Sidhani kama kutakuwa na maandamano. Lakini ni vema kuonyesha uwezo wa walinzi wetu.Wabongo bwana, kweli CCM imewafifisha akili! Sasa kwa nini serikali itumie nguvu zote hizi wakati tumeaminishwa kuwa serikali ya awamu hii inapendwa sana kuliko awamu zilizotangulia. Na je hao 'wachache' wasioipenda wakiachwa waandamane na kuongozwa na poilisi ili waeleze wanachotaka kueleza kuna ubaya au hasara gani? Mimi ningekuwa ninamshauri mtukufu asiyejaribiwa, ningesema atoe amri kwa poiliccm kuhakikisha wanatoa ulinzi wa kutosha kwa waandamanaji po pote pale maandamano yanapopangwa kufanyika ili tusikie wanataka serikali ifanye nini. Sijui kwa nini CCm inaogopa mikutano ya hadhara na maandamano?
Ni sawa na kuishi kwenye eneo lisilo na uhalifu. Sio busara kuacha mlango wazi.
Weka kufuli kubwa mlangoni hivyo kwamba hata kama kungekuwa na mtu anaeshawishika ataipita tu nyumba yako kwa kuliona lile kufuli.


