Ni lini CHADEMA umegeuka kuwa dhehebu la dini?

Ni lini CHADEMA umegeuka kuwa dhehebu la dini?

Katika dibaji ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010-2015, CHADEMA walisema, Kuna sababu tatu zilizosabisha nchi yetu ifike hapa ilipo, nazo ni: ufisadi, ufisadi na ufisadi. Ufisadi ndio tishio kubwa kabisa la mustakabali wa nchi yetu. Ndio kusema tukitaka tutoke hapa tulipo ni lazima tuukatae na tupambane na ufisadi. ‘’

Wakaenda mbali zaidi na kusema, ‘’ Tumefanikiwa kuwaumbua mafisadi wanaoifilisi nchi yetu na ambao wamefunga fungate na Serikali ya CCM’’.

Hawakuishia hapo, wakasema, ‘’ Hivyo basi, hatua ya kwanza ya kutoka hapa tulipo ni kuushugulikia kwa haraka ufisadi kwa kurudisha na kuhuisha uzalendo na uadilifu katika uongozi wa nchi’’.

Wakamalizia katika Ibara ya 6.4.1(V) ya Ilani ya Uchaguzi kwa kusema,’’Ili kuimarisha kujenga uongozi na kuimarisha utawala bora na utawala sheria, Serikali ya CHADEMA itachukua hatua zifuatazo:

Fast forward miaka mitano, utagundua Ilani yao ya Uchaguzi ilikuwa ni kama kikaratasi tu ambacho hakina maana yoyote hasa ikichukuliwa kwa sasa kauli za viongozi wa CHADEMA zimekuwa ni kama kauli za viongozi wa madhehebu ya dini.

Inaeleweka ni kazi ya madhehebu ya dini kuwasamehe wala rushwa na mafisadi lakini kazi ya serikali ni kuhakikisha wanapelekwa mahakamani ili kujibu mashitaka yao.

Yaani ndani ya serikali ya CHADEMA ukitubu dhambi zako za rushwa na ufisadi kwa maneno, unasamehewa na kuwa Mwanachama hai wa CHADEMA na kupewa uongozi. Mbaya zaidi, hata wale waliowataja kama mafisadi papa kwa sasa mlango uko wazi wa kutubu na kusamehewa!

Ni lini CHADEMA imegeuka na kuwa moja ya dhehebu la dini nchini Tanzania?

Mbona upo obsessed sana na Chadema? Kuna busara inaeleza "asiye na zuri la kujiongelea huhangaika kuzungumzia 'mabay' ya wenzie."
 
Mkuu nisaidie maana mie sijaenda shule kama wewe,hivi Hapa na wakulaumiwa,chadema wanaotaka kutumia silaha waliyosema iteketezwe kwa Kuwa inatumika kuwaua watu au serikali iliyoshindwa kuiteketeza silaha hiyo na kuiacha iendelee kuua watu?na je huoni kama wakiitumia then ikawasaidia kupata uwezo wa kuteketeza silaha zingine zinazoendelea kuua watu huoni Hilo likawa ni jambo jema

daaaah??? Zimwi likujualo.....hyo silaha haiwez kuteketeza zote wakati nyingine ndo chambo chake cha kufanyiia kazi mkuu
 
Badala ya kupigana na mtu mmoja mmoja, CDM imeamua kupigana na MFUMO (read kuondoa mfumo unaozalisha mafisadi na ufisadi ambao ni CCM).

Simple and clear
Mkuu,
Kwani mfumo ulishuka kutoka mawinguni?

Mfumo unajengwa na binadamu. Binadamu wanaojenga mfumo wa ufisadi ni mafisadi.

Unapoanza kuwachukua binadamu waliojenga/waliojenga mfumo wa ufisadi na kuwafanya wawe wapambana na mfumo wa ufisadi ni kuhamisha mfumo wa ufisadi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
 
Kwa muungano huu wa kimaslahi wa UKAWA sijaona upinzani Tz hebu nihamishie kambi yangu ACT labda ntaona jipya,
Kuna watu wenye macho lakini hawaoni na tena wana masikio lakini hawasikii! Taabu sana watu wa jinsi hii! Kazi kwelikweli!
 
Mkuu,
Kwani mfumo ulishuka kutoka mawinguni?

Mfumo unajengwa na binadamu. Binadamu wanaojenga mfumo wa ufisadi ni mafisadi.

