Ni lini CHADEMA umegeuka kuwa dhehebu la dini?

Ni lini CHADEMA umegeuka kuwa dhehebu la dini?

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,507
Katika dibaji ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010-2015, CHADEMA walisema, Kuna sababu tatu zilizosabisha nchi yetu ifike hapa ilipo, nazo ni: ufisadi, ufisadi na ufisadi. Ufisadi ndio tishio kubwa kabisa la mustakabali wa nchi yetu. Ndio kusema tukitaka tutoke hapa tulipo ni lazima tuukatae na tupambane na ufisadi. ''

Wakaenda mbali zaidi na kusema, '' Tumefanikiwa kuwaumbua mafisadi wanaoifilisi nchi yetu na ambao wamefunga fungate na Serikali ya CCM''.

Hawakuishia hapo, wakasema, '' Hivyo basi, hatua ya kwanza ya kutoka hapa tulipo ni kuushugulikia kwa haraka ufisadi kwa kurudisha na kuhuisha uzalendo na uadilifu katika uongozi wa nchi''.

Wakamalizia katika Ibara ya 6.4.1(V) ya Ilani ya Uchaguzi kwa kusema,''Ili kuimarisha kujenga uongozi na kuimarisha utawala bora na utawala sheria, Serikali ya CHADEMA itachukua hatua zifuatazo:
6.4.1(v) Viongozi wote wa kisiasa na watumishi wa umma ambao walishabainishwa kujihusisha na ufisadi na ubadhirifu (rejea orodha ya mafisadi) ya umma lakini Serikali ya CCM imeshindwa kuwafikisha mahakamani kwa kuwa ni washiriki, watafikishwa mahakamani ndani ya siku 180 chini ya Sheria ya Kuzuia Mitandao ya Uhalifu na Uhujumu Uchumi ya 1984 pamoja na Sheria nyingine zozote ambazo zitaonekana zimevunjwa. Wale watakaothibitika mahakamani kuhusika na vitendo vya ufisadi, pamoja na kuadhibiwa na mahakama, mali zao zitataifishwa na kurudishwa serikalini. Katika hili viongozi waliopita (wakiwemo Marais) ambao wataonekana kuhusika na vitendo vyovyote vya ufisadi au uvunjaji wa sheria watavuliwa kinga zao na Bunge ili hatimaye waweze kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yao yatakayoletwa na Taifa lao. Hakutakuwa na kiongozi ambaye hatoweza kufikishwa mahakamani kama amefanya vitendo vya uhalifu akiwa madarakani.
Fast forward miaka mitano, utagundua Ilani yao ya Uchaguzi ilikuwa ni kama kikaratasi tu ambacho hakina maana yoyote hasa ikichukuliwa kwa sasa kauli za viongozi wa CHADEMA zimekuwa ni kama kauli za viongozi wa madhehebu ya dini.

Inaeleweka ni kazi ya madhehebu ya dini kuwasamehe wala rushwa na mafisadi lakini kazi ya serikali ni kuhakikisha wanapelekwa mahakamani ili kujibu mashitaka yao.

Yaani ndani ya serikali ya CHADEMA ukitubu dhambi zako za rushwa na ufisadi kwa maneno, unasamehewa na kuwa Mwanachama hai wa CHADEMA na kupewa uongozi. Mbaya zaidi, hata wale waliowataja kama mafisadi papa kwa sasa mlango uko wazi wa kutubu na kusamehewa!

Ni lini CHADEMA imegeuka na kuwa moja ya dhehebu la dini nchini Tanzania?
 
Kabla hujawalaumu viongozi wa CDM kwa kuwapokea mafisadi ungeanza kwanza kuilamu serikali ya CCM kwa kutowachukulia sheria yoyote mafisadi hadi sasa. Siasa ni strategy. Lengo la CDM kukaribisha Wana CCM mafisadi kwa sasa ni ili kuing'oa kwanza CCM madarakani. Mengine baadae. Safari hii tunataka Chengu ajikaange kwa mafuta yake mwenyewe ili tutimize malengo kwanza!
 
Mkuu ulitka cdm ichukue nafasi na wajibu wa chama kilichopo(ccm) kuwahukumu wanachama unaowaita mafisadi wala rushwa.. hao wanaopokelewa chadema ni wanachama waliokuwa makada wa ccm, na walikuwa mafisadi wakiwa ccm na wala hawajawai kuwajibishwa na kupelekwa kwenye vyombo vya dola. sasa unalalamika nini kama mmama mwenye mimba anaekaribia kujifungua kwa kuwalazimisha cdm kuwakataa hao makada wanaohama ccm na kujiunga cdm baada ya kutubu.. kwenye harakati aijalishi ni mtu gani au wa aina gani ilimradi atafuata taratibu na miiko ya chama hyo ni mumini mzuri sana katika kukomboa watanzania kutoka kwa mkoloni mweusi,
 
Viongozi wakuu wa chadema wote ni mafisadi isipokuwa babu slaa tu kwahiyo hawana jipya wanalofanya ni kutembea kwenye njia zao zile zile.
 
