Ni lini Rais Magufuli amerasimisha kazi za Halmashauri kwenda Serikali Kuu?

rais aache upendeleo ktk mkoa wa dar!!

1. vitanda vilipelekwa muhimbili tu... wakati zahanati nazo zinahitaji vitanda.

2. barabara ya mandela - ubungo kibangu.

3. barabara ya mwenge - moroco

kwa kuwa rais umekuwa ukipanga matumizi ww mwenyewe.... utukumbuke na sisi wa huku vijijini....
 
Hapana.

Ukisema cha muhimu barabara inajengwa Tanzania buka kufuata utaratibu kesho utahalalisha hela zichukukiwe Tanzania na kukimbizwa Switzerland.

Kuna sababu utaratibubumewekwa.

Rais hawezibkuamua tu kichwani jwake barabara ipi itengenezwe.

Hizo fedha anazitoa kwenye vote ipi? Atawalazimisha halmashauri wajenge au atazitoa serikali kuu? Wapi haswa?!

Yale yale ya kuvuruga utaratibu na wadanganyika wanaona ni sawa tu
 
Kama rais mwenyewe ndio anafanya allocation ya pesa bunge lina kazi gani?

Waache waendelee kula posho tu hasa wabunge wa ukawa maana hawajielewi mida mingine wanataka tamu ikija tamu wanag'ang'ana kuitaka chungu, kwa maana yake wao nisawa na wafukuza upepo, MUACHENI RAIS AIJENGE NCHI.
 
Mheshimiwa alijiandaa kuongoza nchi kwa miezi mitatu tu achape raba.
Sasa amechanganya cocktail ya grisi,maziwa,wine,bia,kiroba,panadol,perfume... Yani akiiangalia haielewielewi, hajui aweke nini tena.
Siku za mwanzo alikuwa anaongea kwa nadra alionekana ana busara sana, sasa anaropokaropoka anaonekana mfalme juha.
 
Anataka kila sehemu aonekane yeye ndio sterling na kujizolea misifa, kumbe anaharibu kila sehemu.
Alitakiwa apewe wizara tu, mambo mengi kwa wakati mmoja yote yatashindikana.
Bora hata mzee wa msoga aliyekuwa anakabidhi mambo kwa wafuasi na kwenda kutalii.
Kila siku tz inatumbuiwa majipu mwisho wake itaoza mana majipu yatakuwa yamearibu kila mahali nakushindwa hujui uanze kutibu lipi
 
Leo nimemsikia Rais Magufuli akitoa ahadi ya kutengeneza kipande cha barabara konachotoka maeneo ya river side kwenda kwa mzee wa upako. Kimsingi kabisa hiyo ni kazi ya manispaa ya Kinondoni.

Lakini leo nimemsikia Zitto akisema kuwa Rais Magufuli amekwapua mapato ya majiji kwenda serikali kuu. Huu hasa ndiyo udhaifu tena mkubwa.

Kama rais wa nchi atahangaika na vitu vidogo dogo kama hivyo ni lini atalielewa taifa? Eti nimekuja ili nijionee! Kweli?

Kimsingi kwa sisi tunaomwelewa mzee wa upako, rais Magufuli kaenda kulipa fadhila kwa aliyotendewa (kwenye mabano) Sisi tunataka rais aelewe ni kipi anapaswa kufanya kama rais! Bajeti ya kujenga barabara ya Kibangu ambayo anasema fedha zipo ilipitishwa na nani? (Kupoka madaraka ya mihimili kunaendelea) Hili jambo baadhi yetu linatukera kwelikweli!
amesema itaanza kutengenezwa mara moja budget ya ujenzi ikipita..na siyo kwamba kajihidhinishia budget yake ya kujenga hiyo barabata,tuache kupotosha.
 
