Ni maandamano au ni mapinduzi?

Ni maandamano au ni mapinduzi?

nitashangaa kama polisi wakitumia silaha za moto , maana waandamanaji siku hiyo tutakuwa tumebeba BIBLIA NA QURAN takatifu...... Tukiomba Mungu atuletee mapinduzi ya viwanda,kifikra,kiroho na kiakili Tanzania
Hahahaha umepewa onyo umeanza kulainisha lugha, eti kitabu kitakatifu. Kitabu hicho hicho kinakuasa utiii mamlaka iliyowekwa kihalali
 
Haki ya Nani nina hamu ya kuona kwa macho nini kitatokea siku hizo. Jeshi letu limesikika kwa kudhibiti machafuko nchi za wenzetu. sasa ni zamu ya nyumbani
Nakukumbusha tu kule Misri raia walikuwa wakishangilia juu ya vifaru au hukuwaona?
 
Kumbe hata hamjui!
Hata ww si haujui bas na hii ndo teknik ya 26/4. Si Polisi wala JW anaejua nini kinaenda kutokea. Hawajui wajipangaje (kulinda raia/kudhibiti), hata mahali yatakapofanyika na yataratibiwa kwa namna gan kila kitu hakijulikan. Ila yapo.
 
Napata ukakasi kama kweli hio siku watanzania wataandaman?kama tu waliweza kukimbia panya road ,,,,anyway nilipokua mdogo nilisema wakubwa wanafaid kweli kuwa na wanawke wazuri,magari mazur ,nyumba nzuri ,nilitaman sana niwe mkubwa,sasa hatimae nimekuwa mkubwa, nyie andamaneni tu kwakwel mi natimiza ndoto yangu ya utoton aisee
 
Wanaongozwa na Mnyonya koni. Mapinduzi kote duniani hudhibitiwa kwa silaha za moto. Na ndivyo itakavyotokea siku hiyo wakithubutu

Hizo ni dalili za uoga kutaka kumdhibiti mtu asiye na silaha kwa silaha za moto... kama wao wanataka kuwadhibiti aka kushindana nao nguvu waje kavu kavu halafu hapo ndipo tutakapowapima uwezo wao na ukakamavu..
 
Hahahahahahaaaaaaa. Hapo mmeeleweka. Siku hiyo wanaume wa Kazi watakuwa na zana zote halali. subirini mkufilie mbali wakati huyo anayewahamasisha ananyonya koni huko majuu
Kwa kuwa wewe utaishi milele?
 
Me najua maandamano kikatiba yanaruhusiwa ila mapinduzi hapana.
Yanaruhusiwa kwa kufuata sheria na kanuni zake. Sasa sina uhakika kama hivyo vitu vimefutwa na hawa wanaotaka kuandamana.
 
So long mmetoa muda wa kutosha na sisi tukajipanga, haki ya nani siku hiyo mtatafuta pa kukimbilia. stock zote za silaha zilizotapakaa nchi nzima siku hiyo zitakuwa nje nje. Na kwa vile tupo na maandalizi ya Siku ya Muungano, tutatest kila silaha ili tuone kama zipo kisawasawa. Maana nyingine zimekaa muda mrefu
Ni Mange huyu huyu anafanya jeshi litoe stock yote je mkitishiwa na Al shababu itakuwaje.
 
Nitaandamana,nimechoka kusikia watu wanavyokufa ovyo.
 
Maandamano ya kuiponya nchi from incompetent leadership of just one man! Ni kama yale ya Tunisia, Misri n.k. Siyo yale ya Libya na Syria!

NB: Mwambie rais kuwa japo haya maandamano hayana dalili ya kufanikiwa kumwondoa madarakani ila yanapanda kitu kipya kabisa akilini mwa raia. Mange hawezi ila labda kuna wanaoweza ambao labda wamemtanguliza Mange. Wanaweza kuwa wanafaanya majaribio.Mwambie abadilishe staili ya kuendesha nchi, aache chuki dhidi ya wanasiasa wenye mawazo tofauti, achukue hatua pale watu wanavyoona wananyanyaswa na dola.

Mwambie rais coercive/dictorial leaderships sio aina pekee za leadership. Halafu ajisafishe kuhusu jeshi la Rwanda maana raia hatujui ni kweli yanayosemwa au sio kweli maana kama ni kweli huo ni uhaini

Mwambie watanzania wote yeye ni rais wao,aache mara moja kupendelea Mwanza na Geita hata kama hataki kura za sehemu zingine.
 
Nipo home naangalia mkanda wa mapinduzi ya Libya na lraq ...hiyo military propaganda hayiwezi kuwatoa ....embu tufanye kimyaa kimyaa...jipangeni na umma ijipange ifike siku tupige friendly mechi simpo........Relax Eliza!!
 
Yanaruhusiwa kwa kufuata sheria na kanuni zake. Sasa sina uhakika kama hivyo vitu vimefutwa na hawa wanaotaka kuandamana.
Sheria inasema kutoa taarifa 48hrs before leo bado miezi miwili wasiwasi wa nini si msubiri?
 
