olame ndame
Member
- Mar 11, 2016
- 29
- 17
Mimi nikisoma BIBLIA naona manabii na mitume walifanya kazi ya kuwaonya na kuwashauri wafalme na watawala.Wachungaji kazi yao kulilisha ,kulitunza na kuliangalia kundi la Mungu lililo chini yao.Kwa kuwa wakati huu hakuna tena manabii na mitume(kwa mujibu wa Biblia);ni kazi ya wachungaji na wainjilisti kuwashauri na kuwaonya watawala pale wanapoonekana kwenda tofauti na maadili na miiko ya uongozi na kuvunja katiba.Chakushangaza wachungazi(maaskofu) ndio wamekuwa mawakala wa wanasiasa jambo ambalo linawafanya wapiteze sifa ya kuwa mdomo wa Mungu.Ni aibu kwa wakili wa Mungu kujidharau kiasi chakujifanya dalali wa siasa.Si vibaya kiongozu wa siasa kutembelea nyumba yoyote ya ibada,naye ji kondoo kama wengine,alishwe,afundishwe na kuelekezwa maadili mema.Kazi ya kila siku ni kuwaombea.(1timotheo2:1-3;