Cha muhimu barabara inajengwa TanZania, fedha inachukuliwa wapi haijalishi kuna wengi sana wanaochukuwa fedha zetu na kuzipeleka kwenye akaunti zao Uswisi hivyo ni bora mara milioni 10 kwa Raisi Magufuli anayechukuwa fedha na kuziwekeza kuwasaidia Wananchi kwani hiyo br. siyo ya Raisi Magufuli na familia yake bali ni ya WatanZania wote na hiyo ndiyo tofauti ya Magufuli na fisadi Lowasa, Yeye (fisadi Lowasa) alihamisha fedha zetu na kuzipeleka Ulaya kununua majumba london na kwingineko lkn Raisi Magufuli anachukuwa fedha zetu na kuwekeza kwenye Mundo mbinu kwa ajili yetu!

Hivyo hilo swali lako ulipaswa umuulize fisadi Lowasa ni nani alimpa Mamlaka ya kuchukuwa fedha zetu na kupeleka London kumnunulia nyumba takataka zake!
We kunguni inaonekana unamahaba sana na Lowasa.
 
Barbarossa MKUU acha tabia chafu ya kusema MTU una ushahidi gani kuwa Lowassa amefanya hivyo usemavyo? Usipende kujifanya unajua sana sasa hivi kuna sheria ya mitandaoni usije ukajikuta keko au segerea Na hao unaotaka wakusifu watakucheka
 
Acha rais afanye kazi hizo manispaa zilishashindwa kujenga barabara. Naomba unitajie barabara moja ya maana ambayo manispaa wamejenga zaidi ya usanii tu wanapaka rami baada ya miezi mitatu mashimo yanaanza. Kwanza ningekuwa mimi ningewanyan'ganya zote maana miaka 50 hawana barabara hata moja ya kujivunia.
Hizo system mnazozitetea zimefeli kwa miaka 50 acha rais aingilie kati achukue maamuzi zijengwe barabara za maana
 
Leo nimemsikia Rais Magufuli akitoa ahadi ya kutengeneza kipande cha barabara konachotoka maeneo ya river side kwenda kwa mzee wa upako. Kimsingi kabisa hiyo ni kazi ya manispaa ya Kinondoni.

Lakini leo nimemsikia Zitto akisema kuwa Rais Magufuli amekwapua mapato ya majiji kwenda serikali kuu. Huu hasa ndiyo udhaifu tena mkubwa.

Kama rais wa nchi atahangaika na vitu vidogo dogo kama hivyo ni lini atalielewa taifa? Eti nimekuja ili nijionee! Kweli?

Kimsingi kwa sisi tunaomwelewa mzee wa upako, rais Magufuli kaenda kulipa fadhila kwa aliyotendewa (kwenye mabano) Sisi tunataka rais aelewe ni kipi anapaswa kufanya kama rais! Bajeti ya kujenga barabara ya Kibangu ambayo anasema fedha zipo ilipitishwa na nani? (Kupoka madaraka ya mihimili kunaendelea) Hili jambo baadhi yetu linatukera kwelikweli!
Huyo ni JPM kwa rangi zake halisi. Ni majanga na ni asili yake.
 
Cha muhimu barabara inajengwa TanZania, fedha inachukuliwa wapi haijalishi kuna wengi sana wanaochukuwa fedha zetu na kuzipeleka kwenye akaunti zao Uswisi hivyo ni bora mara milioni 10 kwa Raisi Magufuli anayechukuwa fedha na kuziwekeza kuwasaidia Wananchi kwani hiyo br. siyo ya Raisi Magufuli na familia yake bali ni ya WatanZania wote na hiyo ndiyo tofauti ya Magufuli na fisadi Lowasa, Yeye (fisadi Lowasa) alihamisha fedha zetu na kuzipeleka Ulaya kununua majumba london na kwingineko lkn Raisi Magufuli anachukuwa fedha zetu na kuwekeza kwenye Mundo mbinu kwa ajili yetu!

