Ni lazima kutuma pesa ukweni?

DissDotCom

JF-Expert Member
Mar 31, 2014
395
268
Jamani swali langu hivi ni lazima kutuma pesa ukweni?

Hivi unapokua umeoa na tayari umeshalipa mahali umekabidhiwa mke na mmeanzisha maisha yako kuna umuhimu wowote wa kuwatumia pesa wazazi wa mwanamke kila mwisho wa mwezi?

Japo ulazima upo kwenye zawadi pale ambapo unaenda kuwatembelea.
 
Ngoja kwanza, anayetuma ni mkeo au wewe? Kama ni wewe, usipotuma anayelalamika ni mkeo au wakwe zako?

Kama ni mkeo, ni kutokana na mshahara wake? Wengi wanajificha hapa kuwa eti alisomeshwa!

Je, wewe pia kwenu unatuma kwa ‘ratiba' maalum kila baada ya kipindi fulani?
 
Hapa suala si ukweni, bali kusaidia wazazi. Hao wakwe kwa mkeo ni wazazi na kwa ndoa yenu ni wazazi wako pia hivyo unawajibika kuwasaidia.

Ndoa ni taasisi pana sana na mambo madogo ndo mambo makubwa katika ndoa. Furaha ya mkeo inategemea pia wazazi wake. Hivyo ili kuepusha misuguano ni vema mkakakaa na kukubaliana namna ya kuwasaidia wazazi au ndugu kwa kuzingatia kipato chenu.

Epuka dhana kwamba we ndo unawasaidia eti kwa sababu mkeo hana 'kazi' 'mama wa nyumbani'. Mkeo angekuwa mwenyewe bado angepambana ili kusaidia wazazi wake.
 
Ukioa familia maskini na wavivu jiandae kutegemewa kwa kila kitu. Tena wapo ladhi kutumia hata madawa ili wakupumbaze.

Wape mtaji wa laki moja waanzishe mradi wa kuku wa kienyeji ili wasikusumbue tena.

Wakila mtaji wataona aibu kukutafuta tena. Tumia hii ni mbinu ya kibaharia.
 
Acha nidandie treni kwa mbele.

Ukishaoa unaishi maisha yako kwa namna utayokubaliana na mwenzako huku mkochukua tahadhari ya jamii inayowazunguka namna wanavyoishi mnaweza jikuta nanyi mnaishi kama wao japo si sheria.

Kama baba yako yupo, muulize yeye alikuwa anapeleka pesa ukweni?
Kama una kaka wakubwa wailize pia. Kama una dada zako wameolewa muulize mama au baba, shemeji yako anawapa mshiko kila mwezi?

Kuna wanaopeleka matumizi (pesa na vitu) ukweni kila mwezi kwa ridhaa yao kama shukrani kwa kile mkewe anachomfanyia (Mahaba, utamu, mapishi, kujua kulea watoto na ndugu wa mume, anajua bajeti yaani sio mbahili sio mfujaji wa hela, sio mchoyo, hana gubu n.k.)

Hainaga fomula ukikuta unakerwaaa hata ukipigiwa simu na mkwe unajiskia kutukana 😂😂

Nimeteremka kwenye treni nililodandia.

Alamsiki.
 
Nimeoa tabata tu hapo, ila tangu nimeonekana siku y kutoa mahali (sijui ni mahari au nn) nimekuja kutia maguu ukweni after 5 years, wakwe tunaonana juu kwa juu tu like kwenye misiba n.k.

Nakumbuka after hiyo 5 years nilikwenda kawaida kabisaaaa na nauli yangu ya kurudia 400 mfukoni.

NB: Nawajibika pale inapolazimu tu. Ni vile maisha yetu tulivyoamua kuyaweka.#NoOffense#NoHardFeelings.
 
Hakuna ubaya, hasa kama mtasaidia wazazi wa pande zote mbili. Shida inaibuka pale mwanandoa mmoja anapotaka kuelekeza msaada kwa wazazi wake tu.
 
Jamani swali langu hivi ni lazima kutuma pesa ukweni?

Hivi unapokua umeoa na tayari umeshalipa mahali umekabidhiwa mke na mmeanzisha Maisha yako kuna umuhimu wowote wa kuwatumia pesa wazazi wa mwanamke kila mwisho wa mwezi?

Japo ulazima upo kwenye zawadi pale ambapo unaenda kuwatembelea.
Makosa uliyafanya wwe toka mwanzo,kwa kuwaweka Wakwe zako kwenye budget yako ya kila mwezi,sawa siyo mbaya labda kipindi cha nyuma hali yako kifedha ilikua poa! Sasa kama hali ya kifedha imebdalika wwe ongea na Wife wako hali halisi,na wao watajiongoza! Ila shida itakua Kama Mke wako ndiyo first born kwao hapo kazi unayo, maana yeye ndiyo Mara nyingi anahesabiwa Kama breadwinner wa familia!!
 
Jamani swali langu hivi ni lazima kutuma pesa ukweni?

Hivi unapokua umeoa na tayari umeshalipa mahali umekabidhiwa mke na mmeanzisha Maisha yako kuna umuhimu wowote wa kuwatumia pesa wazazi wa mwanamke kila mwisho wa mwezi?

Japo ulazima upo kwenye zawadi pale ambapo unaenda kuwatembelea.
Hakuna ulazima ila ukioa katika familia za kishamba na zenye Uswahili ni mateso tutafute wanawake waliolelewa katika familia zenye misingi ya dini ili kuepusha usumbufu na taabu.
Wanawake wa uswahilini wanaotoka katika familia za kiswahili zisizo kuwa na maadili ni viburudisho tu hawafai kuwaoa ikitokea bahati mbaya ukaoa ni mateso tu.
 
Jamani swali langu hivi ni lazima kutuma pesa ukweni?

Hivi unapokua umeoa na tayari umeshalipa mahali umekabidhiwa mke na mmeanzisha Maisha yako kuna umuhimu wowote wa kuwatumia pesa wazazi wa mwanamke kila mwisho wa mwezi?

Japo ulazima upo kwenye zawadi pale ambapo unaenda kuwatembelea.
Unatuma pesa za nini ukweni? Una mkataba nao wa biashara? Kama hali inaruhusu unaweza kuwatumia mara moja moja sio mbaya kuwaonyesha wakwe zako kwamba unawajali, lakini sio lazima especially kama nyie wenyewe hamjaweza kujisimamia, angalieni kwanza maisha yenu
 
Back
Top Bottom