Ni lini CHADEMA umegeuka kuwa dhehebu la dini?

Ni lini CHADEMA umegeuka kuwa dhehebu la dini?

Mkuu wangu Chadema ni walaghai na wapo kwa ajili ya maslahi tu juzi Mchungaji Msigwa anasema Chadema ni kama Kanisa.

Sasa watu kama hawa wakishika dola mafisadi wote watakuwa wanaenda kutubu kwa Mbowe au Dr.Slaa badala ya kupelekwa mahakamani.

Leo kuna pro-Chadema mmoja kaanzisha uzi anatufahamisha kuwa Lowassa hakutajwa na Slaa kwenye orodha ya mafisadi pale Mwembe Yanga wanadhani Watanzania wote wapo kama Bavicha wanaweza kuwashikia akili.
 
"Chadema ni kama kanisa tunaleta wokovu - Rev Msigwa "

Kwa hiyo ni kweli chadema wameanza kufanya kazi za madhebu hata kule monduli kuna kiongozi wa chadema aliwambia madiwa wamesamehewa dhambi za na zimeshafishwa na kuwa nyeupe kama saruji kuna mstari aliunukuu...nilijiuliza sana hawa wana fata misingi ya sheria zinazo waongoza au wana fanya kama dini zifanyavyo?

Kwa misingi ya ilani yao hiyo na tukitazama kauli za baadhi ya viongozi wao kuwa karibishwa walio watambua kama mafisadi nashindwa kuwaelewa watasema nini kuhusu kilichomo kwenye ilani?
 
Kabla hujawalaumu viongozi wa CDM kwa kuwapokea mafisadi ungeanza kwanza kuilamu serikali ya CCM kwa kutowachukulia sheria yoyote mafisadi hadi sasa. Siasa ni strategy. Lengo la CDM kukaribisha Wana CCM mafisadi kwa sasa ili kuing'oa kwanza CCM madarakani. Baada ya hapo kupambana na mfumo wenyewe wa kifisadi.
Kwa hiyo fisadi ata samehewa?
 
Fisadi yeyote anatakiwa kwa jela kama kina Mramba, hii habari ya kuwasamehe mafisadi kisa mnawakabidhi kadi za Chadema ndiyo utawala wa sheria.
 
Nadhani kuna tofauti kati ya a) kukumbatia ufisadi na b) kumfanya fisadi abadilike na kuwa mtu tofauti kabisa!
Mkuu,
Ni wapi kwenye Ilani ya Uchaguzi wametofautisha kama unavyotaka niamini?

Bila hata kutumia Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA, kuna taratibu za utawala wa sheria katika kushughulika na watenda makosa ya kijinai nchini.

Taratibu za kisheria zinaruhusu wafungwa kupewa msamaha baada ya kutumikia sehemu ya hukumu zao.
 
Mbowe anapenda pesa ajabu kishauza chama kwa 10bn kudadeki pesa hizi ibilisi
 
Mkuu,
Kwa hiyo wakati CHADEMA wanaandika Ilani yao ya Uchaguzi hawakufahamu kama hata mafisadi yatawangua mkono ili kuiangusha CCM?

Kwa hiyo baada ya mafisadi kuwaunga mkono CHADEMA ndiyo utakuwa mwisho wa ufisadi?
Tunakubaliana na mafisadi katika agenda moja tu ya kuung'oa mfumo wa ccm ulioko madarakani. Kama watapigia ukawa kura ya ndio na kuiondoa kabisa ccm, tunakubaliana nao kabisa, na tunawakaribisha. Huu ni wakati wa uchaguzi ambao kila mmoja anasaka kura za ndio bila kujali maadili ya anayepiga kura. Ndio maana tunawakaribisha wema na wabaya wote kutupigia kura ya ndio ifikapo 25/10.
 
CDM wakawasafishe na akina Muhongo, Tibaijuka, wamsafishe pia na Rostam wakimaliza hapo wamchukue na mzee wa vijisenti Chenge. ..CDM msichoke kusafisha ili tupate watakatifu wengi Tz
Mkuu,
CHADEMA hawasafishi mafisadi bali wanawasamehe mafisadi pindi wanapotubu dhambi za ufisadi!
 