Unapoanza kuwachukua binadamu waliojenga/waliojenga mfumo wa ufisadi na kuwafanya wawe wapambana na mfumo wa ufisadi ni kuhamisha mfumo wa ufisadi kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

JUMUIKO la vyama vinavyounda muungano wa kutetea katiba ya Wananchi (UKAWA), linatarajiwa kumtangaza mgombea wake urais jioni hii, jijini Dar es Salaam. Anaandika Saed Kubenea … (endelea).

Taarifa kutoka ndani ya umoja huo zinasema, mgombea urais wa UKAWA aweza kupatikana leo, baada ya mashauriano ya kina yaliyofanyika baina ya viongozi wakuu wa vyama vinavyounda umoja huo. “Jioni hii ya leo, tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la kumtangaza mgombea wetu wa urais. Tutatangaza moja kwa moja mgombea au tutakitangaza chama ambacho kitatoa mgombea,” ameeleza mmoja wa viongozi wakuu wa UKAWA kwa sharti la kutotajwa gazetini. Amesema, “ikiwa tutakitangaza chama, basi kitakachofuata, ni kukiruhusu kuendelea na mchakato wake wa ndani. Lakini katika hayo mawili, moja lazima litafanyika, tutangaza mgombea au chama kitakachotoa
mgombea. Mkutano wa viongozi wakuu wa UKAWA unaotarajiwa kutangaza mgombea wake urais, umepangwa kufanyika katika hoteli ya Bahari Beach.

Kwa mujibu wa mtoa taarifa wa gazeti hili, chama ambacho kitatoa mgombea urais wa Muungano, kimetajwa kuwa Chadema. Mgombea urais wa Zanzibar, atatoka CUF. Anasema, makubaliano kuwa Chadema ndicho kitoe mgombea urais wa Muungano tayari yameridhiwa na Baraza Kuu la Uongozi la CUF, lililokutana mjini Zanzibar jana Jumamosi. Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema, hatua ya CUF mmoja wa washirika wakubwa katika umoja huo kuridhia Chadema kutoa mgombea urais, limekuwa pigo kubwa kwa wapinzani wa muungano huo. “Haya mawili ya rais wa Muungano na rais wa Zanzibar, tayari tumekubaliana. Chadema kitatoa mgombea urais wa Muungano na CUF kitatoa mgombea mwenza. Mbali na mgombea mwenza, CUF kitatoa pia mgombea urais wa Zanzibar,” anaeleza kiongozi huyo.

Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya Chadema zinasema, chama hicho kinaweza kuzuia kumtangaza mgombea wake wa urais katika mkutano wa leo na waandishi wa habari, ili kukamilisha mazungumzo yake ya ndani. Kinachoitwa na chama hicho, “mazungumzo ya ndani,” kimetajwa na afisa mmoja wa Chadema kuwa ni suala la kuchelewa kupatikana jina la mgombea mwenza kutoka CUF. Aidha, taarifa zinasema, kushindwa kwa chama hicho kumtangaza mgombea wake urais wa Muungano, kunatoka pia na kutokamilika kwa “mashauriano” kati yake na mmoja wa watu muhimu nje ya chama hicho.”

Lakini kwa zaidi ya wiki mbili sasa, vyombo vya habari vimenukuu vyanzo mbalimbali vya taarifa vikieleza, anayesubiriwa na Chadema kutoka nje ya chama, ni mbunge wa Mondoli (CCM), Edward Lowassa. Taarifa kuwa Lowassa, mmoja wa wanasiasa machachari nchini, anataka kujiunga na Chadema, zimepamba moto katika wiki za hivi karibuni baada ya jina lake kuenguliwa katika hatua za awali katika kinyang’anyiro cha urais kupitia CCM. Tayari madiwano 20 na viongozi wengine mbalimbali wa CCM wamekihama chama hicho na kujiunga na Chadema, jambo ambalo limeashiria kukamilika kwa safari ya kiongozi huyo ndani ya Chadema.

Chanzo: MwanaHalisi Online
 
JUMUIKO la vyama vinavyounda muungano wa kutetea katiba ya Wananchi (UKAWA), linatarajiwa kumtangaza mgombea wake urais jioni hii, jijini Dar es Salaam. Anaandika Saed Kubenea … (endelea).

Chanzo: MwanaHalisi Online
Mkuu,
Wamemtangaza...?
 
Mbona upo obsessed sana na Chadema? Kuna busara inaeleza "asiye na zuri la kujiongelea huhangaika kuzungumzia 'mabay' ya wenzie."
Mkuu,
Busara vile vile zinaniambia umekosa hoja ndiyo maana umekimbilia kwenye neno obsessed!

