Ni makosa makubwa kushinikiza Serikali - Dk Benson Bana

Hii ndio cream iliyoko UDSM inayopotosha Serikali chini ya kivuli cha usomi huku wakifanyia majaribio doctrate zao za sheria, siasa na utawala.Mwenendo mzima wa madudu mengi ya serikali ni hyo cream ya watu aina ya Bana.Hatimae ya yote wako pembeni wanacheka kwa kuona malumbano ya umma na watawala huku chanzo kikiwa ni wao kwa kuwa washauri wa majaribio [Analysis and Synthesis] za michezo michafu ya kisomi ndani ya Taifa dogo lisilo na uchumi imara.

Ni sawa kwa Taifa kama Marekani wasomi kucheza michezo ya siasa,sheria na utawala pasipo kuangamiza Taifa lao.Na ndio maana mtu mmoja anaweza kuanzisha [Draft] vita na Taifa zima likaenda likapigana na bado Taifa likaendelea kuwepo na likaimalika au kuathirika kidogo sana.Lakini kweli wasomi wetu mchezo wao ulipo lifikisha Taifa kwa kujalibu kuvunja kitu kizima kuwa vipande vipande kisha waone kitaunganika vipi wakati wanajua uchumi wake bado ni tegemezi hiyo ni dhambi na hukumu yake ni risasi ya ubongo,kwa kuwa uhai haufanyiwi majaribio.

Kuna kundi fulani la wasomi pale chuo kikuu ndio maengineer wa michezo mingi michafu ndani ya Taifa hili,chini ya migongo ya kuwa washauri wa wanasiasa wetu,wasio chuja yale wanayoambiwa.Na upumbavu wa wasomi wetu ambao wanakosa busara,zingatia tetesi kwa sie ambao hatukuwepo miaka hiyo kuwa yule msomi maalufu Tanzania zama hizo marehemu Tuntemeke Sanga,aliludi nyumbani toka masomoni marekani BBT Mwalimu Julius K Nyerere akamuita ikulu,akaulizwa na Mwalimu apewe kazi gani kulijenga Taifa lake,Mzee yule nasikia alimwambia Mwl kuwa hakuna nafasi nyinngine zaidi ya huo Urais wake.

Napata picha babu yule wa kizanaki ile sura yake ilibadilika ghafla kifuatacho ITV,alipelekwa Makete akakalia kuti kavu.Na ukweli Mwl alilijua hili tatizo la wasomi la kutaka kuwa watawala kwa niaba ya wakoloni.Yani ile nafasi ya wakoloni wasomi wameidaka na kuifanya wao kuwa ndio watawala kwa niaba ya wakoloni na si viongozi wa kuonyesha njia kwa umma na kujenga Taifa kwa kuwa wazarendo kwa kuvaa ule moyo wa Mwl kuwa utu na ubinadamu kuona asiyeweza nae anawezeshwa kuweza.

Kuna katabaka fulani ka wasomi pale UDSM,ndio Mastrategist na engeneers wa michakato wa pande zote mbili zinazoasimiana lakini wote wanachezeshwa na kundi moja akija huyu anapewa hiki,akija yule anapewa hiki,wanatengeneza tag of war kisha wanafanya observational na kuibuka na kusudio lao wanalotaka.

Tupende Tusipende wasomi wengi hasa walio ngazi za taaluma wanaamini Taifa uongozwa na kuamuliwa na mambo mengi na kikundi cha watu wachache,kwa mujibu wa elimu yao.Kuna wasomi mpaka leo wanaamini kuwa Ibrahim Lincoln hakuwa Rais bora USA na Sir Winston Churchill alikuwa Waziri Mkuu bora Uingereza,lakini hawashangai Profesa Mwenzao Uganda alipewa Urais akashinda ndani ya miezi tisa.

Wao usomi kwao ni vyeti vinasema nini.....una +B au +A ngapi na umesoma chuo gani duniani Havard,Oxford au Yale.Na sio usomi wa Mwalimu kuishi kwa kuanzisha jambo jipya na sio kubishana theory za nani zikifutwa zinaleta utawala bora.Matokeo kuendesha nchi kwa kukalili theory za marehemu kwenye makarabrsha lundo ya vitabu vya dunia kuliko kuishi kwa ukweli halisi wa dunia tunayoishi sasa ndani ya Taifa husika.Hao ndio wakina Bana!!!
 
Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.

Source:Uhuru Jumatano
Kuna haja ya kupima wasomi wa aina ya DK. Bana, je yeye anaona ni halali kwa Serikali kuwaibia wananchi wake km inavyofanya hii serikali dokozi ya CCM???Mbona hatujamsikia kukemea na kukerwa na hii serikali ya wadokozi???Kwa mawazo/fikra zake lipi ni kosa kubwa la kukera kati ya haya mawili??Serikali kukumbatia wezi, mafisadi na wahujumu uchumi au wananchi kupitia wabunge wao kuitaka serikali iwachukulie hatua wezi na waujumu uchumi??? Naanza kupata wasiwasi na PHD za aina hii ya huyu Bana. He is not using his brain critically kuanalyse issues. Kama hadi amepata PHD hajajua kati ya wananchi na serikali nani yupo sahihi hadi sasa katika issue hii. Kweli PHD yake inanipa wasiwasi sana, its either ameamua kujifanya mpumbavu na kufkiria kwa kutumia tumbo au ni insane.

Tulitegemea wasomi wa taifa hili wawe washauri wa wanasiasa ili kuitoa nchi hapa tulipo, instead anaongea utumbo. Na hii imekuwa ni kawaida ya huyu Dr. Watu kama nyinyi kule South Africa walikuwa wanachomwa wao, nyumba zao na familia zao. Huwezi mtu mzima kuongea mambo yakipumbavu na kudhani unasifiwa. Nchi ipo katika msiba wa serikali kuibia wananchi wake, wananchi wanataka serikali iwajibike wewe unatokea kusikojulikana umeshiba viazi unakuja kusema sio sahihi, je kama wao wenyewe hawataki kutoka tunafanyaje??? Je ni sahihi serikali kuibia wananchi na kuwa badhirifu pmj na kukumbatia wizi na mfumo dokozi?????Unataka tukae kimya ili kesho waingie mikataba yakipumbavu, watie nchi hasara zaidi na wafanye ufisadi kwa kasi zaidi???Nimekudharau sana na PHD yako. Naona sasa hizi PHD hata wehu wanazipata, inawezekana hii PHD yako ni ya vyuo vya kata. Wewe ungekuwa mwalimu wangu tungegombana mana nadhani kwa thinking hii ningekuchallenge sana hadi ungeishia kunikamata, mana ndo kawaida yenu wanazuoni wenye ufinyu wa mawazo km wako. Unatutia aibu sana wanazuoni wenzako.Unafanya taifa lipoteze imani na wanazuoni kwa kudhania kuwa wote wana mawazo ya njaa kama yako.
 
dr gani hajui hata namna ya kuiwajibisha serikali
anazalisha wanafunzi vilaza pale chuo
kwa hivo anataka kutuambia serikali haiwezi kuwajibishwa au kushinikizwa?
akapimwe akili pale mirembe au muhimbili hafai kufundisha
 
Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.

Source:Uhuru Jumatano

Kweli ni kosa kuishinikiza serikali, lakini makosa makubwa zaidi, serikali kuwaibia watu wake. Ni kama mzazi/mlezi kumbaka mwanae.


Zaidi ya yote ni makosa makubwa makubwa zaidi kuwa na daktari/wasomi mwenye akili fupi kuliko ufupi wenyewe. Hawa ndo chachu ya kuua uchumi wa nchi, Ni heri angekufa yeye kanumba akabaki kuendeleza sanaa na usanii.
 
jamani usomi mwingine unatia shaka, dkt mzima kweli una mawazo hayo lakini ni uhuru wa kutoa maoni nami naheshimu maoni yako. nafasi na elimu ulioyo nayo kwa kweli mimi naona kama vile havisaidii jamii "elimu ni sharti iisaidie jamii kupambana na mazingira" Aristotle


ni mtazamo wangu tu wadau!
 
