Ni lini Rais Magufuli amerasimisha kazi za Halmashauri kwenda Serikali Kuu?

rais aache upendeleo ktk mkoa wa dar!!

1. vitanda vilipelekwa muhimbili tu... wakati zahanati nazo zinahitaji vitanda.

2. barabara ya mandela - ubungo kibangu.

3. barabara ya mwenge - moroco

kwa kuwa rais umekuwa ukipanga matumizi ww mwenyewe.... utukumbuke na sisi wa huku vijijini....[/QQUOTE
Mkuu amia dar
 
Familia ya Hifikepunye ingefahamu kiwango chako cha kutukuka cha ukilaza ulichonacho,wangekushitaki kwa kuchafua heshima ya jina lao.

Hahahaha!!! Mdogo wake Jesca anaitwa Joel ndo wewe Joel Pombe?
 
wanasemaga abuse of power, naona baba jesca anaelekea huko. kwa kuna hatari ya kuitumbukiza nchi kwenye mgogoro ya upendeleo wa dini, itamlazimu aende na upande wa pili atoe zawadi, ameingilia kazi ya akina mstahiki mayor Jacob
 
Kwa nini asilipe fadhila kama amefanyiwa wema? Ina maana wewe ukifanyiwa fadhila unadhani ni haki yako?
 
Wachina wanakuja kujenga kiwanda cha simu....kibangu wanapelekewa barabara! Wao wanalia na maji pia......mpango ukoje? Kwa sasa watanzania hatuna shida ya kiwanda cha simu! Heri wangejenga kiwanda cha madawa ya binadamu ili wasiagize nje wanunue hapa hapa!
Hata mimi nadhan kiwanda cha simu, cha magari siyo tija kuu kwa Watanzania leo hii. Viwnda ambavyo vinapswa kupewa kipaumbele ni vile vya kuprocess raw material ili kuongeza thamani ya bidhaa zetu. Na kiukweli viwanda vya aina hiyo husaidia kuleta ajira za moja kwa moja. Hivyo mkazo uwe ni viwanda vya kuchakata mazao, samaki, madini na bidhaa zingine. Wachina ni wazuri ila wamekaa kiuchuuzi zaidi kuliko uhalisia!
 
Kwani ulitaka Rais afanye nini sisi tunataka maendeleo basi mengine hatutaki porojo zenu za kitoto.
 
Acha rais afanye kazi hizo manispaa zilishashindwa kujenga barabara. Naomba unitajie barabara moja ya maana ambayo manispaa wamejenga zaidi ya usanii tu wanapaka rami baada ya miezi mitatu mashimo yanaanza. Kwanza ningekuwa mimi ningewanyan'ganya zote maana miaka 50 hawana barabara hata moja ya kujivunia.
Hizo system mnazozitetea zimefeli kwa miaka 50 acha rais aingilie kati achukue maamuzi zijengwe barabara za maana
Je unao ushahidi wa Bajeti kwa barabara ya Halmshauri na zile za Tanroads? Hivi unajua juna mambo ni double standard hasa inapokuja suala la Mhandisi wa Halmshauri na yule wa Tanroads? Unafaham kuwa ni ukweli usiopingika bajeti ya barabara ya Tanroads na zile z a Halmshauri tofauti ni kubwa mno. Tuchukulie barabara yoyote ya kawaida ya kiwangoa cha Kifusi. Rate ya gharama kwa kiwango cha Changarawe Halmshauri huwa ni ndogo huku Tanroads huwa ni kubwa!
 
1) Kafukuza vilaza UDOM
2) Kamchana Jk hadharani
3) Kazoa uchafu ferry kwa mikono yake Independent day
4) Kaapa kupambana na Waagizaji wa sukari now
5) Kaenda kuahidi ujenzi wa Barabara kanisani
6) No Bunge Live
7) Kipeperushi cha Mawio kimefutwa ( sio kufungiwa)
8) Kaamuru Polisi kuiba tairi za Magari kwa wenye trafick case za BRT.
9) Kapiga Marufuku kusema fedha hazitoshi Wizarani.
10) ......
Hayo ni Trailer picha kamili linakuja baada ya kupita Bajeti 2016/17
Duuh..huogopi Sheria za mitandao?
 
"... tunataka Rais wa Maamuzi magumu...",
"..Huyu Rais ndio mrithi sahihi wa Hayati Baba wa Taifa"
Rais mstaafu Kikwete anakumbukwa zaid na waliokuwa wapinzani wake kuliko Rafiki zake.
Hilo ndio lilikuwa kosa kubwa la mwalimu hakuweka taasisi za kuwadhibiti viongozi, hasa kwa sababu alijiamini kuwa ni muadilifu, akasahau kuwa siku moja ataondoka,na Mh magufuli Anafanya kosa lilelile kama anaweza kuchukua pesa bila utaratibu kwa nia njema, wapo watakaochukua, kwa nia mbaya.
 
Kuna sheria inayomkataza rais kujenga barabara iliyo kwenye manispaa?
Upo sahihi kabisa mkuu. Hakuna haja ya kuwa na manispaa wala hawa wabunge na mawaziri hawafanyi kazi yoyote. Kazi zote anaziweza mkuu wa kaya. Akimaliza hiyo ya huko aje na huku kitunda ajionee. Hapa kazi tu
 
Hivi ile ziara ya mkuu ilikuwa rasmi au ilkuwa kwenda kupata upako? Na kama ni upako habari ya barabara inatoka wapi? Kwa kweli makanisa ya kiroho mna bahati. Nadhani next week ataenda kwa mama lwakatare, Geo Davy, Kakobe etc etc. Na bila shaka ahadi zitatolewa tu.
 
Haya maamuzi ya rais kusema chochote au ahadi huwa hakina maana ni kuwafurahishs wananchi tuuuuu...hebu fikiria kila rais alivyoahidi vimetekelezwa?
Wabunge wa ccm wamekomaa na ahadi ya rais badala yakupanga......
Mpaka Leo meli ya mv bukoba hamna
 
Back
Top Bottom