G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,704
- 36,456
Leo nimemsikia Rais Magufuli akitoa ahadi ya kutengeneza kipande cha barabara konachotoka maeneo ya river side kwenda kwa mzee wa upako. Kimsingi kabisa hiyo ni kazi ya manispaa ya Kinondoni.
Lakini leo nimemsikia Zitto akisema kuwa Rais Magufuli amekwapua mapato ya majiji kwenda serikali kuu. Huu hasa ndiyo udhaifu tena mkubwa.
Kama rais wa nchi atahangaika na vitu vidogo dogo kama hivyo ni lini atalielewa taifa? Eti nimekuja ili nijionee! Kweli?
Kimsingi kwa sisi tunaomwelewa mzee wa upako, rais Magufuli kaenda kulipa fadhila kwa aliyotendewa (kwenye mabano) Sisi tunataka rais aelewe ni kipi anapaswa kufanya kama rais! Bajeti ya kujenga barabara ya Kibangu ambayo anasema fedha zipo ilipitishwa na nani? (Kupoka madaraka ya mihimili kunaendelea) Hili jambo baadhi yetu linatukera kwelikweli!