Ni lazima kutuma pesa ukweni?

Ni lazima kutuma pesa ukweni?

Nina Standing order moja tu kwa Bi mkubwa tarehe 27 kila mwezi anapokea mpunga the rest nawapa pakiwa na changamoto au sherehe
 
Jamani swali langu hivi ni lazima kutuma pesa ukweni?

Hivi unapokua umeoa na tayari umeshalipa mahali umekabidhiwa mke na mmeanzisha Maisha yako kuna umuhimu wowote wa kuwatumia pesa wazazi wa mwanamke kila mwisho wa mwezi?

Japo ulazima upo kwenye zawadi pale ambapo unaenda kuwatembelea.
Naomba kukuuliza ,
1)mke wako Ni mfanyakazi?au Ana shughuli inayomuingizia kipato?

2)wewe unaona kuna umuhimu wa kuwatumia pesa wazazi wako Kila mwisho wa mwezi? Jibu la hapa Lina majibu ya swali lako
 
Si lazima lakini utu na ubinaadamu uchukue nafasi. Wale pia ni wazazi wako. Kama unampenda mkeo utapenda pia kuona furaha yake. Sidhani mke kama atafurahia kula kuku ili hali wazazi wake wanateseka na cabbage kila siku.
Umeongea vyema
 
Inategemea na uwezo wa wakwe wako. Kama Hawana uwezo nivyema kuwasaidia kuhakikisha Wanaweza walau kupata chakula cha kila Siku.
Kama tunavyowasaidia watu wenye Shida wengine tuwasaidie pia wazazi wetu wanapokua na uhitaji.
Mie naona chakuzingatia ni uwezo wa mtoaji, je unao uwezo wa kuwasaidia? Kama unao uwezo ni jambo zuri kuwasaidia lakini pia unayo nia ya kuwasaidia? Usijilazimishe kusaidia bila mwenyewe kuridhia maana utakua unasaidia kwa lazima bila Hiari.
Kwahiyo kusaidia au kutokusaidia ni hiari na kadiri ya uwezo ingawa Kama Mungu kakujalia wasaidie wazazi wako wa pande zote na watu wengine wenye uhitaji.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Siyo lazima lakini Kama kuna issue imetokea na inahitaji msaada waking siyo mbaya ukasaidia...
 
Inategemea na ukweni kwako. Unaweza kumtumia kiasi gani Bakhressa akiwa mkwe wako?
Jamani swali langu hivi ni lazima kutuma pesa ukweni?

Hivi unapokua umeoa na tayari umeshalipa mahali umekabidhiwa mke na mmeanzisha Maisha yako kuna umuhimu wowote wa kuwatumia pesa wazazi wa mwanamke kila mwisho wa mwezi?

Japo ulazima upo kwenye zawadi pale ambapo unaenda kuwatembelea.
 
Sio lazima lkn km wazazi wa mkeo hawana uwezo nawe una nafasi nzuri ni vizuri ukawasaidia angalau hata Mara kadhaa kwa mwaka km wazazi na ndugu zako wengine unawasaidia utashindwaje kusaidia wakwe zako, mkeo hatakuwa na amani kuona yy anaishi maisha mazuri ya kifahali huku wazazi wake wakiwa wanataabika hata jamii itamuona ni mtu wa ajabu,tujitahidi kubalance mambo tusiangalie tu upande mmoja km mkeo anakipato kinachomuingizia pesa sio mbaya ila km mkeo Hana chochote kinachomuingizia pesa jitahidi kujali pia family yake hiyo itasaidia kuimarisha uhusiano wenu ,ukipenda ua penda na boga lake ubinafsi hautakiwi
 
Kupanga ni kuchagua ktk vigezo ambavyo ilikuwa razima awe navyo mwanamke kabla ya kuoa ni uwezo wa familia yake sikutaka kabsa kuoa familia tegemez na ninashukuru mnoo tangu nimeoa sjawh ombwa hata mia zaid huwa natuma vizwad tu.
Hili wazo mimi pia naliangaliaga sana...unakuta wewe mwenyewe una fight life likae mahala tena unapoa uanze kuhudumia ukweni
 
Tuseme mada hii ilivyokaakaa( kwa hisani ya sauti ya Mwanri) ninadhani kuna shida pahala.

Nionavyo mimi ndoa hii haijatulia, imekaa kichumi zaidi maana kuna shinikizo la upande mmoja.

Mkiisha kuoana ni lazima muanzishe kichali (makazi) yenu na hapo ndipo mnaanza mipango yenu.

Hakuna cha ukweni wala ubabani hapo, mmekwisha kuunganisha familia, shida zote zitokazo pande mbili za familia ni zenu.

Kwa hiyo kila shida itokeapo ni lazima mkae mjadili na mpange kwa pamoja namna ya kuwasaidia ndugu zenu pasi na upendeleo wala shinikizo lolote toka upande wowote.

Kukiwa na shinikizo la kulazimisha kutuma hela kila mwezi kwa wazazi ama ndugu wa upande wowote, basi maendeleo kwa ajili ya mustakabali wa maisha yenu itakuwa ni ndoto.

Nimechangia kifupi sana ingawa kuna maelezo marefu hapa.

Na hii nimesemea ni kwa ndoa zilizotulia tu.

Lakini ukikuta kuna kulazimisha kipato chenu ama vitu kutoroshwa kisiri ndani ya nyumba bila ya makubaliano na kwenda kusapoti ndugu wa upande fulani, elewa hapo kuna mgogoro mkubwa sana unafukuta kwenye hiyo ndoa.

Ndoa hiyo haijatulia na kuna mwisho mbaya unasubiria kwa kujua ama kutokujua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina muda mrefu toka nimewapa wakwe pesa ,siku hizi naona wife kila aki ongea na mama yake anaombwa hela tuu na mimi na kula ganzi Kama siwa skii vile!!

Sent from my Nokia C2 using JamiiForums mobile app
 
Jamani swali langu hivi ni lazima kutuma pesa ukweni?

Hivi unapokua umeoa na tayari umeshalipa mahali umekabidhiwa mke na mmeanzisha maisha yako kuna umuhimu wowote wa kuwatumia pesa wazazi wa mwanamke kila mwisho wa mwezi?

Japo ulazima upo kwenye zawadi pale ambapo unaenda kuwatembelea.
Mwanamke wa Tanga huyo
 
I
Acha nidandie treni kwa mbele.

Ukishaoa unaishi maisha yako kwa namna utayokubaliana na mwenzako huku mkochukua tahadhari ya jamii inayowazunguka namna wanavyoishi mnaweza jikuta nanyi mnaishi kama wao japo si sheria.

Kama baba yako yupo, muulize yeye alikuwa anapeleka pesa ukweni?
Kama una kaka wakubwa wailize pia. Kama una dada zako wameolewa muulize mama au baba, shemeji yako anawapa mshiko kila mwezi?

Kuna wanaopeleka matumizi (pesa na vitu) ukweni kila mwezi kwa ridhaa yao kama shukrani kwa kile mkewe anachomfanyia (Mahaba, utamu, mapishi, kujua kulea watoto na ndugu wa mume, anajua bajeti yaani sio mbahili sio mfujaji wa hela, sio mchoyo, hana gubu n.k.)

Hainaga fomula ukikuta unakerwaaa hata ukipigiwa simu na mkwe unajiskia kutukana πŸ˜‚πŸ˜‚

Nimeteremka kwenye treni nililodandia.

Alamsiki.
I love you Kasie matataπŸ₯°πŸŒΉβ€
 
Back
Top Bottom