Siasa za Chadema ni one day at a time. Hawana mkakati wowote uliokamilika. Usishangae Lowassa akiwakatalia kuwa mgombea wao wakienda kumuomba tena Samwel Sitta.
Ila hii inaonyesha Chadema wenyewe wanajua Slaa hafai kuongoza nchi, ndio maana wanahangaika kutafuta wagombea wakati yeye yupo...
Mkuu,
Nimeshangazwa kidogo na habari ya gazeti la Mwananchi ambalo linasemema hadi sasa hakuna mwanachama hata mmoja aliyejitokeza kuzichukua fomu za Urais ndani ya CHADEMA wakati Mbunge wa Nyamagana, Wenje alishanukuliwa na Star TV akisema Kamati Kuu ya CHADEMA imempitisha Dk. Slaa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA.

Angalia hii video kuhusu tamko la Wenje,

 
Last edited by a moderator:
Mkuu,
Nimeshangazwa kidogo na habari ya gazeti la Mwananchi ambalo linasemema hadi sasa hakuna mwanachama hata mmoja aliyejitokeza kuzichukua fomu za Urais ndani ya CHADEMA wakati Mbunge wa Nyamagana, Wenje alishanukuliwa na Star TV akisema Kamati Kuu ya CHADEMA imempitisha Dk. Slaa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA.


Angalia hii video kuhusu tamko la Wenje,



Chama cha magumashi hiki...
 
Last edited by a moderator:
Napenda mbinu hii ya Chadema ya watu kuwekwa matumbo moto.

Watu wanaougua matumbo si wana Chadema bali wahasimu wao.

Gumzo la jiji ni lini Chadema watamtangaza mgombea wao.

Asante Chadema, magamba mnawaumiza kweli kweli.
 
Unamsamehe muovu na kumpa mamlaka ya kukutawala hapohapo!

Kibwetele angekuja Tanzania angepata wateja wengi sana kumbe.
Angekupata hata wewe kwani la ajabu ni lipi si unapona hata Osama amekuwa na wapenzi ingawaje alifadhili kuua ndugu zetu hata kwenye magari unakuta picha yake kapozi na AK 47.Kule Afrika ya Kusini baada ya tata Madiba kutawala ulisikia kitu kilichoitwa tume ya ukweli na upatanishi?Ulimsikia Pinda kwenye maswali na majibu pale bungeni alisema wakitajwa wahusika wa EPA nchi itatetemeka?Nakuacha na hayo kwa leo mkuu wangu.

 
Au kwa maana nyingine amekubali kuwa Wanasiasa wa CDM pia ni mafisadi.
Mkuu,
Wakati mwingine nashangaa hizi hoja za baadhi ya watu wanaojaribu kutetea kauli za viongozi wa CHADEMA kuhusiana na ufisadi.

Kwa maana nyingine, CHADEMA kwa sasa wanaisaidia CCM 'kuvua magamba' yaliyokuwa yameng'ang'ania kiunoni!
 
chief, embu tuweke kando kwa muda hayo mambo ya CHADEMA na kashfa zako kwa dini za mwenyezi Mungu turudi kwa CCM yako.

mtuhumiwa mkuu wa ufisadi kwa muktadha uliopo ni EL. kama kweli yeye ni fisadi, imekuwaje hamjamfungulia mashitaka hadi leo? pili, ilikuwaje mwenyekiti wenu alifikia mahali pa kumnadi, tena kwa bashasha kabisa, kwenye kampeni za October 2010?

Mkuu,
Kwa hiyo kwa vile CCM haijamfungulia mashitaka basi hata serikali ya CHADEMA ikiingia madarakani haiwezi kumfungulia mashitaka?

Mbona Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA inasema itahakikisha wale walitajwa kwenye list of shame, Mwembeyanga hata kama ni Marais waliostaafu watafikishwa mahakamani baada ya kuondolewa political immunity.

Kwa hiyo unataka kusema halali ya CCM ni halali ya CHADEMA na haramu ya CCM ni haramu ya CHADEMA. Kumbe hakuna hata umuhimu wa uwepo wa CHADEMA kwa sababu yanayofanywa na CCM ndiyo yatakayofanywa na CHADEMA!

Chief, huu sio utetezi hata kidogo!
 