Mapinduzi yatafanyika kwa kutumia Bible na Masahaf!!! Hahaaaa
 
Nipo shule ndugu tena huku nchi za watu. Nimeibuka kwenye hii ishu kutokana na jinsi inavyotaraji kuzaa vilema watarajiwa na marehemu watarajiwa. Ni vema hawa wanaotaraji kufanya hivyo tukawapa somo la kutosha. Maana wengine wanaendeshwa na akili za Wanyonya Koni huko ng'ambo
Nchi za watu??,mtu unapigwa na vumbi hapo lumumba eti nchi za watu,sema baada magu kusitisha buku 7 na uteuzi ulizira...
 

Uwezo wa kijeshi wa IDI AMIN kipindi kile nani alikudanganya ulikuwa mkubwa kuliko Tanzania, IDI AMIN alikuwa na weak weapons kumbuka aliwekewa vikwazo na silaha alizipata kwa njia haramu, AMINI alikuwa na jeshi lililokuwa halina Umoja, Tanzania ilipata support kutoka sehemu nyingi za dunia ikiwa Cuba,China na tayari nchi ilikuwa moja.

Uwezo wa kijeshi wa Misri ni mara 1000 ya uwezo wa kijeshi wa Tanzania toka zama hizo mpaka leo, Jeshi la Misri liko extra miles kuanzia teknolojia, wingi wavifaa, idadi ya askari active na reserve, uzoefu wa kivita maana wamepigana vita nyingi kubwa namaanisha fighting na sio peace keeping, pia jeshi lao muda wote liko standby aka kwenye tensio kulingana maeneo waliyopo na mipaka yao kuanzia kupambana na wapalestina wanovusha silaha kwenda Gaza, Suez Canal pale, tension na Israeli + islamic millitants.

Pamoja ya nguvu yooote hiyo chini ya mkono wa chuma wa Mubarakk lakini Jeshi la Misri lilishindwa na nguvu ya umma, kifupi hakuna jeshi lolote linaloweza kushindana na nguvu ya umma bali tuombe Mungu aepushie mbali hii dhahma kifupi waandamanaji wasiwe na umoja lakini umoja ukiwepo baina yao nchi nzima hali itakuwa mbaya na ukweli hakuna jeshi litakaloweza kuwadhibiti..

cc : Lu-ma-ga
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Nimefuatilia baadhi ya mitandao ya kijamii hususan Instagram na Telegram kuhusu haya makundi ya watu wanaotamani kuuangusha utawala wa Rais Magufuli. Kwa kiswahili wanasema kuwa hayo ni maandamano ya Amani. Ila kwa Kiingereza wanatamka Tanzania Revolution.

Kwa uelewa wangu, Maandamano tafsiri yake kwa Kiingereza ni Demonstration au Protests. Na Revolution maana yake kwa kiswahili ni Mapinduzi. Kwa uelewa wangu finyu, busara huweza kutumika katika kudeal na maandamano ikiwa ni pamoja na matumizi kiduchu ya nguvu. Ila Mapinduzi hapo lazima ujidhatiti kukabiliana nayo. Hapo silaha za moto na nzito hutumika na ni haki ya vyombo vya dola kutumia nguvu zote ili kulinda himaya dhidi ya maadui wa ndani na nje.

Kingine, Maandamano hudhibitiwa na Jeshi la Polisi. Ila Mapinduzi hapo wanaume wa kazi, JWTZ huingia mzigoni. Hapo silaha zinazotumika ni za moto tu. Hawajafundishwa kutumia TEAR GAS hao.

Kwa hiyo, ni vema wale wanaotamani kuona utawala wa Rais Magufuli unaangushwa wakatafakari upya ni nini hasa wanataka kufanya siku hiyo na nini madhara yake. Ni vema wakaweka wazi je wanataka kuandamana ama wanataka kufanya mapinduzi? Maandamano YES ila MAPINDUZI ni BIG NO. Watu wasije kufumuliwa vichwa wakifanya mapinduzi then wakaanza kulalamika kuwa jeshi la polisi na JWTZ wametumia nguvu ya ziada.
Zanzibar waliandamana au walipindua?
 
Moja ya kitu ulichosahau labda nikukumbushe MISRI ni moja ya nchi yenye jeshi imara kabisa Africa na vifaa vya kisasa kuanzia ndege za kivita za kutosha, mamia ya vifaru na gari za delaya, manowari vita na meli za kivita... lakini mwisho wa siku watu walijiselfie na vifaru barabarani..

Hiyo movie haiwezi fanikiwa sio kwa sababu ya jeshi imara la Tanzania lahasha bali kwa sababu ya uoga na ujinga wa watanzania, Hakuna jeshi lenye nguvu kuliko umma, nahuhakikishia hapo Dar es salaam waandamane watu 10000 tu JWTZ haitaweza kuwazuia kamwe, tuombe Mungu na tuache kauli za kejeli haya mambo ni hatari sana Lizaboni...
Ndoto za nchi za wenzenu endeleeni kuziota tu.....Not in Tanzania..mtuachie kisiwa chetu cha amani.
 
Back
Top Bottom