Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Katika dibaji ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010-2015, CHADEMA walisema, Kuna sababu tatu zilizosabisha nchi yetu ifike hapa ilipo, nazo ni: ufisadi, ufisadi na ufisadi. Ufisadi ndio tishio kubwa kabisa la mustakabali wa nchi yetu. Ndio kusema tukitaka tutoke hapa tulipo ni lazima tuukatae na tupambane na ufisadi.
Wakaenda mbali zaidi na kusema, Tumefanikiwa kuwaumbua mafisadi wanaoifilisi nchi yetu na ambao wamefunga fungate na Serikali ya CCM.
Hawakuishia hapo, wakasema, Hivyo basi, hatua ya kwanza ya kutoka hapa tulipo ni kuushugulikia kwa haraka ufisadi kwa kurudisha na kuhuisha uzalendo na uadilifu katika uongozi wa nchi.
Wakamalizia katika Ibara ya 6.4.1(V) ya Ilani ya Uchaguzi kwa kusema,Ili kuimarisha kujenga uongozi na kuimarisha utawala bora na utawala sheria, Serikali ya CHADEMA itachukua hatua zifuatazo:
Fast forward miaka mitano, utagundua Ilani yao ya Uchaguzi ilikuwa ni kama kikaratasi tu ambacho hakina maana yoyote hasa ikichukuliwa kwa sasa kauli za viongozi wa CHADEMA zimekuwa ni kama kauli za viongozi wa madhehebu ya dini.
Inaeleweka ni kazi ya madhehebu ya dini kuwasamehe wala rushwa na mafisadi lakini kazi ya serikali ni kuhakikisha wanapelekwa mahakamani ili kujibu mashitaka yao.
Yaani ndani ya serikali ya CHADEMA ukitubu dhambi zako za rushwa na ufisadi kwa maneno, unasamehewa na kuwa Mwanachama hai wa CHADEMA na kupewa uongozi.
Ni lini CHADEMA imegeuka na kuwa moja ya dhehebu la dini nchini Tanzania?
Hakuna dhambi mbaya kama ya kukubali kuendelea kutambaa matopeni badala ya kwenda kuoga utakate na uwe msafi.
Mtume Paulo (Saul) katika madhehebu ya Kikristo aliwatesa, aliwadhulumu na kuwaua wakristo wa Yerusalemu, lakini alipoongoka akawa mtume mkubwa katika kanisa na mfano wa kuigwa kwa maisha ya wapenda haki na amani duniani.
Mzee Ruksa alilazimika kujiuzuru kwa uzembe wake wa vifo vilivyotokea huko Shinyanga akiwa Waziri wa mambo ya ndani, akajiuzuru, akatubu na kujirekebisha na akajakuwa rais wa Tanzania visiwani na baadaye Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungua pazia la uchumi huria.
Je upo???????