Masagala
JF-Expert Member
- Jan 28, 2017
- 1,772
- 3,046
TrueHapa suala si ukweni, bali kusaidia wazazi. Hao wakwe kwa mkeo ni wazazi na kwa ndoa yenu ni wazazi wako pia hivyo unawajibika kuwasaidia.
Ndoa ni taasisi pana sana na mambo madogo ndo mambo makubwa katika ndoa. Furaha ya mkeo inategemea pia wazazi wake. Hivyo ili kuepusha misuguano ni vema mkakakaa na kukubaliana namna ya kuwasaidia wazazi au ndugu kwa kuzingatia kipato chenu.
Epuka dhana kwamba we ndo unawasaidia eti kwa sababu mkeo hana 'kazi' 'mama wa nyumbani'. Mkeo angekuwa mwenyewe bado angepambana ili kusaidia wazazi wake.