Ni kweli Wilson Mukama anaandaliwa kumpokea Makamba?

Mkuu Wilson Mkama ni nani ?,anafanya nini, unweza kutuwekea CV yake kwa faida ya wasiomjua kama mimi.
 
WanaJF,
Kuna tetesi zimezagaa mitaani kwamba Bw. Wilson Mukama ndiye anayeandaliwa kumpokea mpayukaji Makamba katika nafasi ya katibu mkuu wa ccm. Tangu wakati wa kampeni mwaka jana hadi sasa Bw. Mukama ambaye ni kada wa muda mrefu wa ccm amekuwa akijitokeza kwenye mijadala kwa njia ya luninga inayohusu mwenendo wa siasa hapa nchini. Ijumaa iliyopita Bw. Mukama alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa kwenye kipindi cha TBC cha This Week in Perspective. Mjadala ulihusu miaka 34 ya ccm. Tafadhali wenye habari zaidi kuhusu tetesi hizi watujuze zaidi. Kama ni kweli je, huyu jamaa ana ubavu wa kushikilia kiti hicho au nae ni mpayukaji tu?
Source of this information please?????????????
 
nataman MAKAMBA aendelee kushikilia hiyo nafasi mpaka 2015,ikiwa ataondoka CDM inabidi waongeze mbinu kakabiliana na CCM
 
Mkuu Wilson Mkama ni nani ?,anafanya nini, unweza kutuwekea CV yake kwa faida ya wasiomjua kama mimi.

Huyu hapa....ndio Katibu Mkuu mpya ajaye

kibonde.jpg
 
Sina uhakika lakini mabadiliko yoyote ya kumtoa makamba yatakuwa mazuri tu!!
 
Mkuu Wilson Mkama ni nani ?,anafanya nini, unweza kutuwekea CV yake kwa faida ya wasiomjua kama mimi.

Huyu jamaa kwa mara ya mwisho alikuwa Katibu Mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji. Lakini amewahi kuwa katibu mkuu pia wa wizara ya afya na naibu katibu mkuu tamisemi. Pia, alikuwa mkuu wa chuo cha siasa cha kivukoni akiwa ametokea kwenue ukuu wa wilaya. Amewahi pia kuwa mkurugenzi wa jiji wakati huo akiwa chini ya Keenja. Ni mzee aliyekulia kwenye chama na amefanya kazi karibu na mzee kingune ngomale mwiru. Kwa sasa ni mwenyekiti Bodi ya TSN inayomiliki magazeti ya serikali ya Daily News na Habari Leo. Nimeambiwa pia kuwa ni mwenyekiti wa mamlaka mpya inayoendesha mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa viktoria mpaka miji ya shinyanga na Kahama. Bahati mbaya jina la mamlaka silifahamu.

Ukweli huyu jamaa ni kifaa. Kwa mabadiliko tunayohitaji Tanzania hawezi kutusaidia. Actually, anayeweza kutusaidia ni mropokaji wa sampuli ya makamba na tambwe hiza.
 
..I think Mukama hawezi kupewa nafasi muhimu namna hiyo maana anazo genes za yule jamaa alietangulia wa Njombe ambaye wamemtelekeza kabisa..
 
Mukama akiwa Katibu Mkuu wa ccm wapinzani wameliwa. Jamaa ni very professional kwenye masuala ya siasa. Ni kada mzima sana katika siasa za nchi hii tangu enzi za akina Nyerere na Kawawa. Inasemekana ni miongoni mwa wajumbe muhimu wa kamati iliyopiga kambi zanzibara kuandaa ilani ya uchaguzi ya ccm ya 2010.
 
Lakini anaweza kuletewa mizengwe na wasiotaka mabadiliko ndani ya chama!
 
Mukama pia alikuwa kwenye kamati ya jaji Kisanga, Nkapa alipowablast kwa kufanya kazi ambayo hawakutumwa, Mukama akawasaliti wenzake kwa kukana kuhusika na ripoti hiyo.
 
Mukama pia alikuwa kwenye kamati ya jaji Kisanga, Nkapa alipowablast kwa kufanya kazi ambayo hawakutumwa, Mukama akawasaliti wenzake kwa kukana kuhusika na ripoti hiyo.

Nakumbuka maneno ya Mkapa siku zile..'kamati ya jaji Kisanga ni batili'.Sasa alikana vipi ripoti kama naye alikuwemo kwenye Kamati?Kwanini asingejitoa kwenye kamati,kabla ya ripoti kusomwa/kukabidhiwa kwa Rais?
 
Kwa mabadiliko tunayohitaji Tanzania hawezi kutusaidia. Actually, anayeweza kutusaidia ni mropokaji wa sampuli ya makamba na tambwe hiza.[/QUOTE]

nakubaliana na wewe kabisa

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom