Ni makosa makubwa kushinikiza Serikali - Dk Benson Bana

Hawa ndoi yanao ishauri CCM na kujenga hisia za woga kwa umma.Mtu kama huyu ni wa kumpuuza na kmbeza. by the way makada wa CCM pale political science dept UDSM wapo kibao! SHAME ON HIM!:shetani:

ni kweli kabisa usemalo hata fund inayoendesha REDET huwa wanapewa na magamba shame on them
dr.bana
dr kilian
prof mukandala
na yule aliyeacha kufundisha akaenda kuwa mshauri wa raisi hakuna kitu hata sijui anamshauri nini?

labda bana naye ameshaambiwa atakwenda kuwa mshauri wa raisi
 
msomi kutoka chuo kikuu cha dsm dk benson bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.dk bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.dk bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.

Source:uhuru jumatano
......hii ndio shida ya kuishi kwa kujipendekeza au kwa fikra zisizosahii za mwenyekiti, bana anatarajia kwa kujipendekeza aonwe siku zijazo kwa taarifa yake mtindo anaotumia ni wa kizamani kweli kweli.
 
Anavizia ulaji toka kwa JK, huyu naye hata haelewiki upepo unavyovuma ndivyo anavyokwenda, lakini basi ndiyo wasomi wetu wa TZ
 
Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.

Source:Uhuru Jumatano

Mkuu kuna baadhi ya degree huwa zina 'expire'. Hata hivyo kwenda shule si lazima kuna maana ya kuelimika. Kama serikali ikiwa imeingia madarakani kwa njia za ujanja ujanja, itaendeshwa hivyo hivyo hadi pale itakaposhinikizwa kuendeshwa kwa staili inayotakiwa.

Dk Bana anajua anachokifanya inawezekana anatafuta kitu, lakini naamini kuwa anajua ukweli uko wapi, na anajua kwanini anasema uongo.
 
ni kweli kabisa usemalo hata fund inayoendesha REDET huwa wanapewa na magamba shame on them
dr.bana
dr kilian
prof mukandala
na yule aliyeacha kufundisha akaenda kuwa mshauri wa raisi hakuna kitu hata sijui anamshauri nini?

labda bana naye ameshaambiwa atakwenda kuwa mshauri wa raisi
Kama Bana akiwa mshauri wa rais tutarajie nn kwa fikra zake hizi mgando? Hv tutafikiri kwa kutumia matumbo na kuacha kutumia vichwa hadi lini? Hovyo kweli kweli.
 
Huyu mzee shule yake ni ya kweli maana PHD yake ni ya Manchester UK.Nimejaribu kusoma gazeti lenyewe la Uhuru alichoeleza ni tofauti na kichwa cha habari .Huu ni uhuni tu umetumiwa na Mhariri wa gazeti la magamba

Hebu tupe kwa ufupi ukweli alisemaje?? ukiacha upambe wa mwandishi wa hizi habari.
 
Acha yawe makosa lakini pia elewa kwamba ni makosa pia kwa viongozi kutumia vibaya madaraka yao. Tanzania bila ufisadi inawezekana na njia pekee ni kwa kuing'oa Magamba baaaaas!
 
Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.

Source:Uhuru Jumatano
Serikali ilishayumba tayari kwa wimbi la ufisadi na utumiaji mbaya wa madaraka, wanachofanya wabunge ni kuiweka sawa.
 
Rais wa 32 wa Marekani, Frank Delano Roosevelt, alipofuatwa na wapiga kura wake wakimtaka afanye matakwa yao, aliwajibu "nakubaliana nanyi, nishinikizeni nifanye mnavyotaka".

Roosevelt hakuogopa kushinikizwa, alitaka kushinikizwa. Wengine wanaweza kuuliza kwa nini alitaka kushinikizwa wakati yeye kama rais ana nguvu ya kufanya bila kushinikizwa? Siasa.

Siasa za nchi yake ziligawanya nchi kati ya progressives na conservatives. Ili kuonyesha msukumo unatoka kwa wananchi, rais Roosevelt hata baada ya kuwa na nguvu za kiraisi kufanya mipango yake ya New Deal, alitaka kuwaonyesha watu wote kwamba ana support ya wananchi.

