situation of ours!!!!!!
Dr bana badilika ndugu, Hivi wewe Udaktari wako ni wa nini, unatumia macho na masikio gani? Nani amekupa kazi ya kutetea serikali wewe? unalipwa shillingi ngapi? je Una ndungu maskini huko vijijini? Tafakari na chukua hatua
ni aibu kwa elimu ya tanzania, ni aibu kwa chuo kikuu kuwa na msomi of this kind. inawezekana watanzania kwa mifumo yetu ya elimu maswala yasiyo na madesa ndiyo majibu yetu. labda kuna kosa la mwandishi maana haya ni maneno mtu anaongea na mwandishi anachagua ya kuandika. kazi ya bunge ni nini?kama siyo kusimamia serikali
Huyu Mr. Benson Bana ataendelea kuishi kwa kujipendekeza kwa viongozi mpaka lini? Eti anajiita Doctor, doctor gani ambaye hawezi hata kutambua kuwa kama hutaki kuwajibika unawajibishwa? Ananitia kichefuchefu huyu doctor uchwara!!!!Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.
Source:Uhuru Jumatano
Huyu DR. BANA anasumbuliwa na matatizo ya kutokujua na kuamini kuwa MAFISADI hawatakiwi ktk nchi hii. Ila huyu Mzee ni KILAZA kweliiii; Kama SIO wananchi (pamoja na wananchi ambao ni viongozi wa kisiasa wazalendo) kuwabana viongozi wezi na mafisadi ni NANI HUYO ATAKAYEWEZA KUWASHUGHULIKIA HAO WEZI WALIOKUBUHU....?? BANA be serious, otherwise unaendelea kuleta tafrani mioyoni mwetu.Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali. Source:Uhuru Jumatano
Kama kuna wasomi nchi hii nimewafuta kwenye data base yangu hata wakizungumza chochote sioni umuhimu wake kwangu na kwa taifa wakwanza ni huyu dr Bana, usomi wake utabaki kwenye vyeti lakini kiutendaji huyo ni zero hana maana kwenye taifa letu, sijui anatafauta uwaziri (vyeo vya kupewa) au?Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.
Source:Uhuru Jumatano
Mzee huyu anafaidika sana na UFISADI na kama namuonea aje akanushe hapa. Ni Dr. Ambaye uwezo wake wa kufikiri umechuja.
Amekula sana hela ya mafisadi kupitia REDET na leo anaona serikali ikianguka naye atachunguzwa. Only that.
View attachment 52635
Jamani huyu Dr Banna alipewa huu udokta kama kiongozi wa magamba au aliukeshea kabisa huo udokta wake....nway tutafika tu!
huyu Bana huenda ni "msomi" lakini siyo "mtaalamu" wa mambo ya siasa. Hajui kuwa chimbuko la demokrasi ni kushinikizana; shinikizo la wengi ndilo linalotekelezwa. Inawezekana anazungumzia siasa za Tanzania ambapo hakuna demokrasia, lakini katika nchi zenye demokrasi mambo ya siasa yanakwenda kwa kushikizana kila siku. Mdiyo maana kwa Marekani kuna interest groups zinazoshinikiza wabunge na serikali kuhusu sera wanazotaka wao hadi wanafanikiwa kuzipata.