Mashangao makubwa, waliokuwa wanadaiwa ni mafisadi (ccm) sasa wanakaribishwa ukawa. Kumbe lengo la ukawa ni madaraka tu na si vinginevyo.
 
mkuu unafkir kila kitu ni cha kujibu, kuna mengineo ni ushuzi aiwezekani kujibu

Ilikuwaje mkawadanganya wananchi kuwa mngewapeleka mafisadi mahakamani na kuwafunga kama mtu "akitubu" anasamehewa? Kusamehe si ni kazi ya makanisa na misikiti?!

CHADEMA ni chama cha kilaghai.
 
Siasa ni strategy. Lengo la CDM kukaribisha Wana CCM mafisadi kwa sasa ni moja. Kuing'oa kwanza CCM madarakani. Baada ya hapo kupambana na mfumo wenyewe wa kifisadi.
Tuangalien. hyo kauli mm cjaona ukweli & km mafsad wakienda cdm mm ntahama. cwezi kufuata mafsadi. Hii nafananisha na mbwa kumfuata chatu. huku ni kupoteza dira na tamaa. Mafsadi hawatatupeleka ppte & naamn walshatubu sana huko makansan ila bado sembuse cdm
 
kamanda the other wise..ccm ndyo inayoendeshwa kwa njia ya kilaghai na kitapeli

Ni lini CHADEMA imegeuka kuwa dhehebu la dini na kuanza kusamehe mafisadi na wala rushwa?

Kwa namna hii na zile porojo zenu za kipindi kile inamaana hakuna mtu ambaye angefikishwa mahakamani wala kufungwa, wangetubu waendelee "kula maisha".
 
Mashangao makubwa, waliokuwa wanadaiwa ni mafisadi (ccm) sasa wanakaribishwa ukawa. Kumbe lengo la ukawa ni madaraka tu na si vinginevyo.

Kwa mwendo huu inamaana hawa CHADEMA wakifanikiwa kuingia Ikulu (kitu ambacho ni ndoto) hata mahakama wataziondoa kwasababu hazitakuwa na kazi tena watu watakuwa wanatubu wanasamehewa.

Kweli wajinga ndiyo waliwao.
 
Siasa ni strategy. Lengo la CDM kukaribisha Wana CCM mafisadi kwa sasa ni moja. Kuing'oa kwanza CCM madarakani. Baada ya hapo kupambana na mfumo wenyewe wa kifisadi.
Mkuu,
Umesoma vizuri thread yangu au umesoma tu kichwa cha thread na kujibu.

Soma tena vizuri!
 
Mkuu ulitka cdm ichukue nafasi na wajibu wa chama kilichopo(ccm) kuwahukumu wanachama unaowaita mafisadi wala rushwa.. hao wanaopokelewa chadema ni wanachama waliokuwa makada wa ccm, na walikuwa mafisadi wakiwa ccm na wala hawajawai kuwajibishwa na kupelekwa kwenye vyombo vya dola. sasa unalalamika nini kama mmama mwenye mimba anaekaribia kujifungua kwa kuwalazimisha cdm kuwakataa hao makada wanaohama ccm na kujiunga cdm baada ya kutubu.. kwenye harakati aijalishi ni mtu gani au wa aina gani ilimradi atafuata taratibu na miiko ya chama hyo ni mumini mzuri sana katika kukomboa watanzania kutoka kwa mkoloni mweusi,
Mkuu,
Umesoma Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA Ibara ya 6.4.1(v)?

Naomba usome tena vizuri!
 
Mkuu,
Una maana gani?

Nielimishe!
attachment.php
 
Kama fisadi leo ataamua kwa dhati kuupinga mfumo wa kifisadi wa CCM, anakaribishwa chadema kwa ajili ya lengo hilo. Nyakati hizi za Uchaguzi mkuu anayeunga mkono kuiangusha ccm nirafiki yetu mkubwa bila kujali alikotoka!! Kura ya kila mtu kwetu ni ya muhimu sana bila kujali dini yake, msimamo wake, itikadi yake n.k.!! Tunaomba kila mtu ifikapo oktoba 25 aka
 
Back
Top Bottom