Hivyo hilo swali lako ulipaswa umuulize fisadi Lowasa ni nani alimpa Mamlaka ya kuchukuwa fedha zetu na kupeleka London kumnunulia nyumba takataka zake!
Mkuu haijalishi hata kama ni Rais inatakiwa aheshimu vyombo vilivyopo vya kutoa maamuzi vilivyo chini ya hayo maeneo kama manispaa ya kinondoni au kama ni ya kitaifa basi aachie bunge na si kuingilia kila kitu inaonesha kakosa kazi ya kufanya yeye kama Rais haiwezekani kabarabara hakazidi hata kilometa 1afu anakuja kuitolea ufafanuzi wa jinsi ya kufanya na huku wasaidizi wake waliopo chini yake wapo
 
Jamani lumumba mshaurini baba jeska mara moja moja awe anasafiri kwenda nchi za mbali kubadili mawazo na kuona wenzake wanafanyaje asidhani yeye ndio kila kitu kwenye nchi.
 
Wachina wanakuja kujenga kiwanda cha simu....kibangu wanapelekewa barabara! Wao wanalia na maji pia......mpango ukoje? Kwa sasa watanzania hatuna shida ya kiwanda cha simu! Heri wangejenga kiwanda cha madawa ya binadamu ili wasiagize nje wanunue hapa hapa!

Jiangalie Utabomoka ndugu Yangu!

Ataekwamisha Tanzania ya Viwanda nitambomoa-Baba J,
 
Hapana.

Ukisema cha muhimu barabara inajengwa Tanzania buka kufuata utaratibu kesho utahalalisha hela zichukukiwe Tanzania na kukimbizwa Switzerland.

Kuna sababu utaratibubumewekwa.

Rais hawezibkuamua tu kichwani jwake barabara ipi itengenezwe.

Wewe unafahamu utaratibu wa TanZania ulivyo? Unafahamu Raisi wa JMTZ ana Mamlaka kiasi gani Kikatiba? Au unaweza kuniambia ni kifungu gani cha Katiba Raisi wa JMTZ alichovunja?
Raisi wa Tanzania yuko juu ya yote hapa TZ, kwanza hata Mkuu wa Wilaya tu ana huwo uwezo wa kuamrisha br. ijengwe mahali fulani bila ya kuwa amevunja Katiba yoyote ile, sasa kama Mkuu wa Wilaya anaweza kufanya hivyo iweje Raisi ashindwe?

Mnachoshindwa kuelewa ni kwamba Raisi Magufuli anatumia madaraka yake kama Raisi kikatiba na hakuna analofanya ambalo ni kinyume na Katiba inavyomruhusu kama Raisi wa JMTZ!

Mimi nimeshashudia maraisi waliopita kwa mfano, Raisi anakwenda Hospitalini kumtembelea mgonjwa akifika hapo Raisi anasema huyu mgonjwa akatibiwe nje ya nchi, halafu Raisi anaondoka sasa waliobaki huku nyuma ni lazima wampeleke mgonjwa nje ya nchi fedha mtaipata wapi hiyo ni shauri yenu hivyo kwa kifupi kwa TanZania kauli ya Raisi ni sheria na Raisi yuko juu ya Sheria na ndiyo maana hakuna Mahakama ya kumshtaki wala kumhoji, hivyo mimi kwangu alivyofanya ni sawa kabisa kwa mazingira yetu jinsi yalivyo, kwa maana hiyo br. siyo mali yake bali ni mali ya wana Dar wote wakati kuna wengine wanatumia hiyo power kubwa ya Uongozi kusiphon fedha nje ya nchi huko kusaidia Wazungu, fisadi Lowasa, Mbowe &Co. wamehamisha mabilioni ya fedha zetu kupeleka Ulaya, Asia na Dubai fedha ambazo zinahitajika hapa nyumbani na zingeweza kutusaidia sana badala yake hizo fedha zinajenga Dubai, Hong Kong n.k na isitoshe bado Mbowe, Lowasa &Co. wanawachangisha masikini kwenye Mikutano yao hivyo hakuna mwenye moral authority ya kuhoji maamuzi ya Raisi Magufuli ya kutumia fedha zetu kujenga br. kwa matumizi yetu!
 
Back
Top Bottom