List of shame ni valid mpk leo hii, haijawahi kupingwa. Ilani hiyo ya uchaguzi ndio ilikuwa CDM ikichukua nchi iifate, so why CDM wanakuwa 2 faced? Btw, Ili Fisadi abadilike awe tofauti na kiukweli aonekane ametubu, msingi mkuu tutakaoamini kuwa ametubu na amebadilika ni kuona kuwa amekiri kufanya ufisadi na amerudisha kila mali ya umma aliyohodhi na kuiba. Maneno matupu pekee hayavunji mfupa.
Mkuu,
Ninashangaa sana baadhi ya watu wameanza kuja na kauli za huruma wakati msingi wa Ilani ya CHADEMA ilikuwa ni kuhakikisha mafisadi wanafikishwa mahakamani.

Kwa sasa wameanza kuikana hata Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA.

Kuna kitu hakiko sawa kwa sasa ndani ya CHADEMA!
 
attachment.php

maxresdefault.jpg


​Na hii ni KWELI KABISA!
 
Chadema ni ulaghai mtupu dhidi ya ufisadi
Mkuu,
Kwa wale ambao kweli wameingia ndani ya CHADEMA kwa kuvutiwa na Sera na Itikadi itakuwa ni vigumu sana kuvutiwa na maneno yanayosemwa na viongozi wakuu wa chama.

Kuna maelfu kama siyo malaki ambao walivutiwa na nia/bidii ya CHADEMA katika kupambana na ufisadi, lakini ninaamini kwa kinachotokea kwa sasa itabidi wajiulize mara mbili mbili kama walichokuwa wanakiona kilikuwa kinatoka ndani ya mioyo ya viongozi wa CHADEMA au ulikuwa ni usanii tu.
 
kwanza hongera kwa uchambuzi huo, umefanya kazi kubwa na kuweka reerences. lakini ni kusaidie pia kidogo nadhani umeongea from the blue sky, na pengine umeacha baadhi ya issues, moja ni fisadi gani Chadema imepokea? ni wapi Chadema wamesamehe fisadi? lakini ukumbuke kuwa CCM na serikali yake ndio wameuwa wakiendesha serikali kwa msingi wa kikristo wa samehe saba mara sabini, yaani waliokula la EPA wanaambiwa wamerudisha wakasamehewa, huo i utawala wa kisheria kweli? yaani eti waliosema vijisenti na Escrow na kutumia nguvu kushambulia watu ei nao wamesamehewa na pengine kubewa adhabu ya miezi sita eti? eti hata wale waliokili kuchukua tu pesa kidgogo kuwa wanzo nyingi nyumbani kwao nao wamesamehewa, unaanzia wap uisema chadema kuhusu msimamo wake?
Katika dibaji ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010-2015, CHADEMA walisema, Kuna sababu tatu zilizosabisha nchi yetu ifike hapa ilipo, nazo ni: ufisadi, ufisadi na ufisadi. Ufisadi ndio tishio kubwa kabisa la mustakabali wa nchi yetu. Ndio kusema tukitaka tutoke hapa tulipo ni lazima tuukatae na tupambane na ufisadi. ‘’

Wakaenda mbali zaidi na kusema, ‘’ Tumefanikiwa kuwaumbua mafisadi wanaoifilisi nchi yetu na ambao wamefunga fungate na Serikali ya CCM’’.

Hawakuishia hapo, wakasema, ‘’ Hivyo basi, hatua ya kwanza ya kutoka hapa tulipo ni kuushugulikia kwa haraka ufisadi kwa kurudisha na kuhuisha uzalendo na uadilifu katika uongozi wa nchi’’.

Wakamalizia katika Ibara ya 6.4.1(V) ya Ilani ya Uchaguzi kwa kusema,’’Ili kuimarisha kujenga uongozi na kuimarisha utawala bora na utawala sheria, Serikali ya CHADEMA itachukua hatua zifuatazo:

Fast forward miaka mitano, utagundua Ilani yao ya Uchaguzi ilikuwa ni kama kikaratasi tu ambacho hakina maana yoyote hasa ikichukuliwa kwa sasa kauli za viongozi wa CHADEMA zimekuwa ni kama kauli za viongozi wa madhehebu ya dini.

Inaeleweka ni kazi ya madhehebu ya dini kuwasamehe wala rushwa na mafisadi lakini kazi ya serikali ni kuhakikisha wanapelekwa mahakamani ili kujibu mashitaka yao.

Yaani ndani ya serikali ya CHADEMA ukitubu dhambi zako za rushwa na ufisadi kwa maneno, unasamehewa na kuwa Mwanachama hai wa CHADEMA na kupewa uongozi.

Ni lini CHADEMA imegeuka na kuwa moja ya dhehebu la dini nchini Tanzania?
 
Back
Top Bottom