Huyo ni kiongozi. Hasemi "ni makosa makubwa kushinikiza serikali" anasema "ni wajibu wa kila mwananchi kuishinikiza serikali"

Wakati wenzetu huko marais kama Roosevelt waliwaasa wafuasi wao kushinikiza serikali, sie mpaka leo tuna "maprofesa" - watu wanaotakiwa kuwa wsomi na kujifunza kutoka historia- ambao mpaka leo wanatuletea mtazamo wa kuiona serikali ni kama ya enzi za Ching, inatawala kwa "mandate of heaven". Haishinikiziki wala kukosoleka.

Ndio wasomi wetu hao!
 
hakuna cha dokta wala mganga hapo,sana sana huyo ni mchumia tumbo ambaye hataki kujionyesha hadharani......
 
Sijafikia level ya udaktari kama yeye lakini nachelea kupinga uelewa wake kuhusu hili.
Katika nchi ya kidemokrasia wananchi ndio decision makers namaanisha ndio wanaoamua serikali ifanye nini na kama imeshindwa wanachukua uamuzi wa kuiwajibisha kulingana na katiba....wananchi bungeni ni wabunge na wameona serikali imeshindwa,serikali bungeni ni mawaziri na mkuu wao ni waziri mkuu...sasa wananchi hao kwa kufuata katiba wanataka kuiwajibisha serikali inayowatumikia kwa kushindwa,eti unasema wanakosea....ni haki yao kikatiba na udhaifu wao umeanikwa hadharani...sasa dk.Bana hajui kama wananchi ndio wenye mamlaka yaani decision makers....arejee ibara ya nane ya katiba yetu.
Kwa maelezo haya tuu inatosha kukuita wewe ni dr wa ukweli umekosa vyeti tuu bac!!!!!!!
 
Gazeti mojawapo limemnukuu Dr Benson Bana kwamba kuiendesha serikali kwa mashinikizo ni hatari. Nafikiri kweli hii ni hatari, hatari tena hatari sana!. Siku moja nikiwa Mwanza kituo kimoja cha daladala, ikapigwa kelele kuashiria kulikuwa na mwizi ameiba. Watu wakakusanyika wakazomea mwizi na kumpiga. Baada ya muda kidogo yule kijana akafariki wakati polisi ndiyo wamefika kufuatilia kelele. Baada ya muda kidogo tena akatokea ndugu wa yule kijana marehemu na kuanza kulia na kutamka kwamba ndugu yake sio mwizi na alikuwa amemtuma maeneo ya hapo kumsubiria mama yao ambaye angeshuka kutoka vijijini. Ikapatikana hadithi ya kweli kwamba yule kijana alikuwa aibiwe na alipopiga kelele za mwizi wale wezi wakamgeuzia yeye na wakatoweka.

Hivyobasi, mashinikizo yanayotolewa dhidi ya Waziri Mkuu ama Mawaziri sio kwamba kwa asilimira mia yana nia njema ndani yake. Kuna wanaopiga kelele, wanatengeneza taarifa za kuimplicate watu kwenye kashfa ili wao waonekani safi katika jamii kumbe la!. Kuna kelele za ukweli ndiyo lakini pia umakini unatakiwa kwa sababu kelele zingine pia sio za ukweli. Nchi wachafu ni wengi, tena wengi sana tu, sio wapinzani wala watawala, wapiga kelele wala wapigiwa kelele, the problem is rooted from our mind set - from family levels. Ndugu wakiwa na mbunge asiye na mali wanamdharau, akiiba akawa na mali anaonekana mjanja.

Siku nyingi tu nilishagundua kwamba bunge linakuwa linatamani kuvuka mipaka yake na kuingia katika kufanya majukumu ya Serikali. Mfano nina matukio kadhaa yanayodhihirisha hili. Moja EL alipojiuzulu bado bunge liliona alipaswa kuwajibishwa zaidi na kupelekwa hadi mahakamani na huko mahakamani, wakae wenyewe (wabunge) ili wamhukumu na adhabu ambao ni mpaka wao waridhike ndiyo waamini kwamba amewajibika ama amewajibishwa. Mbili, Serikali ilipotoa taarifa za utekekelezaji wa scandal ya Richmond kuna baadhi ya mambo wabunge hawakuridhika, wakataka wao ndiyo wangeifanyia Serikali mfano adhabu ya karipio kutoka kwa Raisi (mamlaka ya nidhamu) kwa Hosea ilionekana ndogo na wabunge wakatamani wao ndiyo wangekuwa mamlaka ya nidhamu (tatizo la sheria husika labda). Tatu, njoo issue ya Jairo, Bunge bado linataka lichukue mamlaka zaidi, kwani linatamani kuchukua mamlaka ya Serikali kuhakikisha linadraft hadi barua ya adhabu ya ya Jairo. Nne, hapa juzi pia tumeshuhudia wabunge pamoja na hoja nzuri walizokuwa nazo, walizidi ukomo wao wa kutaka Raisi awaadhibu Mawaziri kwa taarifa za kisiasa (no natura justice at all - sijui hawakujifunza kwa EL!). Eti wakaazimia kupiga kura ya kukosa imani kwa PM (hapa Zitto kajivumisha kweli, wengine hawajui tu mkakati wa Zitto!)

Sitetei kuwa Mawaziri hawakosei, wanakosea sana, kama wabunge wenyewe wanavyokosea, lakini mashinikizo yanayotoka, in a long run, madhara yake sio mazuri sana kama watu wanavyoweza kufikiri kiurahisi. Hekima au busara inatakiwa itumike zaidi, kuliko upepo wa kisiasa ambao kwa asilimia kubwa naona hausaidii hata kidogo kutatua matatizo sugu ya nchi hii ambayo ni kama imelaaniwa kwani kila ninayemwangalia usoni namwona yupo corrupted.
 
Wana bodi huwa inaniwia vigumu kuwatofautisha uwezo wao wa kufikiria Kati ya dr bana, proffesor majimarefu ,dr Matusi (lusinde) na huyu Dr anayesubiriwa ili baraza la mawaziri libadilishwe ambaye ameboronga sanaaaaaa kwenye hiyo taasisi kubwa ulimwenguni Mzee wa Afro (minywele mingi ) Migiro
 
Msomi kutoka chuo kikuu cha DSM Dk Benson Bana amesema ni makosa makubwa serikali kuongozwa kwa mashinikizo.Dk Bana alikuwa akirejea shinikizo la kuwawajibisha mawaziri mafisadi na wazembe lililotolewa na bunge katika kikao kilichoisha jumatatu wiki hii.Dk Bana ameonyesha kukerwa na kitendo hicho kwani ni kutaka kuyumbisha serikali.

Source:Uhuru Jumatano

Wasomi ndo janga la taifa la Tanzania, wanatusaliti watanzania mil karibu 50 kwa kuilinda system. Wanajipendekeza kwa serikali, hawawezi kusema ukweli, waoga. ispokuwa wachache sana kama akina Dr KITILA, BIG up.
 
Kuna mambo ya msingi umesema ambayo nakubaliana na wewe ila nina swali. Kwa kuwa unakubali kuna tatizo, lakini lisitatuliwe kwa mashinikizo, unataka nini kifanyike kukomesha tatizo?
Hizi kelele na upepo, kama unavyoona wewe, ni hatua ya kwanza. Kuna hatua za kuendeleza tunapoelekea 2015, mchakato wa katiba na hata chaguzi kuu baada ya 2015. Lakini kwa sasa Zitto na wenzake wapige kelele za mwizi, tena wapige sana. Tofauti na mfano wako wa kijana asiye mwizi kuuawa, Zitto na wenzake wamepigia wezi kabisa, lakini wamepigia kelele wezi wachache tu! Kuna wezi wengi sana, ambao bado zamu yao haijafika! Kubwa la majambazi bado hawajalifikia, lakini hawajachelewa, MAPAMBANO YANAENDELEA. Harakati hizi zinapaswa kuungwa mkono na wote, siyo wapinzani tu, ila wote wenye mapenzi mema na Tanzania.

Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
 
Hivi shinikizo ni nini? Linatatizo gani? Jee kama kunautendaji mbovu shinikizo hilo haliitajiki? hasa kwa viongozi ving'ang'anizi?
 
Bana ni sehemu ya kundi la wasomi wachumia tumbo, mara zote hasemi ukweli hasa akijua kuwa ukweli huu utakuwa mwiba kwa serikali; nafikiri anavizia ateuliwe kuwa vice chancellor mlimani
 
Back
Top Bottom