Benson Bana itakuwaje ukerwe na jambo ambalo ni utaratibu wa kawaida katika mambo ya siasa? Ikiwa watu wanaona wazi kuna mawaziri wenye tatizo na raisi hachukui hatua ungependekeza wafanyeje? Wavumilie tu hadi raisi atakapomaliza muda wake?

Tatizo lako Benson ni kuwa hii kuandikwa kila siku magazetini inakufanya ujione umekuwa authority wa mambo ya siasa na uongozi nchini. Huna lolote kwani point zako nyingine ni sawa tu na point za KCC yeyote yule ambaye angepewa nafasi ya kuandikwa magazetini. Mara nyingine nahisi KCC angeongea vitu vya maana zaidi kwa kuwa yeye yuko in touch zaidi na reality on the ground kuliko wewe uliye detached katika kiota chako hapo mlimani na nyumbani mbali na watu wa kawaida (common man on the street).

Kama nilivyomweleza January Makamba, ikiwa mtu amependekeza suluhisho kwa tatizo linaloikabili jamii, kama hutakubaliana na suluhisho lililopendekezwa una wajibu wa kijamii kuliboresha suluhisho lililopendekezwa, au kutoa suluhisho mbadala lililo bora hata zaidi. La sivyo kaa kimya.

Wewe Benson si lazima kila jambo linalotokea nchini utoe maoni yako. Mara nyingine kuwa na akili kunaonekana kwa kukaa kimya. Hapa ulitakiwa ukae kimya.
 
"A government of the people, by the people, and for the people".

Sasa serikali ishinikizwe na nani kama siyo wananchi wake walioipigia kura? Njaa na kujipendekeza kwingine kuna sikitisha kwa sababu mtu anajivua usomi na kuvaa ushabiki.
 
Mzee huyu anafaidika sana na UFISADI na kama namuonea aje akanushe hapa. Ni Dr. Ambaye uwezo wake wa kufikiri umechuja.

Amekula sana hela ya mafisadi kupitia REDET na leo anaona serikali ikianguka naye atachunguzwa. Only that.

View attachment 52635


Mkuu umenena vyema kabisa. Ni jambo lisilotarajiwa kwa Mbwa kumng'ata mwenye Mbwa!
 
Sidhani kama kuna muda wa kujisumbua kubishana na huyu Dr
Wakati wote hata kukiw ana mjadala wowote unaoihusu nchi hii yeye anakuwa upande wa kuitetea serikali
hajawahi hata wakati mmoja kuonyesha kuwa serikali inakosea
Hata kama kuna udhalimu na ufisadi wa kutisha yeye amekuwa upande wa serikali kutuonyesha kuwa haina makosa
Always huwa anatetea hata kisichofaa kutetewa
 
Hapa kuna vitu mnachanganya, Dr.Bana siyo msomi kwa sabab msomi anakuwa analytical, ameclaim tuu! Msiwadhalilishe wasom
 
Mtu anaye claim principles fulani, either being wrong or otherwise siyo msomi a learned person Bana siyo wa crbr hiyo!
 
  • Thanks
Reactions: DSN
Dr. Banaaaaa. Mwenye kosa ni huyo kiazi aliyekwenda kumhoji. Kwani watu wenye mawazo ya maana wamekwisha humu nchini? Tukichukua nchi hawa ndiyo wa kwanza kuwashughulikia.
 
Hasara kwa taifa, Kama mwalimu yuko hivi anaowafundisha watakuwaje?

Mtu msomi wa jinsi yake anatakiwa awe mkweli, asilete ushabiki. Serikali inashinikizwa na wananchi kwani wananchi ndio mabosi viongozi ni vibarua wetu Wanaofanya kazi kwa mkataba wa miaka mitano mitano. Tumewapa ajira, wamejisahau na kutufanya sisi vibarua.

Tulikaa kimya wakaona kuwa sisi ni mafala, sasa tumeamka tunataka vibarua tuliowaajiri waache wizi na kiranja mkuu wao na msaidizi wake (PM) awawajibishe.

Kosa lipo wapi ????
 
Back
Top Bottom