Umetumia kipimo gani kufikia kwenye hitimisho linalosema niko obsessed sana na Chadema?
 
Mkuu,
Haya siyo maneno yangu bali ni Ilani ya Uchaguzi ya Chadema!

kwanini unatumia maneno ya ilani ya uchaguzi 2010-2015 huku ukijua kuwa cdm bado haijatoa ilani ya 2015-2020?hata ccm tu bado yao haijatoka!sio tabia njema kutumia elimu,taaluma au uelewa wako ili kupotosha ukweli.Na hicho kifungu ulichotaja kinaelezea kupokea wanachama au kuwashitaki wezi?Na kuwashitaki siku180 baada ya nini?hizo siku 180 zimefika au bado?mkiweka mada mjipange ili tuone hoja,hv wenzenu wa upinzani mbona wanawashinda kujenga hoja mara nyingi hata bungeni?
 
Mkuu,
Wamemtangaza...?
Mkuu Ng'wamapalala.

Huyu jamaa ni wa kumuonea huruma huo uzi umeletwa asubuhi hapa na Lizaboni sasa yeye kaenda kwa Kubenea kaucopy anadhani kaja na kitu kipya nimecheka sana anavyousambaza kama kapagawa si bure lazima atakuwa kanywa banana si unajua uwa wanapewa pale UFIPA.
 
Last edited by a moderator:

Kuna wanaJF wengine inataka moyo kujibu hoja zao.

Hata hivyo, tutaenda nao pole pole kwa faida ya janvi.
 
kwanini unatumia maneno ya ilani ya uchaguzi 2010-2015 huku ukijua kuwa cdm bado haijatoa ilani ya 2015-2020?hata ccm tu bado yao haijatoka!sio tabia njema kutumia elimu,taaluma au uelewa wako ili kupotosha ukweli.Na hicho kifungu ulichotaja kinaelezea kupokea wanachama au kuwashitaki wezi?Na kuwashitaki siku180 baada ya nini?hizo siku 180 zimefika au bado?mkiweka mada mjipange ili tuone hoja,hv wenzenu wa upinzani mbona wanawashinda kujenga hoja mara nyingi hata bungeni?
Mkuu,
Kwani hufahamu kuwa mpaka sasa CHADEMA ndiyo serikali kivuli?

Hii ndiyo Ilani ya Uchaguzi inayotumiwa na CHADEMA katika utekelezaji wa kazi za serikali kivuli.

Kwani hufahamu hilo?
 
Mkuu nisaidie maana mie sijaenda shule kama wewe,hivi Hapa na wakulaumiwa,chadema wanaotaka kutumia silaha waliyosema iteketezwe kwa Kuwa inatumika kuwaua watu au serikali iliyoshindwa kuiteketeza silaha hiyo na kuiacha iendelee kuua watu?na je huoni kama wakiitumia then ikawasaidia kupata uwezo wa kuteketeza silaha zingine zinazoendelea kuua watu huoni Hilo likawa ni jambo jema
Mkuu,
Nitakusaidia vipi wakati hoja yako haieleweki!

This is classic argumentum ad populum!
 
Kabla hujawalaumu viongozi wa CDM kwa kuwapokea mafisadi ungeanza kwanza kuilamu serikali ya CCM kwa kutowachukulia sheria yoyote mafisadi hadi sasa. Siasa ni strategy. Lengo la CDM kukaribisha Wana CCM mafisadi kwa sasa ni ili kuing'oa kwanza CCM madarakani. Mengine baadae. Safari hii tunataka Chengu ajikaange kwa mafuta yake mwenyewe ili tutimize malengo kwanza!

Amma kwa hakika JF mapunguani ni wengi na kwa bahati nzuri kabisa wewe ni mmoja wapo.

Huyo unaemuita "Chengu" nnauhakika akisema leo hii anahamia chadema mtampokea kwa shangwe na hoi hoi na vifijo.
 
Japo hata polisi humtumia jambazi kupata kupata taarifa za jambazi sugu, kwenye hili Chadema wakimsafisha mhali, sitapigia kura eneo la urais.
 
Mkuu,
Kwani hufahamu kuwa mpaka sasa CHADEMA ndiyo serikali kivuli?

Hii ndiyo Ilani ya Uchaguzi inayotumiwa na CHADEMA katika utekelezaji wa kazi za serikali kivuli.

Kwani hufahamu hilo?
Kwahiyo Tanzania inatekeleza sera zake kwa ilani ya ccm na cdm?kazi ya serikali kivuli ni ipi?karibu kwenye mjadala.
 
Back
Top Bottom